Maisha yako ni kama siti kwenye bus

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Daima wengi hupendelea siti ya dirishani... Lakini hapa huzalisha mapendeleo binafsi japo hiki ni kigezo nyongeza lakini msingi ni uleule siti ya dirishani
Iwe mbele kwa dereva
Iwe katikati karibu na mlango
Iwe nyuma kabisa kigezo ni kilekile.. Siti ya dirishani
Hii ina faida nyingi na maslahi mapaka
Inakupa uhuru wa kulimiliki dirisha, ulifungue utakapo ulifunge unapoamua.. Kwa hali ya upepo, baridi, joto ama harufu mbaya.. Una uhuru nalo.. Hii ndio standard ya maisha wengi waitafutayo.. Wengine wameshaipata Wengine bado wanaitafuta na wengi bado wanaiota.. Siti ya dirishani

Siti baada ya siti ya dirishani.. Hii ni chaguo la pili baada ya kukosa siti ya dirishani.. Utaitamani lakini ni ngumu kumuuliza jirani aliyeikalia atashukia wapi uimiliki.. Ni siti yenye uhuru nusu.. Uhuru nusu una karaha zake.. Huwezi kufanya kitu mpaka upate kibali na ruhusa ya aliyekalia siti ya dirishani.. Hapa hii ni uchaguzi wa pili katikati maisha.. Lakini wenye nafuu..

Siti ya tatu ni siti ya katikati.. Haina uhuru kwa asilimia 75.. Kulifikia dirisha ni mpaka upate ruhusa ya wawili, na yeyote atakayetaka kutoka kwenye siti yake itabidi usimame umpishe kasoro wa mbele yako tuu..
Lakini wa nyuma,
wa kushoto,
wa kulia wote hao ni wako..
Hata kukiwa na hali isiyo sawa ndani ya gari mwathirika mkumbwa ni wewe ..
Iwe uvundo
Liwe joto
Iwe baridi
Hata matukio ya nje itabidi usubiri kuhadithiwa maana huwezi kuyaona kwa wepesi

Maisha yetu ni kama siti kwenye bus
Waliojiajiri na kujenga hawana tofauti na siti ya dirishani.. Viewing tu ndio vitawabagua.. Lakini Wote wanajitegemea

Walioajiriwa ni siti baada ya siti ya dirishani.. Hawana uhuru kamili lakini wana nafuu.. Na wamepanga nyumba nzima! Viwango vya mishahara na maokoto ndio vitawabagua na wengine hapo wana mijengo na wanatembelea makalio

Siti za katikati ni kina sisi wa vibarua ana ajira daraja la chini kabisa, kufukuzwa ni mara moja tuliopanga chumba kimoja.. Usafiri wetu sometimes ni no 11 na mchana kuupitisha wima ni jambo la kawaida sana.. Usumbufu ni kila mahali na kila upande.. Kero hazikomi....!

Je umekalia siti gani? Mwaka 2023 unapoelekea ukingoni maombi na sala zangu kwani zi pamoja nawe ili mwaka ujao ukapate siti uipendayo kwa juhudi na mapenzi mema ya Maanani...Nakuombea...!!!?
b62e12483165049391a73bc025686f1c.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom