Mwenyekiti wa kwanza/muasisi wa CHADEMA ana mamlaka gani kikatiba kwenye chama?

Gagnija

Platinum Member
Apr 28, 2006
11,849
10,432
April 2014 kwenye bunge la katiba, Tundu Lissu alitoa mashambulizi makali sana kwa baba wa taifa Mwl Nyerere. Moja ya mashambulizi hayo ni madai kuwa mwalimu alizoea vya kunyonga, hivyo asingeviweza vya kuchinja.

Mashambulizi hayo yaliwaudhi baadhi ya watanzania, akiwemo mzee Mtei aliyelazimika kutoa karipio kali kwa Lissu na kuonya kuwa iwe mwiko kwa mwanachadema kumtukana mwalimu.

2014 Mtei hakuwa kiongozi wa Chadema, hilo karipio alilitoa kwa mamlaka gani aliyonayo?

Karipio lenyewe hili hapa:
"Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa".
 
Mh. Mzee wetu MTEI si lazima awe kiongozi bali kwa yeye kama moja wa wazee wanaojua kipi Mwalimu amechangia mpaka hapa tulipo alikuwa sahihi.

Tofauti na Lissu sehemu kubwa ya maisha ya mwalimu amesimuliwa na kushuhudia sehemu ndogo mno ya mapambano ya enzi.

#NB MWACHE MZEE MTEI AZEEKE SALAMA

Vijana anzeni Mapambano walipoishia wazee.
 
Mh.Mzee wetu MTEI si lazima awe kiongozi bali kwa yeye kama moja wa wazee wanaojua kipi Mwalimu amechangia mpaka hapa tulipo alikuwa sahihi.

Tofauti na Lissu sehemu kubwa ya maisha ya mwalimu amesimuliwa na kushuhudia sehemu ndogo mno ya mapambano ya enzi.

#NB MWACHE MZEE MTEI AZEEKE SALAMA

Vijana anzeni Mapambano walipoishia wazee.

..Lissu ame-experience sera mbaya za Kijamaa na Operesheni Vijiji za Mwalimu Nyerere.

..Kwa hiyo anapomkosoa anajua nini anachokisema.

NB.

..Lissu aliteleza siku alipochangia kuhusu Mwalimu Nyerere na Muungano ktk Bunge la Katiba.
 
..Lissu aliteleza siku alipochangia kuhusu Mwalimu Nyerere na Muungano ktk Bunge la Katiba.
Hakuteleza; alisahau kwamba wenye chama wakati wanahangaika kukijenga yeye alikuwa anabeba mabegi ya Mrema nccr hadi 2004 chadema ilipoanza kung'aa.
 
Heshima Yako Mkuu
 
Hakuteleza; alisahau kwamba wenye chama wakati wanahangaika kukijenga yeye alikuwa anabeba mabegi ya Mrema nccr hadi 2004 chadema ilipoanza kung'aa.

..angekuwa active ktk siasa za Nccr tungemjua tangu akiwa huko.Lissu amejulikana akiwa nje ya Nccr.

..Ungeaminika zaidi kama ungesema alikuwa mbeba mikoba wa kambi ya Mabere Marando ambayo ilikuwa na wasomi wanasheria.
 
..Ungeaminika zaidi kama ungesema alikuwa mbeba mikoba wa kambi ya Mabere Marando ambayo ilikuwa na wasomi wanasheria.
Issue ni kwamba yeye na huyo Marando wameingia chadema ikiwa tayari inang'aa.

Mzee Mtei alichofanya hadi kumjulisha katiba na sera kupelekwa Butiama 1992, ilikuwa kumkumbusha kuwa hivyo alivyoviona vinaelea 2004 kuna watu walihangaika kuviunda awali.
 
..Chadema ya Mtei ilikuwa hoi bin taaban.

..Prof.Baregu aliombwa kuwa mgombea Uraisi akaingia mitini.

..Chama kilipata nguvu mpya baada ya Mbowe kuwa Mwenyekiti na ku-recruit wanaharakati mbalimbali, akiwemo Lissu, pamoja na vijana toka chuo kikuu kama Zitto, Mdee, Mnyika, etc.
 
..Chama kilipata nguvu mpya baada ya Mbowe kuwa Mwenyekiti na ku-recruit wanaharakati mbalimbali, akiwemo Lissu, pamoja na vijana toka chuo kikuu kama Zitto, Mdee, Mnyika, etc.
Zitto kaenda kusoma chuo kikuu akiwa tayari mwanachama wa chadema. Ni Zitto huyuhuyu anayebezwa leo aliyehamasisha vijana nchini, hasa vyuoni, kujiunga chadema.
 
Zitto kaenda kusoma chuo kikuu akiwa tayari mwanachama wa chadema. Ni Zitto huyuhuyu anayebezwa leo aliyehamasisha vijana nchini, hasa vyuoni, kujiunga chadema.

..ni kweli Zitto ametoa mchango mkubwa kuijenga Chadema.

..kuhusu kuondoka kwake Chadema sina uhakika lawama ziende kwa Zitto, au viongozi, na wenzake aliowaacha ktk chama.
 
Back
Top Bottom