Mwenge nako kulikoni?

Mkare

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
504
78
Wakuu, nimepita Mwenge asubuhi hii mida kama ya moja na nusu hivi wakati naeleka kibaruani na kukuta makundi ya watu na FFU wakiwa kwa mbali kidogo huku nikisikia amri fulani inatolewa. Naomba kama kuna mwenye idea ya nini kinaendelea anijuze.
 
Na mimi nilipita pale, nikapigwa butwaa, nikadhani ya Arusha yamehamia huku. Ukweli ni ugomvi wa humo ndani ya msikiti. Kuna madai fedha zitokanazo na miradi ya msikiti zimeliwa. Kuna wanaoamini ndani ya msikiti kuna watu wamepandikizwa na CHADEMA(ooops) tena wanadaiwa ni Makafiri(wakristo) ambao ndio wanafisadi hizo hela kwa kushirikiana na uongozi wa Msikiti. Ilikuwa pata shika lakini Polisi wakati huu waliwahi na kufanya kazi yao ya kulinda usalama. Sijapata habari ya majeruhi.

Chokochoko katika Msikiti wa Mwenge ni za siku nyingi. Kuna kipindi wanakuwa na mihadhara mikali mikali kweli wakidai hili na lile. Mingi mihadhara hii ni kudhalilisha dini zingine, lakini pia ipo ya ya siasa, na mara nyingi inabidi kweli uwe mvumilivu kuendelea kuwa jirani na msikiti wakati wa mihadhara hii. Huwa natamani kuingia ndani niwashauri jinsi ya kujiendesha, lakini nikifanya hivyo nadhani sitakuwa na mapenzi mema na shingo yangu!
 
Nami nimepita hapo Mwenge na kukuta ni vurugu tupu. Nilipouliza nimeelezwa kuna mgogoro kati ya viongozi wa dini wa Misikiti midogo ya eneo la Mwenge/Kijitonyama na viongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Mwenge. Watu walikuwa wanaeleza kuwa Viongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Mwenge wamehodhi mapato ya pango yanayotokana na vibanda vinavyozunguka msikiti huo, na hivyo viongozi wa Misikiti midogo wanasema wanasikia harufu ya ufisadi!! Nilisikia kuwa Mbunge wa Ubungo Ndugu Mnyika yuko huko ndani msikitini na viongozi wa mtaa wakijaribu kusuluhisha hili na lile. Mazingira hayakuwa mazuri ikabidi niondoke kwani mawe yalianza kurushwa nikaogopa ki corolla changu kisivunjwe vioo!! Nawasilisha, nikipata habari zaidi au fafanuzi wa kina nitawajulisha.
 
dini nyingine tabu tupu sipati picha ndio wangekuwa super power nadhani 'makafiri' tusingekuwepo duniani.
 
Shukrani, ila usitake kuchafua hewa asubuhi asubuhi mkuu.
 
dini nyingine tabu tupu sipati picha ndio wangekuwa super power nadhani 'makafiri' tusingekuwepo duniani.

Hivi wewe katika coment zako lazima uingize udini?? yaani hiyo inahusiana nini na dini unayoizungumzia, mbona Sumbawanga watu wamekuwa na mtafaruku na kanisa na hakuna aliyeisema dini husika.

Hebu fikiria kwa kutumia kichwa chako na sio kinyeo before you comment!
 
Nami nimepita hapo Mwenge na kukuta ni vurugu tupu. Nilipouliza nimeelezwa kuna mgogoro kati ya viongozi wa dini wa Misikiti midogo ya eneo la Mwenge/Kijitonyama na viongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Mwenge. Watu walikuwa wanaeleza kuwa Viongozi wa Msikiti wa Ijumaa wa Mwenge wamehodhi mapato ya pango yanayotokana na vibanda vinavyozunguka msikiti huo, na hivyo viongozi wa Misikiti midogo wanasema wanasikia harufu ya ufisadi!! Nilisikia kuwa Mbunge wa Ubungo Ndugu Mnyika yuko huko ndani msikitini na viongozi wa mtaa wakijaribu kusuluhisha hili na lile. Mazingira hayakuwa mazuri ikabidi niondoke kwani mawe yalianza kurushwa nikaogopa ki corolla changu kisivunjwe vioo!! Nawasilisha, nikipata habari zaidi au fafanuzi wa kina nitawajulisha.
Senkiu odo
 
Kiraka sioni ni busara kumtukana mwenzio ni vyema ushauri aachane na hayo maswala ya udini maana hata hapo unaposema sumbawanga kama unarfuatilia media vyema soma gazeti la Al Nuur la Ijumaa iliyopita upate udini uliojiri pale. sema tu tuache kuingiza maswala ya kuhusisha dini au chama fulani cha siasa katika mambo ya msingi.
 
Bwana jamaa kazidi yeye kila post lazima ahusishe na udini , tena uislam... sidhani kama ni vyema.
 
Naamini JF ikitumiwa vizuri ni kisima cha habari na maarifa, ila nachelea watu wanaogeuza jalala la kila taka zao, haitusaidii bali tunapoteza nguvu bure kudiscuss nothing, haitusaidii kitu,
 
Ni kweli kabisa kuna watu wana2mia hili jukwaa vibaya,sijui wanataka jf nayo ifungwe?..2na matatizo mengi ya kisiasa,kiuchumi na kijamii,..2yalist,yafanyiwe analysis na 2toe solution..
 
Back
Top Bottom