Mwenyekiti BAVICHA na Redbridge CHADEMA ajiunga CCM

*"Nimeamua kujiondoka rasmi katika chama cha demokrasia na maendeleo ( chadema) na kujiunga rasmi na chama cha Mapinduzi (ccm) baada ya kutorizishwa na uendeshwaji wa chama na uchu wa madaraka ikiwamo kung'aninia nafasi ya uwenyekiti na uendeshwaji wa chama kwa ujumla na nimeamua kumuunga mkono Mheshimiwa J.P Magufuli ( Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania )"*

- Lee Saydou, Mwenyekiti Bavicha na Redbridge Chadema Jimbo la Kinondoni.View attachment 824479
Duh, ni hataree
 
Nadhani kama Mbowe anaendelea Kungangania chama kwa kisingizio kuwa wengine ni mapandikizi watakiua chama basi nawashauri wale wote wasiopenda mfumo mbovu wa Kidikteta popote duniani basi wajitoe wote Chadema wamwache Mbowe na Lema peke yao. Ambapo 2020 Lema anapigwa chini Arusha na Mbowe anapigwa chini Hai. Hivyo watabaki Mbowe Mwenyekiti na Makamu wake ni Lema.

Kusema kuwa chama kitauawa na mapandikizi wakati kinakufa Mbowe akiwa amekishikilia yeye mwanyewe ni ujinga wa hali ya juu.

Ni bora angeachia kiti halafu kikamfia MTU Mwingine tungemkumbuka Mbowe na angepata sifa sana hata baadae akija kutokea anagombea hata Urais watu wangesema huyu ni MTU imara aliyekijenga chama lakini pia ni mpenda demokrasia wa mfano wa kuigwa.

Lakini anayoyafanya Mbowe kwa kujifanya kuwa yeye ndiye anayeweza kulinda chama kisianguke wakati kinaanguka ni kujiangamiza kisiasa.

Kuna watu wanajitokeza kumtetea Mbowe lakini utetezi wao ni wa kitoto sana.

Mbowe anaendesha chama Kibepari sana. Chama kisicho na mipango ya maendeleo zaidi ya kutumika kama shamba la bibi la mawakili kula pesa za kesi za kijinga wanazojitafutia wenyewe.

Leo wanajenga makesi ya kipuuzi nchi nzima badala ya kutumia pesa hizo kwenye maendeleo ya chama.

Wale wote wasiopenda siasa za Mbowe za Ukabila na kuendesha chama kwa kiki za matukio bila mipango huku ruzuku zikitumika vibaya bila malengo ni wakati wa Kuachana na hicho chama kwa haraka kabisa kabla ya 2019 ili waweze kuwatumikia wananchi kupitia chama kingine.
Uzuri Rais wetu nimemwelewa sana na kugundua kuwa alikua anaipenda sana Chadema na viongozi wake ndio maana anawachagua kila kukicha.
Nadhani hata Tundu Lisu kama angeamua kurudi CCM Leo hii angekua Mwanasheria Mkuu wa serikali na kuisaidia nchi hii kukiko kutumikia SACCOS ya watu wawili Lema na Mbowe tena wa kabila moja tu.
Nimemsikiliza vizuri sana Rais wakati anawaapisha wale aliowateua ,hakika wapinzani wangetambua kuwa mkuu wa nchi anawapenda wasingekua wanamtukana majukwaani badala yake wangejenga vyama vyao na kujifunza mbinu za kubana matumizi angalau kwa miaka miwili na kutumia hela ya ruzuku kujenga ofisi zao.
 
Mbowe ni sikio la kufa
Mie nafurahia anavyong'ang'ania madaraka abaki,ili akimalize kabisa kama anavyofanya Mbatia
 
Yaani wanasahau hawakukianzisha hiki chama bali waliingia baada ya kukipenda. Waasisi hilo halowashtui. Lengo la Ccm ni kuifanya CHADEMA kama walivyo wafanya NCCR, na CUF. Na ili wafanikiwe ni Mbowe aondoke maana wamemshindwa. Hakika Mbowe ni mwamba kwa Ccm
Ndugu Chama uanzishe wewe au nani,as long as kodi ya mwananchi inatumika kama ruzuku yako hiko ni chama ni mali ya umma,ndomana hata wewe unaikosoa CCM japo sio mwanaCCM ni haki yako maana ni mali ya umma ilee....
 
Huyu Mbowe Uenyekiti wa Chama tu analeta UKURUNZINZA je angepewa URAIS wa Nchi si ndio angeleta UMUGABE kabisa!
 
Waende tu.
Mkakati ni kuua upinzani na kuwapa cheo serikalini. Kama ndio hivyo wwngi atawapata.
Upinzani hauwezi kufa,watawapata watafuta fursa,si unajua zile 1.5 zinaweza nunua wafia tumbo wote,lkn haziwezi nunua kero za wananchi.
 
Usizisome, ni rahisi kihivyo tu!
tapatalk_1531465620116-jpeg.817111
 
umeshapikwa kisiasa umeiva aya subiri kuteuliwa udc, hongera cdm kwa kulea na kurecruit viongozi
 
Kwa CHADEMA hata kama walikuwa hawajui nia ya CCM , mpaka hapa sasa hata ambaye ni mgumu kuelewa sasa AMEELEWA.
Hii hamahama, mlengwa kabisa ni mbowe utadhani ccm wao walishawahi hata kufanya uchaguzi wa mwenyekiti zaidi ya kufanya appointment.
Kwa jinsi hii BASI ccm wanamjenga MBOWE kuwa mwenyekiti wa kudumu wa chama cha CDM.
1.5 itawanunua wafia tumbo wote,lkn Mbowe bado yupo sana,ila heri zirudi mtaani kuongeza mzunguko.
 
Nadhani kama Mbowe anaendelea Kungangania chama kwa kisingizio kuwa wengine ni mapandikizi watakiua chama basi nawashauri wale wote wasiopenda mfumo mbovu wa Kidikteta popote duniani basi wajitoe wote Chadema wamwache Mbowe na Lema peke yao. Ambapo 2020 Lema anapigwa chini Arusha na Mbowe anapigwa chini Hai. Hivyo watabaki Mbowe Mwenyekiti na Makamu wake ni Lema.

Kusema kuwa chama kitauawa na mapandikizi wakati kinakufa Mbowe akiwa amekishikilia yeye mwanyewe ni ujinga wa hali ya juu.

Ni bora angeachia kiti halafu kikamfia MTU Mwingine tungemkumbuka Mbowe na angepata sifa sana hata baadae akija kutokea anagombea hata Urais watu wangesema huyu ni MTU imara aliyekijenga chama lakini pia ni mpenda demokrasia wa mfano wa kuigwa.

Lakini anayoyafanya Mbowe kwa kujifanya kuwa yeye ndiye anayeweza kulinda chama kisianguke wakati kinaanguka ni kujiangamiza kisiasa.

Kuna watu wanajitokeza kumtetea Mbowe lakini utetezi wao ni wa kitoto sana.

Mbowe anaendesha chama Kibepari sana. Chama kisicho na mipango ya maendeleo zaidi ya kutumika kama shamba la bibi la mawakili kula pesa za kesi za kijinga wanazojitafutia wenyewe.

Leo wanajenga makesi ya kipuuzi nchi nzima badala ya kutumia pesa hizo kwenye maendeleo ya chama.

Wale wote wasiopenda siasa za Mbowe za Ukabila na kuendesha chama kwa kiki za matukio bila mipango huku ruzuku zikitumika vibaya bila malengo ni wakati wa Kuachana na hicho chama kwa haraka kabisa kabla ya 2019 ili waweze kuwatumikia wananchi kupitia chama kingine.
Uzuri Rais wetu nimemwelewa sana na kugundua kuwa alikua anaipenda sana Chadema na viongozi wake ndio maana anawachagua kila kukicha.
Nadhani hata Tundu Lisu kama angeamua kurudi CCM Leo hii angekua Mwanasheria Mkuu wa serikali na kuisaidia nchi hii kukiko kutumikia SACCOS ya watu wawili Lema na Mbowe tena wa kabila moja tu.
Nimemsikiliza vizuri sana Rais wakati anawaapisha wale aliowateua ,hakika wapinzani wangetambua kuwa mkuu wa nchi anawapenda wasingekua wanamtukana majukwaani badala yake wangejenga vyama vyao na kujifunza mbinu za kubana matumizi angalau kwa miaka miwili na kutumia hela ya ruzuku kujenga ofisi zao.
Kama kinakufa hofu ya nini,chaguzi huru? Waacheni wananchi waamue.Msiwachagulie
 
Back
Top Bottom