Mwenye hili gari anaibiwa mafuta hapa Arusha

Mwenye hili gari anaibiwa mafuta hapa Arusha

Wewe ulishawahi kuanika shati lako halafu ukalinyatia na kuliiba?
Kuna kisa kilitokea mtwara dereva toka alikua akiuza diesel usiku pahala fulani kama ndani ya garage wakiwa wananyonya ghafla ikaingia defender imezima taa jamaa nusura azimie akamwambia yule mwenyeji ndg yangu naona hapa ajira yangu imeisha na ndio siri itavuja hadi dar maana tumeshakamatwa akajibiwa usiwe na hofu hata hao walioingia nao wameleta diesel kama wewe! Kweli wazee wa kazi wakashusha mzigo wakatokomea!
Ndugu maisha yetu wabongo ni magumu sana hasa kipindi hiki
 
Kazi ya dereva ni kufikisha mzigo..... habari za mafuta wewe ziache tu


Wamejiongeza!

Ova

Hujui jiwe amekaza unawaharibia ugali

Acha kuwaharibia wanaume wenzio!

Watu wengine bwana ni sumu!!mimi nilidhania labda ni gari la serikali kuwa ni kodi zetu,sasa mtu binafsi je kama posho za safari wanazopewa hazikidhi!!na kwa magari hayo makubwa mtu anapewa mafuta kulingana na umbali wa safari yake!!madam aende na kurudi?!!je kama mwenyewe anajua jinsi ya kuendesha na kubana mafuta tatizo liko wapi??

Mkuu acha UNAAA!!hilo gari lingekuwa ni la serikali hapo ningekuita mzalendo namba 3!!baada ya RENATUS MKINGA na JPM,ila sasa hilo ni gari la binafsi na mtu anapewa mafuta kulingana na umbali wa safari yake,je kama ana anajua jinsi ya kubalance mafuta ili yamfikishe anakoenda na kurudi tatizo liko wapi??VITU VINGINE SIO VIZURI,sasa kuna faida gani utakayoipata baada ya kuripoti ?

Wivu, pambana na hali yako
Umefanya jambo la maana sana mkuu Kirchhoff kukemea vitendo vya wizi maana hata vitabu vyote vya dini vinakataza "wizi".

Imeandikwa "USIIBE"!

Ni aibu sana kuona kuna watu wanashabikia vitendo vya wizi, Watanzania badilikeni, acheni kutegemea wizi katika kutafuta maisha. Tabia ya Wizi imeneenea sana miongoni mwa Watanzania katika sekta zote.
 
We jamaa huna kazi ya kufanya jomba? Unajua nilikuwa nayapeleka wapi hayo mafuta? Wacha wivu wewe, kama imekuuma si ukatafute na wewe kazi ya Utandiboi
 
Wizi ni wizi tu.hata kama ni mtu binafsi haiwezi kuwa ni sawa.ingekuwa gari lako vipi ungejisikia.tabia za upigaji nyoka ni za kizamani sama aisee.baadaye anaweza hamia kwenye kuuza tairi
 
Ahsante sana kwa mada hii. Imetusaidia mimi na wewe kufahamu jf ina watu wa aina gani. Wanashabikia upumbavu, kukataa haki na kuhalalisha tabia chafu za uharamia. Chunga sana comments za hawa watu waliokushambulia. Si watu wa kuamini kwa lolote maana kwao uhayawani ndio msingi wa maisha. Ova!

Kweli mkuuu. Majambazi ndo dalili hizo. Afu watakuja na maneno ya Demokrasia. Dikteta. Nk ona Sasa. Mtu anaibiwa wanasema Sawa. Unadhani watakuwa na uchungu na mali za Nchi.
 
Mimi sio CCM mkuu, ila siungi mkono wizi, ushajiuliza ingekua gari ya baba yako ungefurahia hilo?
Sio gari ya baba yangu mm Nina Lorry nawapa mafuta lita 650 kwenda Kia watajua wenyewe wauze yote wasiuze ila nataka gari yangu iende na kurudi mengine juu yao mpaka unawapiga picha watu ni umbea mkuu nyinyi ndio mnatupatia magonjwa ya moyo kwa picha picha km hizo hao nao binadamu
 
Ahsante sana kwa mada hii. Imetusaidia mimi na wewe kufahamu jf ina watu wa aina gani. Wanashabikia upumbavu, kukataa haki na kuhalalisha tabia chafu za uharamia. Chunga sana comments za hawa watu waliokushambulia. Si watu wa kuamini kwa lolote maana kwao uhayawani ndio msingi wa maisha. Ova!
mm wapo katika.list ya watu wasio waaminifu humu
 
Wanauza hadi tyre na vipuli yan gar ikifungwa kifaa kipya wanauza wananunua kifaa kibov kibov . . Kuna ma bos wanazingua sana ila cpend wizi
 
Semitrela kama ndivyo liitwavyo nimeliona maeneo ya Uswahilini hapa Arusha likinyonywa mafuta na Dereva na Tandiboi wake wakiyatia kwenye dumu la lita 20 hv na kijana mmoja kuondoka nalo..
Nimepiga picha kinamna namna majizi yasinishtukie. Hapa natumia browser nashindwa kuyaweka

kichwa T 176 ARS
Tela T 348 DES
Huu ndo tunasemaga penye riziki hapakosi fitina
 
Kuna watu wanatetea huu wizi (kama kweli jamaa walikua wanaiba) halafu watu hao hao wanaotetea huo wizi siku akipita kibaka kakwapua simu basi wao ndio huongoza kumkimbiza kisha kumkamata na kumuua! Wizi ni wizi tu haijalishi umeiba nini.
 
Semitrela kama ndivyo liitwavyo nimeliona maeneo ya Uswahilini hapa Arusha likinyonywa mafuta na Dereva na Tandiboi wake wakiyatia kwenye dumu la lita 20 hv na kijana mmoja kuondoka nalo..
Nimepiga picha kinamna namna majizi yasinishtukie. Hapa natumia browser nashindwa kuyaweka

kichwa T 176 ARS
Tela T 348 DES
Sasa ikiwa ameendesha vizuri mafuta alopewa yakabaki ulitaka ayapeleke wapi. Anajilipa. 2400x20 =48,000.
 
IMG_1985.JPG
 
Mleta mada umeniudhi sana maana huo ni uchawi kama wachawi wengine, nini faida ya umbea au unataka uajiriwe wewe kwenye hilo gari?.

NIMECHUKIZWA SANA NA TABIA YAKO YA UNAA!!!
 
Back
Top Bottom