Mwenye nyumba anaponyimwa chakula na mkewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenye nyumba anaponyimwa chakula na mkewe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Iga, Nov 8, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Nov 8, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu fikiria uko nyumbani kwako. Umezeeka na una wajukuu. Mkeo kafariki au kakukimbia. Unapata mke mwingine. Anapika chakula. Wageni wamekuja. Mke wako, jamaa zako na wanao wanawakarimu.

  Chakula kinaliwa chote na wewe hukupata hata tonge. Na hili linaendelea kila siku. Inakulazimu kukwangua vyungu upate matandu. Ndiyo unayoishia.

  Usiende mbali. Hii si hadithi. Ndio hali halisi ya Watanzania. Mke mpya ni uongozi mpya. Jamaa ni maafisa wa chama tawala na serikali. Watoto ni wake na watoto zao.

  Mzee ndie wananchi wa Tanzania. Je, hali kama hii, utaishughulikia vipi mwenzetu!!!!
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa ni kisa cha kwenye familia halisi ningekuambia kuwa unaposikia fainali ni uzeeni hiyo ndio maana yake.Kama ujanani mwako ulikuwa mbinafsi utarajie mateso uzeeni.Ila kwa hili la nchi sielewi.Labda kama huyo mzee bado ana nguvu basi amfukuze mke mpya abaki mwenyewe akijipikilisha na kujilia vyake tartiibuuu.
   
 3. BrownEye

  BrownEye Member

  #3
  Nov 8, 2008
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sishangai hata kidogo katika hili, kwa sababu nimewahi shuhudia kwa macho yangu mama mwenye nyumba tena ni mke wa ndoa aliyejaliwa watotot kibao na wajukuu akimyima mumewe chakula na hata sabuni ya kufulia nguo, watoto nao wakubwa na akili zao wanashabikia eti baba yao enzi zake alipokuwa nazo alimyanyasa mkewe.
  Hao ndio wabongo halisia. ...... Mkono mtupu haulambwi
   
 4. A

  Aunty Lao JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2008
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 215
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hatuwezi jua ni nini kilichomkera huyo bibie mpaka afanye hivyo ila yote haya ni hutukona na tabia aliyokuwa nayo huyo baba toka awali. Huu ndo mda wake wakuvuna alichopanda.
   
 5. eddy_mhando

  eddy_mhando JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2016
  Joined: Oct 7, 2014
  Messages: 2,346
  Likes Received: 1,860
  Trophy Points: 280
  mkuu bado upo maana kitambo duh
   
Loading...