Mwenye kujua tafsiri ya hii katuni

1. Mcheki nahodha wa chombo, anapiga vipi makasia? Kwa staili yake chombo hakiwezi kusonga mbele.
2. Mcheki kichwa, yeye anajikinga na mwavuli bila kujua hatari ya maji yanayoingia chomboni ni kubwa zaidi ya maji anayozuia na mwavuli.
3. Mcheki fasta fasta, muda si mrefu pumzi itamwishia maana matundu ni mengi naye anafanya kazi ya mtu mmoja tu.
nahodha wa chombo hukaa nyuma kweli,ila hutizama chombo kinaloelekea na si kinakotoka hivyo hapo nahodja ni jip namba moja.
 
Nikionacho kwenyepicha nikwamba huyo bw.mkubwa wakatikati anajikinga na mwamvuli pasipo kujua kwamba sio mvua bali nichombo alichomo kinavuja huyo mwenye ndoo anajaribu kukiokoa kwakumwaga maji nje na huyu aliyepo yuma ya boss anajaribu kukiongoza chombo kifike salama nihayo tu.
 
e7541ce147645c9fe98184fb413aaace.jpg
Kama picha inavyojieleza, haya wataalam wenye kujua tafsiri kazi kwenu
mi naona hapo kuna mmoja ni kichaa yaani kajifunika mwavuli wakati maji yanatokea chini
 
Daaaa kweli humu kuna vichwa binafsi sikuelewa kivile saiv nmeunganisha doti nmeelwa vzr kweli " A PICTURE WORTH A 1000 WORDS " ujumbe umfka vzr zaid kulko ka ungeandika mi paragraph mingi
 
Mr Tembo anatokwa na Jasho, Mr Katiba anatokwa na Jasho.
Alafu kuna Mfalme Juha baada ya Kusaidia haijulikani amejikinga Jua au Maji yanayotokea Chini?
 
1. Mcheki nahodha wa chombo, anapiga vipi makasia? Kwa staili yake chombo hakiwezi kusonga mbele.
2. Mcheki kichwa, yeye anajikinga na mwavuli bila kujua hatari ya maji yanayoingia chomboni ni kubwa zaidi ya maji anayozuia na mwavuli.
3. Mcheki fasta fasta, muda si mrefu pumzi itamwishia maana matundu ni mengi naye anafanya kazi ya mtu mmoja tu.
Hahaahaha hapana aisee cna hata hela ya kutafuta wakili mmoja mkuu wacha nikae kimya
Bravo
 
Huyo braza wa katikati hapo anategemea mwavuli utageuka parachuti apae. Mwavuli hapo unawakilisha wanachama wachache wanaomsapoti kwa bahati mbaya hawana nguvu kuwazidi wapiga dili (hayo matundu yanayopitisha Maji kwa wingi ndani ya chombo)
 
Anayeendesha mtumbwi hana uhakika kama watafika! huyo mwenye mwamvuli yeye hajali chochote! yaani haoni shida anayo ipata mwendesha mtumbwi! huyo anaemwaga maji, anaonekana kuchoka! na anahisi usumbufu wote anaopata unasababishwa na huyo mtu wa kati.
 
e7541ce147645c9fe98184fb413aaace.jpg
Kama picha inavyojieleza, haya wataalam wenye kujua tafsiri kazi kwenu

Kwanza ieleweke kwamba,
1. Hayo maji siyo ya mvua bali ni maji yanayoingia chomboni kwa kasi kupitia matundu yaliyopo kwenye sakafu ya boti.

2. Mheshimiwa anaonekana kutokifahamu chombo na kutokua na uwezo wa kutofautisha matukio, hiyo inathibitishwa na kitendo chake cha kujikinga na mwamvuli wakati maji si ya mvua bali ni ya mtu wausafirio ambayo yanaingia chomboni kupitia matundu yaliyopo kwenye chombo.

3. Pamoja na jitihada na watu wengine wawili waliomo chomoni, mmoja akijaribu kupunguza maji huku mwingine akipiga makasia lakini kati yao hakuna mwenye uwezo na ujasiri wa kumuambia ukweli mheshimiwa kwamba maji yale hayatokani na mvua bali matundu ya chombo.

4. Mheshimiwa anaonekana kutojua jukumu lake la kuendesha chombo na hivyo kumuachia msaidizi waki kazi ya kupiga makasia.

*******TUTAFIKA TU************
 
Cartoon za kisiasa hizo.

Mwenyekiti wa Chama amewapa kazi ngumu sana Katibu Mkuu kuendesha Chama kifike safari ili hali kuna vikwazo vingine sana vya safari hiyo.

Katibu Mwenezi naye amepewa kazi ya kukisafisha Chama wakati kuna uchafu msingi sana,je hayo maji yatakwisha wakati matundu ni mengi sana?

Lakini kwa umahiri wa Mwenyekiti hapo ataamua jambo tu na Vyombo kitakaa sawa na kufika Pwani salama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom