Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023, Miradi yote iliyokaguliwa Chalinze imezinduliwa bila kipingamizi chochote na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

CHALINZE: MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YOTE CHALINZE, JE CHALINZE ITAONGOZA TENA MWAKA HUU?.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Jumatatu Mei 15, 2023 umefanikiwa kumulika na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani. Miradi yote iliyokaguliwa Chalinze imezinduliwa bila kipingamizi chochote na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wakiongozwa na Abdalla Shaibu Kaim.

Kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka Jana 2022, Halmashauri ya Chalinze iliongoza Kitaifa katika Halmashauri zilizofanya vizuri katika ubora, utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru. Je mwaka huu Chalinze itaongoza tena?

Miradi ambayo imekaguliwa na Mwenge wa Uhuru kwa kukidhi vigezo na kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru ni pamoja na:-

Mradi wa Tanki kubwa la maji lililojengwa Kijiji Cha Mtambani kata ya Bwilingu, uzinduzi wa karavati la daraja barabara ya Msolwa kwenda Makondo Mengi Kata ya Bwilingu na kuzindua Kituo cha Redio Chalinze Fm iliyopo katika Jengo la Makuu Makuu ya Halmashauri ya Chalinze na kuzindua Kituo cha kisasa cha Mabasi Chalinze kilichojengwa kwa kiwango Cha lami .

Pia, Mwenge wa uhuru umezindua gari maalum la kusombea taka lililonunuliwa na Halmashauri ya Chalinze kwa ajili usafi wa mazingira katika mji wa Chalinze, kuzindua mradi wa pikipiki Kikundi cha vijana Lugoba ambao wamenufaika na mikopo ya Halmashauri ya Chalinze, kuzindua Kituo cha maabara katika zahanati ya Sareni Kata ya Lugoba pamoja na kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Msata.

Tarehe 16.5.2023 Mwenge wa uhuru umekabidhiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo katika Kijiji cha Fukayosi kuendelea kumulika maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambaye pia Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete anawashukuru wote kwa ushirikiano katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

KAULIMBIU MWENGE WA UHURU 2023: TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.27.jpeg
    166.3 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.31.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.31.jpeg
    129.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.39.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.39.jpeg
    115 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-18 at 00.14.29.jpeg
    93.9 KB · Views: 7

Similar Discussions

Back
Top Bottom