Mwenyekiti wa CCM taifa anaua chama

Mwenyekiti wa CCM taifa anaua chama

JK katumwa kuja kuiuwa CCM

Unaweza ukawa uko sahihi, maana mkapa kazi yake ilikuwa kuua nguvu za kifedha za nchi, uuzaji wa Nbc. Chama hiki kulikuwa kikwazo kwa harakati za kuzuia uporaji wa rasilimali za kusini mwa Africa enzi hizo.
 
Amini usiamini utaanza kufa wewe na kuicha ccm ikiwa hai ikiwatumikia watanzania kwa ari zaidi na nguvu zaidi.

hivi watu wa ccm mbona hamna mshipa wa aibu kwa wizi wote huu mliotufanyia wmnapata wapi ujasiri wa kuongea hadharani.
 
Nashukuru sasa hiv wife anaichukia ccm had naona ananizid jana alinikaripia wakati hotuba ya mzee wa tezi inaendelea eti kisa pale mheshimiwa aliposema ni za iptl sio za umma,aliona bora tuangalie cd ya abiud misholi tupate neno kuliko kusikiliza porojo,sasa had dada wa kazi kamuambikiza kuichukia ccm
 
Watu wengi walitegemea kutakaswa kwa chama hicho kupitia hotuba ya mwenyekiti Jana. Baada ya hotuba yake jana, ni dhahiri kuwa mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya chama cha mapinduzi ni mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati chama kikizidi kupoteza mvuto mbele ya macho ya watanzania, hakuna juhudi za makusudi kukinusuru chama hicho. Hotuba ya mwenyekit wa CCM kwa wazee wa Dar es salaam ilikuwa nafasi adimu na pekee ya kukiinua chama na kurejesha mvuto kwa watanzania. Kilichotokea jana, mwenyekiti, kuamua kupiga danadana kwa namna tofauti kwenye skendali ya Escrow. Kusema Mhongo anawekwa kiporo ni kukiangamiza chama. Kushindwa kumwajibisha Maswi moja kwa moja ni kukiua chama. Mbaya zaidi, ni pale alipomwajibisha Tibaijuka ambaye ni mnufaika wa mbali sana katika skendali hii.

CCM kama chama itasema nini mbele ya watanzania?. Kwanini chama kikose mvuto kwajili ya watu wawili?. Nani mwenye ujasiri wa kuinadi CCm mbele ya watanzania wa leo baada ya hotuba ya jana?.

Huu ni mpango wa Mungu ili nchi iendelee kukombolewa. Muhongo yeye aendelee kukalia kiti chake tu maana wananchi ndiyo wanazidi kuona kiburi ya DHAIFU pamoja na chama FISADI.
 
Hiyo ndiyo sura halisi ya CCM kuwa ni chama cha kutetea mafisadi
 
Nashukuru sasa hiv wife anaichukia ccm had naona ananizid jana alinikaripia wakati hotuba ya mzee wa tezi inaendelea eti kisa pale mheshimiwa aliposema ni za iptl sio za umma,aliona bora tuangalie cd ya abiud misholi tupate neno kuliko kusikiliza porojo,sasa had dada wa kazi kamuambikiza kuichukia ccm

uyo wife wako ni mchaga?
 
Back
Top Bottom