1st AID
JF-Expert Member
- Jul 29, 2014
- 1,079
- 523
Kabla sijaangalia chanzo (ambacho sikijui) cha kwanini mke kuamua kuwa msiri kwenye mali zilizopo kwenye ndoa. Tuangalie vipengele hivi viwili kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971, pamoja na kwamba ndoa ni swala la kiutamaduni lakini sheria inahusika.
1.Haki ya Mgawanyo wa mali za familia/Ndoa.
Mali yoyote ambayo imepatikana wakati wa uhai wa ndoa na kwa nguvu na au machango wa pamoja wa wanandoa. Iwapo mali iliyopatikana na mwanandoa mmoja wapo kabla ya ndoa au kwa nguvu zake mwenyewe lakini imeboresha/imetunzwa na mwanandoa mwingine mali hiyo itatambulika kama mali ya ndoa.
2. Aina za mchango.
Kutekeleza kazi nyumbani hasa kutunza familia; mfano kuosha vyombo, kupika, kufua nguo, kubeba maji na kazi zingine zinazofanana na hizo kwa maslahi ya familia.Kutunza mali za ndoa: mfano kufyeka, kulima, kuvuna shamba, kufanya marekebisho ya mali za ndoa kwa maslahi ya familia.
Mchango wa fedha wa mwanandoa katika kununua mali.
Lakini kama kuna mali yoyote ambayo mwanandoa mmoja amempa mwanandoa mwenzake kama zawadi, mali hiyo itakuwa ya yule aliyepewa pekee.
Narudi kwenye uzi kwanza sioni sababu ya kwanini jamaa achanganyikiwe, kama ndoa yao ina umri huo mdogo wa miaka minne na kumeanza usiri kama huo lazima kuna tatizo mahali. Kuna weza kuwa na tatizo kwa mume uwenda hana mipango ya kimaendeleo ambayo mwenza wake kahisi kwamba kwa kuendelea kuwa wazi wanaweza kuishi kwa pato la kusua sua na hivy akaona afanye njia mbadala.
Pili nafikiri ameona adai kwamba mali hiyo ni yake peke yake ili kuweza kuendelea kuitunza dhidi ya matumizi mabaya ya mumewe!? Tusihukumu kabla ya kujua upande wa pili.
Nadhani mali hiyo plus mradi mumewe hakumpa kama zawadi, so no wasiwasi hapo. hizo ni njia mbala za wanawake wenye akili kuongeza pata bana.