Mwenyekiti wa CCM taifa anaua chama

Mwenyekiti wa CCM taifa anaua chama

CCM imeuawa na Kikwete kitambo sana. Yafuatayo yamefanywa na Kikwete kuiangamiza ccm:-
1. Kudandia hoja ya upinzani ya uundwaji wa katiba mpya.
2. Kuyakana maoni ya wananchi juu ya katiba mpya wanayoitaka.
3. Kumteua Nape kuwa katibu mwenezi wa ccm taifa. Najua hili hufanywa na kamati kuu ya chama. Lakini kama mwenyekiti ana mkono wake.
4. Kuendekeza urafiki na uanamtandao katika uteuzi wa viongozi mbalimbali
5. Kuwawajibisha watu wachapa kazi kama Kagasheki kwa kuwa tu amedhibiti maslahi haramu ya marafiki zake
6. Kuogopa kuchukua hatua/maamuzi kwa masuala muhimu ya nchi kama rais. Siku zote anasubiri watu wasemeee mpaka basi ndo anakuja kutoa maamuzi tena maamuzi laini.
7. Kupingana na chama chake ama watendaji wakuu wa chama chake hadharani. Mifano ipo mingi sana nitataja 2 tu.
(a) CCM haikutaka katiba mpya, JK kalazimisha na alikiri hili alipokuwa anakabidhiwa katiba pendekezwa a.k.a katiba ya fisadi Chenge.
(b) Katibu mkuu ccm taifa na katibu wa itikadi na uenezi walizunguka nchi nzima na kuwanadi maziri 6 kuwa ni mizigo na wakamshauri JK awawajibishe. JK aligoma.
(Naomba na ninyi wasomaji kama una la kuongezea hapa fanya hivyo).
Sasa kwa maelezo haya unataka uone nini zaidi kujua kwamba huyu JK ni Golberchiev wa CCM?
 
Katika watu wanaotia aibu wewe huwezi kukosekana jk kaongea mamno ya msingi na yenye mashiko na kuifungua jamii kwa kiasi kikubwa hasa kwa kutoa elimu ya uraia kwa wale ambao walikuwa hawajui undani wake.

jk na wewe wote ni sawa
 
Huyo Reginald Mengi aliyekutuma amekulipa kiasi gani?
 
CCM imeuawa na Kikwete kitambo sana. Yafuatayo yamefanywa na Kikwete kuiangamiza ccm:-
1. Kudandia hoja ya upinzani ya uundwaji wa katiba mpya.
2. Kuyakana maoni ya wananchi juu ya katiba wanayoitaka.
3. Kumteua Nape kuwa katibu mwenezi wa ccm taifa.
4. Kuendekeza urafiki na uanamtandao katika uteuzi wa viongozi mbalimbali
5. Kuwawajibisha watu wachapa kazi kama Kagasheki kwa kuwa tu amedhibiti maslahi haramu ya marafiki zake
6. Kuogopa kuchukua hatua/maamuzi kwa masuala muhimu ya nchi kama rais. Siku zote anasubiri watu wasemeee mpaka basi ndo anakuja kutoa maamuzi tena laini.
7. Kupingana na chama chake ama watendaji wakuu wa chama chake hadharani. Mifano ipo mingi sana nitataja 2 tu.
(a) CCM haikutaka katiba mpya, JK kalazimisha na alikiri hili alipokuwa anakabidhiwa katiba pendekezwa a.k.a katiba ya fisadi Chenge.
(b) Katibu mkuu ccm taifa na katibu wa itikadi na uenezi walizunguka nchi nzima na kuwanadi maziri 6 kuwa ni mizigo na wakamshauri JK awawajibishe. JK aligoma.
(Naomba na ninyi wasomaji kama una la kuongezea hapa fanya hivyo).
Sasa kwa maelezo haya unataka uone nini zaidi kujua kwamba huyu ni Golberchiev wa CCM?
Ndo maana unajiita kigodoro kwa vile hoja zako umezipata kwenye kigodoro
 
Uchaguzi wa SM ulioshirikisha Wananchi Matokeo--
Ccm 47%
Ukawa 53%

Mapingamizi 33%

Ccm Halali ni 47% + 33% = 80%

Ukawa 53% - 33% ongezeko la Mapingamizi ccm = 20%.

Je kulipowekwa Vikwazo ccm wangeshinda kwa 100% kama wananchi wangepewa fursa?
Labda hizo takwimu umepewa kitandani.
 
Watu wengi walitegemea kutakaswa kwa chama hicho kupitia hotuba ya mwenyekiti Jana. Baada ya hotuba yake jana, ni dhahiri kuwa mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya chama cha mapinduzi ni mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati chama kikizidi kupoteza mvuto mbele ya macho ya watanzania, hakuna juhudi za makusudi kukinusuru chama hicho. Hotuba ya mwenyekit wa CCM kwa wazee wa Dar es salaam ilikuwa nafasi adimu na pekee ya kukiinua chama na kurejesha mvuto kwa watanzania. Kilichotokea jana, mwenyekiti, kuamua kupiga danadana kwa namna tofauti kwenye skendali ya Escrow. Kusema Mhongo anawekwa kiporo ni kukiangamiza chama. Kushindwa kumwajibisha Maswi moja kwa moja ni kukiua chama. Mbaya zaidi, ni pale alipomwajibisha Tibaijuka ambaye ni mnufaika wa mbali sana katika skendali hii.

CCM kama chama itasema nini mbele ya watanzania?. Kwanini chama kikose mvuto kwajili ya watu wawili?. Nani mwenye ujasiri wa kuinadi CCm mbele ya watanzania wa leo baada ya hotuba ya jana?.
hesabu za mjinga
 
Ukweli ni kwamba, asilimia 90% ya hotuba ya rais ilikuwa kukanusha uongo na uzushi wa PAC, IPP na mawakala wao kwamba fedha "zilizokwapuliwa" ni Tshs. bilion 306; kwamba fedha za umma ziliibwa; na nchi imetapeliwa. Pesa ya ESCROW haizidi billion 200 - PERIOD! Na fedha hii ni malipo ya IPTL kwa kutoa huduma ya umeme kwa TANESCO/taifa. Asilimia 10% ya hotuba ilikuwa maneno ya siasa ya kunusuru CCM na kumfurahisha fisadi Mengi kwa kumtoa kafara Tibaijuka na kumtisha Muhongo. CCM haiwezi kufa kwa kuegemea uongo na uzushi kama alivyobainisha Rais wetu kwa kutumia ripoti za CAG na common sense!

Maamuzi ya Muhongo yalitokana ya ushauri wa Mwanasheria Mkuu na Hukumu ya Mahakama - hii ni katika misingi ya Utawala wa Sheria. Mlitaka taifa liendelee kulipa mabilioni kwa Mkono na riba kwa kesi zisizoisha? Hivi kuna ubaya gani kwa Muhongo kufanikisha upatikanaji wa umeme wa bei poa kutoka IPTL na kunusuru malipo ya zaidi ya billion 100 ambazo bado IPTL wandeendelea kuidai TANESCO kwa mujibu wa mkataba?

Mwisho kioja kikuu cha jana ni kuona washangiliaji wote baada ya Tibaijuka kuenguliwa pale Diamond Hall ni wanawake. Je? walikuwa wanashangilia kwa kuangushwa mwanamke mwenzao? Au kwa kujua kwamba fedha alizolipwa Tibaijuka ni kwa ajili ya elimu ya watoto wa kike? Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kamati ya ziti ilimsaidia sana kwa kumwondoa yeye sasa inaonyesha yale waliosema kuwa ikulu ilihusika katika hili ni kweli Big Boss kumbe ndiye mastermind wa deal hili anataka sasa tuamini kweli mkwe wa bosi aliyesemwa na Mbunge wetu wa Ubungo Myika,
Uchunguzi wake wa siku mbili wakati anaumwa tezi ni bora kuliko wa kamati iliyokuwa imesheheni wataalamu waliobobea Msanii Hoyee
 
Watu wengi walitegemea kutakaswa kwa chama hicho kupitia hotuba ya mwenyekiti Jana. Baada ya hotuba yake jana, ni dhahiri kuwa mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya chama cha mapinduzi ni mwenyekiti wa chama hicho.

Wakati chama kikizidi kupoteza mvuto mbele ya macho ya watanzania, hakuna juhudi za makusudi kukinusuru chama hicho. Hotuba ya mwenyekit wa CCM kwa wazee wa Dar es salaam ilikuwa nafasi adimu na pekee ya kukiinua chama na kurejesha mvuto kwa watanzania. Kilichotokea jana, mwenyekiti, kuamua kupiga danadana kwa namna tofauti kwenye skendali ya Escrow. Kusema Mhongo anawekwa kiporo ni kukiangamiza chama. Kushindwa kumwajibisha Maswi moja kwa moja ni kukiua chama. Mbaya zaidi, ni pale alipomwajibisha Tibaijuka ambaye ni mnufaika wa mbali sana katika skendali hii.

CCM kama chama itasema nini mbele ya watanzania?. Kwanini chama kikose mvuto kwajili ya watu wawili?. Nani mwenye ujasiri wa kuinadi CCm mbele ya watanzania wa leo baada ya hotuba ya jana?.
Majasiri wa kuinadi na kuisifia ccm hata baada ya hotuba ya JMK wako watatu: Kinana, Nape, na Mwigulu Nchemba.Tena Nchemba atazunguka nchi nzima akitumia chopa.
 
Hili la akina mama kulipuka kwa nderemo na vifijo hata mm liliniacha kinywa wazi. Kumbe wanawake hawapendani kiasi hiki? Walikuwa wanaongozana naye, wanampokea katika hafla tofauti, kumbe kwa unafiki?
JK huyu mama kakukosea nn? Au kakunyima binti yake Kagem ulitaka kuposa? Maana na Kagem kaporomosha mitusi twiter leo mpaka basi.
Are u serious JK? Uchunguzi wa Tibaijuka tu ndiyo umekamilika kati ya wote waliopata mgao wa escrow? Mbona umesema tume ya maadili na takukuru wanaendelea?
 
Naomba Nape aite press conf. kumpongeza Mwenyekiti wake kwa hotuba nzuri
 
Jumlisha na hayo mapingamizi hawajafikisha 80%, achana nao na data zao za uongo hao.
na hiyo 47% waliyopata wamefanya fujo vituo vingine ukawa wameshinda wasimamizi mbele ya polisi wakatangaza ccm wameshinda.
 
Yaani hii laana inayoitwa CCM itakapoondoka kwenye nchi yetu mbona tutakuwa tumeneemeka! CCM ni Chama Cha Mashetani.
 
Anachofanya kikwete anakijua na amekusudia kwa aababu kuu mbili kwa mujibu wa mtu wa karibu na familia ya kikwete:
Kwanza ccm ilimsusia 2010 ndo maana aliitumia familia yake na kila mtz alijua kuwa ikulu ni ya familia
Pili yeye binafsi na familia yake ni wanufaika wakuu wa mgawo wa escrow hana uwezo wa kuwatosa wengi coz hana namna nyingine ya kuwanusuru wkt kipindi chake kinaelekea ukingoni.
Tatu alichokuwa anakimbilia ikulu tangu ujana wake amekipata ambacho ni kupiga dili za biashara ikiwemo kuuza tembo kwa rais mwenzake wa china kwa fadhila ya uprofesa, kula ujana na kupiga totozi(hii nimeongeza mm).
 
Ukweli ni kwamba, asilimia 90% ya hotuba ya rais ilikuwa kukanusha uongo na uzushi wa PAC, IPP na mawakala wao kwamba fedha "zilizokwapuliwa" ni Tshs. bilion 306; kwamba fedha za umma ziliibwa; na nchi imetapeliwa. Pesa ya ESCROW haizidi billion 200 - PERIOD! Na fedha hii ni malipo ya IPTL kwa kutoa huduma ya umeme kwa TANESCO/taifa. Asilimia 10% ya hotuba ilikuwa maneno ya siasa ya kunusuru CCM na kumfurahisha fisadi Mengi kwa kumtoa kafara Tibaijuka na kumtisha Muhongo. CCM haiwezi kufa kwa kuegemea uongo na uzushi kama alivyobainisha Rais wetu kwa kutumia ripoti za CAG na common sense!

Maamuzi ya Muhongo yalitokana ya ushauri wa Mwanasheria Mkuu na Hukumu ya Mahakama - hii ni katika misingi ya Utawala wa Sheria. Mlitaka taifa liendelee kulipa mabilioni kwa Mkono na riba kwa kesi zisizoisha? Hivi kuna ubaya gani kwa Muhongo kufanikisha upatikanaji wa umeme wa bei poa kutoka IPTL na kunusuru malipo ya zaidi ya billion 100 ambazo bado IPTL wandeendelea kuidai TANESCO kwa mujibu wa mkataba?

Mwisho kioja kikuu cha jana ni kuona washangiliaji wote baada ya Tibaijuka kuenguliwa pale Diamond Hall ni wanawake. Je? walikuwa wanashangilia kwa kuangushwa mwanamke mwenzao? Au kwa kujua kwamba fedha alizolipwa Tibaijuka ni kwa ajili ya elimu ya watoto wa kike? Mungu Ibariki Tanzania.

Ww ni sawa na mbwa!!!!!!
 
Back
Top Bottom