Mwenge stend leo ni vunja bomoa ondoa

Mwenge stend leo ni vunja bomoa ondoa

LEGE

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
5,122
Reaction score
9,222
Leo ukifika MWENGE lazima ushangae kwani ni kweupeee hakuna msongamano wa watu wala daladala stendi ni nyeupe mpaka raha.
hakuna kukanyagana tena wala kupigana vikumbo.

Leo asubuhi na mapema polisi FFU na baadhi ya mgambo wameendesha operation ya bomoa bomoa meza na mabanda yote ya wamachinga yaliyopo ndani nje nayaliyo karibu na MWENGE STENDI.

kiukweli wamefanya KAZI nzuri sana hasa ni baada yakuzifuata mpaka meza zilizokuwepo zimehifadhiwa.

sababu wangeziacha jioni wanazibeba na kujakufungua biashara na kuwapa pesa watu wanaojiona kama MWENGE STENDI ni yakwao Mali yao wakiongozwa na babu kesi.

haina jinsi wakulaum mtalaum ila inabidi tukubali tu kuwa kitu kisipokuwa mahari pake ni uchafu.

kuna watu wanalipa mamilioni ya kodi ila hawa wangine kodi yao wanalipa kwa KESI yeye ndio tra WA mwenge

TUKIO KATIKA PICHA: BOMOA BOMOA YA VIBANDA VYA BIASHARA MWENGE LEO, MAKUBWA YAVUMBUKA.!

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetublogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SIKILIZA TONE RADIO HAPA

<iframe width="480" height="302" src="http://www.ustream.tv/embed/9555115?v=3&amp;wmode=direct" scrolling="no" frameborder="0" style="border: 0px none transparent;"> </iframe>
<br /><a onclick="_gaq.push(['_trackEvent', 'Outgoing', 'www.ustream.tv', '/']);" rel="nofollow" href="http://www.ustream.tv/" style="padding: 2px 0px 4px; width: 400px; background: #ffffff; display: block; color: #000000; font-weight: normal; font-size: 10px; text-decoration: underline; text-align: center;" target="_blank">Live streaming video by Ustream</a>
Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com


Ilikuwa Mida ya Saa tatu za asubuhi ambapo Magari zaidi ya 10 ya Jiji yalikuwa yamejipanga eneo la mwenge Huku kukiwa na Ma Askari wa FFU wa kutosha pamoja na Migambo wa Jiji huku wakiongozwa na watu wa Jiji kwa ajili ya Kukamilisha swala zima la bomoa bomoa vibanda vyote ambavyo havina mpangilio.. zoezi hilo lilianza kwa utulivu na kuendelea kwa utulivu kutokana na ulinzi mkubwa uliokuwepo huku wananchi wakiendelea na kazi zao kama kawaida na kukatazwa kukatiza katika eneo la tukio kwa usalama wao..

Hata hivyo Baada ya vibanda hivyo kutolewa kumegundulika kuwa kulikuwa ni kuchafu kupindukia kutokana na uchafu uliokuwa umezagaa kila kona..

Kulia ni Magari mbalimbali ya Serikali yakiwa yamepaki eneo la Mwenge huku zoezi likiendelea



Hili ni eneo la ndani ya Mwenge ambapo wamebomoa vibanda vyote


Akina Mama eneo la Mwenge ndani ndani kiasi wakiwa wanahaha huku wakihangaika kutoa vitu vyao baada ya Bomoa Bomoa kupita... Hawa ni wale wauza Chai na Supu asubuhi
Huwezi amini lakini ndio hali halisi sasa eneo jirani na Kituo cha Mabasi Mwenge hakuna tena Adha ya vibanda , lakini umebaki uchafu uliopitiliza na kugundulika kuwa hawa watu walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo ambayo si salama
Hili ni eneo ambalo lilikuwa ni Maarufu kwa ajili ya kuuza vitu mbalimbali kama mitumba na viatu lakini kwa sasa hakuna kitu ni peupe


Huu ni uchafu uliopitiliza
wakiendelea kukusanya mabaki ya Mabanzi katika eneo hilo la mwenge
Kwa wale akina dada hili lilikuwa eneo maarufu sana kwa ajili ya Kutengenezea nywele na saloon bubu ambazo zote zimevunjwa vunjwa kwa sasa
Hapa juu mwanzo kulikuwa na mabanzi ya kutosha na wakina dada wengi walikuwa wanapenda kuwa hapa wakitengenezwa nywele zao wasijue kuwa walikuwa wakikaa katika eneo chafu kama hili.
Gari hili likijiandaa kuondoka baada ya somba somba
Kwa kuliangalia Eneo hili utasema ni chafu sana lakini ndio ambalo lilikuwa maarufu hasa kwa akina mama na akina dada kutengenezea kucha zao na kusuguliwa miguu, Je kama wangejua ni pachafu hivi wangeweza kugusa hata kuja kutengeneza kucha?


Bomoa bomoa ikiendelea

Baada ya kufanya manunuzi watu hutupa takataka tuu, zilikuwa zikijificha kulingana na mkusanyiko wa watu lakini hii ndio hali halisi sasa


Hakuna Vibanda lakini adha imebakia sasa ni ya uchafu
Je hapa tutapona magonjwa ya mlipuko?
Peupe hata kuna nafasi ya kutembea kwa miguu
Huu ni upande wa pili wa kuelekea Mikochemi ambapo bajaji Hupaki napo wamesafisha kwa kubomoa vibanda vyote hapa ni Shwari peupe



Picha hizi mbili ni eneo maarufu sana ambapo watu walikuwa wanauza Vifaa vya umeme na DVD, Sub Woofer pamoja na Radio bila kusahau TV sasa pamebaki kama hivi, Je walikuwa hawajui kama ni pachafu kiasi hiki?
Mgambo wakiwa wamemaliza kazi yao hapa ......

Picha na Pamoja Blog/ Dar es salaam yetu Blog
 
Leo ukifika MWENGE lazima ushangae kwani ni kweupeee hakuna msongamano wa watu wala daladala stendi ni nyeupe mpaka raha.
hakuna kukanyagana tena wala kupigana vikumbo.

Leo asubuhi na mapema polisi FFU na baadhi ya mgambo wameendesha operation ya bomoa bomoa meza na mabanda yote ya wamachinga yaliyopo ndani nje nayaliyo karibu na MWENGE STENDI.

kiukweli wamefanya KAZI nzuri sana hasa ni baada yakuzifuata mpaka meza zilizokuwepo zimehifadhiwa.

sababu wangeziacha jioni wanazibeba na kujakufungua biashara na kuwapa pesa watu wanaojiona kama MWENGE STENDI ni yakwao Mali yao wakiongozwa na babu kesi.

haina jinsi wakulaum mtalaum ila inabidi tukubali tu kuwa kitu kisipokuwa mahari pake ni uchafu.

kuna watu wanalipa mamilioni ya kodi ila hawa wangine kodi yao wanalipa kwa KESI yeye ndio tra WA mwenge

Mbona upo kishabiki sana wewe kidogo babu kesi wewe inaonyesha una chuki binafsi na kesi eeh!
 
Hakuna lolote. mbona Ubungo wamesharudi ? Wewe subiri pitia jioni ndo utajua.
 
Mleta mada umeandika kama we ndio uloendesha oparesheni
mi nadhani pale mwenge n center nzur kwa biashara na lengo la serekali ni kuongeza ajira nchni,chukuen ushauri wangu huu hapa,nnsf wapewe eneo hilo wajenge kituo na majengo meng ya biashara ya kisasa,ili mkusanye kodi nyie wenyewe baada ya huyo babu kesi,ilo linawezekana,lengo letu n kupiga hatua kimaendeleo
 
Pole zao walioumia,
wakati mwingine njaa inatufanya tufanye
vitu hata kama tunajua kuwa tunavunja sheria.
 
Tatizo la serikali yetu ni kufanya mambo kama zima moto. Watajidai endelevu baada ya wiki moja utaona kimya na watu watarudi kwenye maeneo hayo kwa nguvu. Hata kwenye mafuriko ni hivyo hivyo. Mpaka mvua inyeshe ndipo utasikia kauli za kuwataka wahame. Wakati wa kiangazi wanawaona kabisa wakijenga hawasemi kitu. Imekuwa ni serikali ya matukio. Walipaswa pia kufanya doria hata usiku kwani kuanzia saa 1 ndipo biashara huanza kusogezwa maeneo yasiyoruhusiwa.
 
Shikamooo Zembwela kwa karipio lako kali juu ya mwenge stendi sasa safii
 
Mwenge imetakata kabisa baada ya kipindi cha East Africa radio kinachoendeshwa na mwanahabari zembwela kukaripia kwa ukali sana uchafu na uwekaji mabanda pale mwenge stendi leo kumesafishwa kupo safi.

Ama kweli taaluma ya habari ikitumiwa vizuri huwa inaleta manufaa papo hapo.

Asante zembwela kwa kalipio lako.
 
Na mimi shikamoo Zembwela.., yaan nimepita hapo mwenge jana na leo kuna tofauti kubwa saaanaaa.., hakuna kibanda hata kimoja.., jiji litapendeza namna hii.., ila hili zoezi hili liwe endelevu..! SHIKAMOO ZEMBWELA!
 
Mwenge imetakata kabisa baada ya kipindi cha east africa radio kinachoendeshwa na mwanahabari zembwela kukaripia kwa ukali sana uchafu na uwekaji mabanda pale mwenge stendi leo kumesafishwa kupo safi.ama kweli taaluma ya habari ikitumiwa vizuri huwa inaleta manufaa papo hapo. Asante zembwela kwa kalipio lako.

nDO MAANA WAANDISHI WA HABARI UTAWASIKIA WAKISEMA WAO NI NGUZO YA NNE YA UONGOZI HAPA NCHINI. HAWAJAKOSEA KWA KWELI. NI KAMA VILE WANAZIKUMBUSHA HIZO NGUZO NYINGINE TATU. BIG UP ZEMBWELA
 
tukiwa na tabia ya kupongezana hivi kabla mtu ajafa me naona itakuwa jambo la maana sana sio mpaka mtu afe ndo usikie kweli alikuwa mtu wa watu asiyependa makuu kweli ameacha pengo
 
Bada ya sku 2 wanarudi ndio Ujinga wa hili linchi
 
Kwa Dar hiyo ni nguvu ya soda..Jioni pako full kama kawaida..

Waje waige Arusha..Kusafiii.
 
Back
Top Bottom