Huyu mwanamke aliye nikataa kwa fedheha nimemkumbuka mno sijui yupo wapi sasa hivi

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Ndugu zangu..

Katika harakati za kutafuta hela nilikua nasafiri kuelekea dodoma enzi hizo tunazungukia singida manyoni then dom, siti yangu ilikua ya dirishani mtoto mzuri chuga girl pembeni yangu ile tumefika babati nikaona acha nizuge kushuka chini nichek chek mazingira lengo nikirudi juu demu ni msogeze kwenye sit yangu ya dirishani kijanja then ni mbananishe haswa asije niona boya boya,

mtoto alikua mzuri mweupe mrembo haswa akikaa hips zinafutuka namna hiii na ana kaumbo kakichokozi kweli macho yote na msurvey kimachale machale tuu jinsi alivyo barikiwa, macho yake yalikua kama ana sinzia vile na nyusi za kujaa kiaina. Na nywele mpaka huku kwenye paji la uso zinamfika.

Hapo nilitoka achana na demu wangu basi nikaona acha ni komae na huyu tunaenda mkoa mmoja wote nitamsakia huko huko ila acha ni mchombeze chombeze, yani nilimbania kule dirisha kama mtu aliefunikwa na pazia maneno ya hapa na pale, vistory vya kichokozi ,

Chombeza mtoto anakua kama analainika kama anakua mgumu tena , mwamba nikaona asinicheze kaza kiume ila kilicho nikuta ase nilikataliwa na demu katika harakati zangu za kuwanga kutongoza sitokaa ni sahau, nilitamani lile bus lifike dodoma mapema nishuke zangu maana konda alinihamisha hadi siti lakini yule mwanadada alikua anapiga kelele mithili ya nimeingilia himaya yake ya siri bila idhini yani alishindwa kunikataa kistaarabu nilipigiwa makelele, fedheha na dharau mpaka abiria wote walishtuka sana wengine waka wana hisi labda itakua na mshika mtoto maeneo kwa nguvu kumbe wapi, nilikatakiwa kwa dhihaka sana si kawaida niliaibika mno nilitamani hata nishukie njiani ila wapi.

Nashukuru kuna mzee mmoja alinitia moyo kinamna huku akiniambia kaa kimnya mjukuu wangu usijibu chochote hawa ndivyo walivyo wewe kaa kimnya tuu mwache aongee atoe sumu moyoni.

Yani mpaka sasa hivi nikitaka mtokea demu safarini lazima ni mchokoze kwanza kwa style ya kumuudhi ili kupima reaction yake , nikiona normal basi mwamba najiongeza nikiona upuuzi napiga zangu kimnya busy na mambo yangu

HUYU DEMU SIKU MPATA ILA ALINIAIBISHA SANA POPOTE ULIPO NIMEKUKUMBUKA SANA , NA KAMA HUJAOLEWA FANYA UOLEWE CHAPU NA UACHE DHARAU HUKO ULIPO
 
Back
Top Bottom