Mwenyekiti wa CCM umetuumbua

Mwenyekiti wa CCM umetuumbua

Hahaaa hyo ndio maana ya transparency kwenye uchaguzi, mtu ka Gwajima haamini macho yake
 
Huyo hapo alivyo yapokea matokeo yake pale kawe
Hahaaa hyo ndio maana ya transparency kwenye uchaguzi, mtu ka gwajima haamini macho yake
Screenshot_20200721-173145.jpeg
 
Hapana kaka, hili limetudhalilisha na kutufedhehesha sana.....yaani number ya kiatu igeuke iwe ndiyo idadi ya kura no no no no....!!
Wamevuna walicho kipanda maana wamepanda chuki na matusi wakati wakihama kutoka cdm
 
Hiyo itakuwa powa sana hata kama mtu unashindwa unakuwa na imani ya kilicho tokea.
Muda wa kuipata haupo kwa sasa bali tuombe kura zihesabiwe pia kituoni na majibu tupewe peupe kuondoa malalamiko na mafindofindo
 
Hiyo itakuwa ni bora kuliko hata mambo ya tume huru ya kiujanja ujanja
Tunataka hata kura za uchaguzi mkuu October 28 kura zote kila jimbo zihesabiwe kwa uwazi namna hii kama alivyoolekeza mwenyeketi wa CCM.
 
Hapana kaka, kugombea ni haki ya kila mwanachama....sasa kitendo cha kutangaza hata sisi wa zero, 1, 2 hadi 6 ni aibu. Haya ni majibu ya tezi dume jamani.

Miaka ya nyuma tulikuwa tunatangaza watatu tu wa mwanzo ilikuwa inatosha ili kukilinda chama.
Nimekuelewa mkuu
 
Muda wa kuipata haupo kwa sasa bali tuombe kura zihesabiwe pia kituoni na majibu tupewe peupe kuondoa malalamiko na mafindofindo
Je mawakala hawatanunuliwa au hawataondoshwa vituoni wakati wa kuhesabu kura?
Uzalendo kwa nchi kwanza
 
Ndio mkome. Siku nyengine Kabla ya kuchukua formu mtajitathmini Kwanza Kama unatosha au la kwa nafasi unayoomba. Sio mnakurupuka kuchukua formu tu.
 
Kati ya makosa makubwa aliyo yafanya ndio hilo
Huyo naye atulie Sasa kapoteza ushawishi wake kwa jamii na hii mikaganyiko ya siasa, badala aombe kura anainanga CDM
 
Kama mulikwenda kutaka uongozi.. hamutakiwi kuumizwa na hayo madogo.. kikweli wa ubunge au kutaka teuzi baadae.. basi hayo vijimaneno.. hayatawasumbua.. bali mutafanya mazuri.. juu yenu kujiongeza.. muwapuruvu sivyo wanavyofikiri.. chukueni kama challenge ya mazuri mbele..
 
Kati ya makosa makubwa aliyo yafanya ndio hilo
Sikuhizi kila mtu ana mdharau tu asifikiri kipindi ana mashabiki wengi enzi za ukawa na Sasa ni sawa, atulie kimya na ile video ndio imeharibu haswa
 
Back
Top Bottom