Mwenyekiti BAVICHA na Redbridge CHADEMA ajiunga CCM

Watanzania huyu ni tapeli amejiunga leo ccm na amejitangaza kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Bavicha (W) Kinondoni...mpuuzeni amewatapeli Uvccm, Mwenyekiti wa Bavicha (W) Kinondoni ni Mm Benjamin Kambarage sijahama, sijahamia na sina mpango wa kwenda ccm..
 
Mastermind wa CCM kwenye huu mkakati wa kumuondoa Mbowe sio smart anamaanisha hata Mwanachadema wa ukweli aliyekua na mawazo kama ya kwao kuhusu Mbowe aone umuhimu wa kubaki Mbowe!Toka lini adui yako akapenda maendeleo yako
Wapumbavu tu hao... CCM kama wamekereka na mwenyekiti kukaa muda mrefu wakaanze na kina Cheyo na Lipumba.. maana hao ndio wamekubuhu kwa kukaa muda mrefu. Lipumba alijiondoa uenyekiti CUF ila CCM ikamrudisha uenyekiti kwa sababu yuko nao.. Uenyekiti wa Mbowe unawapa taabu sana na wataendelea kupata taabu saana!
 
Kama kinakufa hofu ya nini,chaguzi huru? Waacheni wananchi waamue.Msiwachagulie
Tutasema kwa sababu Ruzuku ni pesa za kodi zetu.
Uchaguzi ni pesa za kodi zetu.

Msajili wa vyama analipwa na pesa za kodi zetu.
Na vyama vinatushawishi ili viingie madarakani kusimamia rasilimali zetu.

Sasa haiwezekani kuwa na chama cha MTU binafsi kwa mgongo wa walipa kodi.

Na kama Mbowe atangangania kwenye uenyekiti wa chama ambacho watu wengi mpaka sasa wameuawa kwa kutetea uhai wa chama halafu yeye analeta usultani basi akabaki huko nyumbani kwake na familia yake lakini sio kuzunguka kuhamasisha watu wanapigwa risasi ili tu ajione fahari kutembea na mabodigadi mgongini wakati chama ni kimebaki kama kamati ya send off.

Mbowe asijidanganye kuwa chadema ikifa itarudi tena.
Sio kwa utawala huu wala ujao.
Labda kizazi kijacho lakini sio hiki.

Mbowe mwenyekiti gani hana agenda mpaka utokee msiba ndio utamsikia.

Makosa mengi sana ya watendaji yanafanyika ambayo yapo kisheria kabisa wala hayahitaji maandamano ,ni suala la kwenda tu mahakamani. Ujue mbowe ni Pandikizi niambie ni lini mbowe amefanya majumuisho ya kura za jimbo lolote au kata yoyote na kutonyesha kuwa wameshinda kwa jumla ya kura kituo kwa kituo zaidi ya kusema tumeibiwa kura bila kutoa takwimi za ushindi?


Munalalamika oooh dikteta dikteta wakati dikteta mkuu yupo ndani ya Chadema.
 
Dalili za ccm kuchoka na kufilisika, huyu hajawahi kuwa m/kiti wa Bavicha, m/kiti wa Bavicha kinondoni ni Kambaragwe
 
Kwa CHADEMA hata kama walikuwa hawajui nia ya CCM , mpaka hapa sasa hata ambaye ni mgumu kuelewa sasa AMEELEWA.
Hii hamahama, mlengwa kabisa ni mbowe utadhani ccm wao walishawahi hata kufanya uchaguzi wa mwenyekiti zaidi ya kufanya appointment.
Kwa jinsi hii BASI ccm wanamjenga MBOWE kuwa mwenyekiti wa kudumu wa chama cha CDM.
Mbowe aliwahi kugombea na nani?

CCM hata michakato yake ya kumpata mgombea urais inakua ni mchuano kama kombe LA dunia.
Ndio maana akishapatikana wa CCM basi wata wanajua kuwa rais tayari.


Hebu tujiulize tu kuwa kama Mbowe haamini MTU mwingine tena ndani ya chama chake anatoa taswira gani kwa vyama vinavyoshindwa kwenye urais na kikabidhi Nchi kwa wapinzani wao bila kuanza kusema hatuwezi kukabidhi nchi kwa watu wasiosomeka.

Hulka ya Mbowe ni ya kidikteta na ya hovyo kabisa . Hulka ya kutowaamini watanzana na waafrika wenzetu kwa kuachiana madaraka ndiyo inayotumiwa na CCM kule Zanzibar . Ooh tukimkabidhi Maalim Seif nchi atamrudisha Sultan.

Mbowe asikilize maoni ya watu wengi. Ikiwezekana aitishe Mkutano mkuu kwa dharura asikilize maoni ya wajumbe wa kutoka maeneo ya nchi nzima. Kuliko kujibanza na kakundi ka watu wawili watatu wa nyumbani kwake na kujifariji kuwa ujenzi wa demokrasia una safari ndefu yenye milima na mabonde wakati yeye hataki kupita kwenye hiyo milima na mabonde.
 
Back
Top Bottom