Mwenyekiti CCM K'njaro naye aanguka jukwaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti CCM K'njaro naye aanguka jukwaani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Aug 24, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  SIKU tatu baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kuishiwa nguvu wakati akizindua kampeni za Uchaguzi Mkuu wa chama hicho akiwa jukwaani, jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Vick Siro Swai, naye aliishiwa nguvu jukwaani na kuelekea kuanguka kabla ya kuokolewa na wasaidizi wake wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani katika Jimbo la Hai.

  Tukio hilo lilitokea kwenye uwanja wa CCM eneo la BomangÂ’ombe muda mfupi baada ya mwenyekiti huyo kuanza kuwanadi wagombea udiwani.
  Baada ya kukutana na kadhia hiyo ya kiafya, mwenyekiti huyo alipumzishwa kwa muda wa dakika 30 na baadaye kupewa maji ya kunywa kabla ya kurejea tena.

  Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku tatu baada ya Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kuishiwa nguvu wakati akizindua kampeni za chama hicho kwenye viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, kabla ya kusaidiwa na wasaidizi wake.

  Aliporejea kuhutubia jukwaani alisema alipatwa na tatizo hilo kutokana na kushikwa kiu na baadaye aliendelea kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Fuya Kimbita, ambaye anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

  Mama Swai alisema CCM inategemea kuendesha kampeni za amani na utulivu na haitarajii kusukumwa kwa ajili ya kuchukua hatua za kujihami endapo watafanyiwa vurugu.
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tunampa pole. Tunamuomba Mungu ampe afya njema
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwaka huu wale wote watakaosimama kwenye majukwaa ya kampeni kuomba kura, huku wakiwa ni mawakala wa kuzimu, watapata aibu ya kukata na shoka.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Pole na swaumu Mama Swai....:confused2:
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inawezekana manga wao mmoja:smile-big:
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Hakuna video clip yake.....I bet naye alisema aisee!!!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  naona wataalam wataileta tu hiyo clip

  aisee....

  sijui tusubiri wa wapi sasa... hizi tactics zinasaidia nini?
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Aisee, kusimama jukwaani huku unahofu ya kuona utakayo kuyasema ni ya uongo mtupu, ni lazima uishiwe nguvu kwa vile hata dhamira ina kusuta
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwani nae kafunga?
  Baadae itakuwa ndo style ya kukonga nyoyo za watu.
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  :tea:
  Au huyu mama alidhani hii ni sera mpya kuanguka jukwaani ili upate kura za huruma?....I say!!!
   
Loading...