Mwenyekiti Wa Ukombozi Na Ufahari!

" By W. J. Malecela

"Mwenyekiti wa Chama cha kuwakomboa wananchi, anapotumia magari kama ya watawala, ..................."
Yapi ni magari ya watawala?
Labda unisaidie ili nitambue magari ya watawala ya viongozi wa vyama na ya raia wa kawaida.
 

Mbona hujasema maisha ya Mzee wako Malecela anavyokula pensheni ya jasho letu na kutumia kila kitu bure.
Kumbe NYANI HAONI KUNDULE, ndio maana walikushiti katika Bunge la Afrika Mashariki. Maisha yetu hayawezi kurekebishwa na kutotumia gari moja la MBOWE na kutumia magari elfu yaliyopo serikalini, Mbona watu wa MVUMI ni waelewa sana tofauti na wewe.
 
Ikiwa vigezo vya uongozi ni magari! si hasha ukashindwa kuwa "convince" Dodoma kukupeleka Arusha.

Natamani mada ingekuwa; anaeaminisha watu kuwa kafilisika kwa kushindwa kulipa fedha za walalahoi alizokopa NSSF anatamba na ma VX 8.
 
Mimi nimeshindwa kuelewa hoja anayoijenga William. Je ni kosa kwa Mtu kama Mbowe ambaye ni mfanya biashara kununua gari aina ya VX? Hivi kweli kwa mtu anayemiliki biashara kama zake, hatashindwa kununua gari kama hilo. Kitu ambacho William ameshindwa kukisema hapa ni kuwa Mbowe amerudisha gari na mwenyekiti wa upinzani alilopewa na serikali. Kwani anaona gari hilo ni gharama tuu kwa serikali masikini kama yetu.

Inabidi tuachane na haya mawazo potofu ya kuwa kusudi mtu hawatumikie wananchi lazima awe masikini. Watu wanachopinga sio mtu kutumia hela yake, bali matumizi mabovu ya hela za serikali.

Kwenye suala la Savimbi, William anadai tunaangalia mazuri yake tuu. Hivi ndivyo tunavowajudge watu siku hizi? Na vile vile anamsifia Idd Amini. Kweli ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni! Savimbi alikuwa ni mtu mshenzi na mzandiki ambaye hata siku moja hawezi kutumika kama kioo cha jamii. Sitashangaa nikisia William anamsifia Hitler kwani naye kuna mambo mazuri aliwahi kuyafanya.
 

Sijui kama huyu baharia amesoma hili jibu! But it is well put forward. Naweza kusema kuwa limetoa summary ya majibu ya wengine wote na hata wale walioishia kumtukana huyu bwana. Safi sana...
 
wily ni kilaza 2 wewe, kawashike wapuuz wenzio kwenye kijiwe chako huko, blog,, ulioanzisha ndo kijiwen kwako co hapa,, nyambafuuu teh teh teh
 
 
watoto wa vigogo mmekuwa vinara wa anasa mnajifanya nyie hii nchi ya kwenu pekeenu et ee? Mmekuwa mabingwa wa methal misemo na vitendawil ikulu na kwenye majumba ya anasa na makasino pole yenu, mtakipata dc seazon
 

Ngongo:

Hii misemo ya Kiswahili:
Kipenda roho hula Nyama mbichi. na
Ukipenda Chongo utaiita Kengeza.
Kwavile jamaa wameipenda CDM basi isijadiliwe wala Isikosolewe!
Hata pesa kama zatokana na Wanachama kuna kila sababu zitumike vizuri, hasa ukizingatia Umaskini na Udhaifu wa Wachangiaji wenyewe.
Ni juzi tu CDM walidai wafuasi wao hawana nauli za daladala. Na kuwataka waunde Maandamano toka watokako kwenda Jangwani.
Kwa hiyo mfano tunaouona hauna tofauti na Ufahari unaopigiwa kelele wa CCM na Serekali yake. Hata Bw Yesu alifundisha kwa Mifano na tena akasema "Utaujua mti kwa Matunda yake"
Kwa hiyo anachotahadharisha Willim ni kuwa " samaki akunjwe angali Mbichi" au Kuna hatari ya kjikuta mmetoa Chui mdogo shimoni na kuingiza Mkubwa!
 
Point za William iko wazi kwa chama kinachotaka mabadiliko ya kumkomboa Mtanzania, hasa masikini wa kijijini. Ajabu kubwa sana Pro CDM wengi waliojibu au pro-Chairman wamakwepa kuijibu, na majibu yao mengine ukiyasoma yanakufanya ufikiri ni yupi haswa anayelipwa kuandika mambo yasiyo namsingi, Je ni mtoa mada au huyu mpinga mada ambaye naye anajiona ni sehemu ya ukombozi wa nchi.
 

Bravo mkuu!
Hawa ndio watanzania, wanaoaminishwa kuwa chadema au ccm itawakomboa! Kwangu ni sawa kuchukua maji ya betri, ili kusafisha jicho lililoingia mchanga. Ni wazi utakuwa kipofu tu! Ndicho kinachoenda kututokea, soon!
Mungu wetu anaita!
 
Kwakuwa huyu Baharia kasema picha ndio zinaongea zaidi basi mimi sina la kusema, lakini nina uhakika gari hili hata leo hii huwezi kulinunuwa kama huna mshiko wa kueleweka.

 
Yaani huyu mvuta Bangi anaburuza Escalade halafu unamshangaa Mbowe kuwa na gari mtumba la Dubai? kweli laana ya Nyerere itawaandama kizazi chenu chote.

 
Mkuu Sangara,

Pamoja sana afadhali wewe umekuja na majibu ya maana kidoooogo ingawa matumizi ya ruzuku ya CDM hatujaelezwa kama ilitumika kununua haya maV8 au ni wivu unawasumbua wapinzani wa CDM.Kimsingi nakubaliana kabisa na maelezo yako bado nasubiri kanusho kutoka kwa kiongozi wa CDM kwamba chama hakihusiki kwa namna yoyote na manunuzi ya maV8s na kwamba waTanzania wakikipa ridhaa ya kuongoza hakitanunua magari ya kifahari.

Kwakuwa mpaka sasa hakuna kanusho bado naendelea kuamini ruzuku ya CDM ambayo chanzo chake ni kodi zetu imetumika vibaya na ni mategemeo yangu wote waliohusika kufuja kodi zetu wataadhibiwa kwa mujibu wa taratibu na kanuni za chama.


 
Nimeamini jamaa hakufikiri vizuri kabla hajaanzisha huu uzi.......
kwa hiyo anataka kusema tubaki ccm kwa vile chadema itakuwa kama ilivyo ccm sasa?
apeleke hoja za kipuuzi mtera akashee na lusinde sio hapa jf
 
tatizo ni kwamba hujui nyakati zikoje will, coz harakati za 60's, 70's, 80's, and 90's kifupi harakati za 20th century haziwez kufanana hata kidogo kutokana na utandawazi uliopo usitegemee kuona wakomboz wa leo hii wanatembea kwa miguu km akina savimbi na wote uwajuao, also wakomboz wa leo hawawez kuish nyumba za nyasi km akina savimbi na castrol and watsoever kutokana maendeleo yaliopo sasa, kutembelea ma vx8 inategemea na source ya icome iliyotumika kupurchase hayo magari, talkin abt mboe unachemsha kabisa coz ni personal fund inayotumika kitu ambavho ni contrary to ccm ambao wanatumia magari yatokanayo na fedha za watanzania, so km kiongoz anayepigania ukomboz wa watanzania anajitolea kwa hali na mali kutumia mali zake hata katika shughuli za kichama hii inastahil pongezi sana, sio km akina mkapa, mwinyi , na vigogo wengi tu ambao pamoja na kustaafu still bado wanatumia magari ya walipa kod yaani it is so shame to me kwa hawa watu, so bwana will u hav to tink big b4 u say tins like this coz unadhid kutudhihirishia kuwa hata kushindwa kwako EA kunatokana na kuwa they knew dat u cant be a gud representative of our country coz u cant tink big. caution avoid ur poorly tinking arguement. dem ................. t will
 
Ben, swali la kujiuliza ni je nini kimefanyika mara baada ya yeye kuondoka hapo?Mtu kama rais akitembelea sehemu kama hiyo ni lazima ajuwe kama kuna kilichofanyika(endapo kuna maagizo yoyote aliyoyaacha) mara baada ya yeye kuondoka.

Kwenda kuwatembelea wananchi kihivyo si ni kama ni mgonjwa umeenda kumtembelea hospital ukijuwa ataendelea na matibabu? Ameenda kuwapa pole kwa umasikini ama kwenda kuhamisisha maendeleo ili kuondoa umasikini?

Hao wananchi walimweleza nini?Na yeye alisema nini?Ama aligawa pesa na kandambili?

Mtoto anayempa lawalawa, ni bora angempa zawadi either ya kitabu ama mpira, na aache maagizo ya shule/madarasa, maktaba ya kujisomea, ama hata uwanja wa watoto kucheza mpira nk.

Hii nchi bana.

Kwakifupi ndugu William, uongozi ni matendo, nakubaliana kwa kiasi flani na hoja yako, lakini uwakilishaji si mzuri.

Ni kweli wananchi wetu ni masikini sana, na viongozi ni lazima wajaribu kureflect hilo, siasa haitakiwi iwe kitu cha kukimbilia, especially kwenye nchi ambayo inahitaji ukombozi kwenye kila nyanja, you name it.

Kuna kama "ganzi" flani hivi ambayo ukiwa hapo bongo unakuwa "a victim of" bila kujitambua.Ambayo inaweza kutafsiriwa na wengine kama "a dont care mentality"

Kama kweli nchi yetu ni masikini kiasi hiki, basi si kila jambo la kuiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…