Mwenyekiti wa Taasisi ya Imamu Bukhary Sheiky Khalifa Hamisi anashikiliwa na Polisi

Mwenyekiti wa taasisi ya Imamu Bukhary Sheikh Kahalifa Khamisi anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kutokana na press conference ya juzi.

Polisi wanataka kujua kwanini aliunga mkono kauli ya Lowassa na pia kwanini aliwataka Waislamu wote nchini kuungana kutetea haki za waislamu waliopo Magereza.

Mbona majibu ya maswali ya polisi kama yapo wazi. Sababu ni yeye kuwa muislamu, na Lowassa aliongelea uislamu, wale walioko magerezani baadhi yao ni waislamu, halafu basis ya majibu haya atawaambia ndivyo Quaran tukufu na mafundisho ya Mtume Muhammad yanavyoelekeza. Sasa polisi wakitakakwenda mbele zaidi inabidi waishambulie basis ya kauli zake kitu ambacho ni kigumu kwa secular government.
 
Hii zaidi ya kagame...maana huyo hu deal na wagombea urais zaidi....wengine hashughuliki nao
 
Kwa hiyo hata kama kuna njama za kutaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha dini au siasa Serikali ikae kimya tuu?. Au watu wakiuawa pasipokuwa na hatia serikali upuuzie tuu. Hilo halitakuja kuwezekana hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app



Tatizo lako ndugu yangu umelishwa maneno, na umeshindwa kujiuliza maswali ya msingi
1. Kama kuna njama na ushahidi upo kwanini wasipelekwe mahakani??
2. Kama ushahidi haujakamilika ni upelelzi gani wa miaka mitano? au basi jeshi letu la polisi liwe wazi kuwa halina weledi wa upelelezi??
3. Na kama ni hivyo kwanini wasiombe msaada basi mbadala na kuwatesa raia wake?
4. Pia wale ni watuhumiwa tu bado hawajakutwa na makosa yeyote hivyo kwanini basi wateseke?
Busara iwe inakuongoza katika kufukiri na kufanya maamuzi yako.
 
Back
Top Bottom