Mbuzimtu
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 355
- 178
Watu wengi walitegemea kutakaswa kwa chama hicho kupitia hotuba ya mwenyekiti Jana. Baada ya hotuba yake jana, ni dhahiri kuwa mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya chama cha mapinduzi ni mwenyekiti wa chama hicho.
Wakati chama kikizidi kupoteza mvuto mbele ya macho ya watanzania, hakuna juhudi za makusudi kukinusuru chama hicho. Hotuba ya mwenyekit wa CCM kwa wazee wa Dar es salaam ilikuwa nafasi adimu na pekee ya kukiinua chama na kurejesha mvuto kwa watanzania. Kilichotokea jana, mwenyekiti, kuamua kupiga danadana kwa namna tofauti kwenye skendali ya Escrow. Kusema Mhongo anawekwa kiporo ni kukiangamiza chama. Kushindwa kumwajibisha Maswi moja kwa moja ni kukiua chama. Mbaya zaidi, ni pale alipomwajibisha Tibaijuka ambaye ni mnufaika wa mbali sana katika skendali hii.
CCM kama chama itasema nini mbele ya watanzania?. Kwanini chama kikose mvuto kwajili ya watu wawili?. Nani mwenye ujasiri wa kuinadi CCm mbele ya watanzania wa leo baada ya hotuba ya jana?.