Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kuchaguliwa Desemba 18 mwaka 2019, fomu zaanza kuchukuliwa

Mbepo yamba

JF-Expert Member
Aug 5, 2012
1,110
1,475
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani hapa nchini na mabingwa wa demokrasia kwa kuiiishi, leo kupitia Karibu Mkuu Vincent Mashinji, kimetangaza rasmi kufungua mchakato wa kupata wagombea watakaochuana kwa nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho kitaifa.

Fomu za wagombea wa nafasi hizo ikiwemo Mwenyekiti wa chama, zimeanza rasmi kutolewa siku ya leo ambapo uchaguzi mkuu huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na wafuatiliaji wa masuala ya siasa za ukanda huu wa Africa Mashariki unatazamiwa kufanyika tarehe 18 December, ukiwa ni takribani mwezi mmoja kamili tangu zoezi la kuchukua fomu na kurudishwa lilipotangazwa.

Tunawatakia kila jema kuonesha ukomavu mkubwa wa demokrasia
 

Attachments

  • New Doc 2019-11-18 11.35.53.pdf
    647.1 KB · Views: 1
Sasa kazi kwa CCM kutafuta mamluki wao wawapandikize chamani. wajitahidi sana kabla ya muda wa kuchukua form kuisha.
Note! Huku hakuna kukatana hovyo kwa vigezo vya kijinga. CCM nafasi yenu hii ya kumng'oa Mbowe na vibaraka wake. changamkieni fursa kabla ya muda kuisha.
hapo ume nena. maana hawachelewi kupandikiza watu wao. au kuwazimia taa ili wapigane.. nakimbuka enzi za NCCR kule Tanga..
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vicent Mashinji leo November 18, 2019 ametangaza rasmi siku ya Uchaguzi Wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

“Tutakuwa na Mkutano Mkuu wa Taifa itakuwa December 18, 2019, tushapeleka mialiko kwa watu mbalimbali, katika miongoni mwa mambo tutakayoyafanya siku hiyo ni kuchagua Viongozi wakuu wa Chama” Katibu Mkuu CHADEMA Dkt. Vicent Mashinji

Mchakato tunaoanza nao ni kuchukua na kurudisha fomu za Wagombea, huu mchakato unaanza leo November 18, 2019.

Wote ambao wangependa kugombea nafasi mbalimbali wanakaribishwa kuja kuchukua fomu, kujaza kwa ufasaha na kwenda kugombea” Katibu Mkuu CHADEMA
 
Viva Chadema. .. kigingi cha mpingo kwa CCM na vibaraka wao...
Tuna imani mtatuletea viongozi bora kabisa..
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Safi Sana. CHADEMA inaiishi demokrasia ya kweli. Chadema hakuna nafasi yoyote hata ile ya mwenyekiti ambayo itagombewa baina ya mtu na kivuli. Ni mtu kwa mtu/watu. Hongereni sana CHADEMA
Mbona CCM kwenye uenyekiti wanaogopa hata kuweka kivuli? Ushawahi kuona wewe wameweka kivuli?
 
Back
Top Bottom