Kuomba kwingi hakusaidii bila kuchukua hatua

Kuomba kwingi hakusaidii bila kuchukua hatua

Joined
Mar 25, 2026
Posts
12
Reaction score
25
Sijui nani anahitaji kusikia hii.

Ila kama una changamoto fulani.

Sio mbaya ukienda Kanisani. Au msikitini.

Umuombe mungu akupe hekima, nguvu na uzima wa kutatua hiyo changamoto.

Tatizo ni kuomba sana bila kuchukua hatua yeyote.

Kutumia muda wako wote kusikiliza vipindi vya dini bila ACTION kunapelekea kuwa na depression.

Kama una tatizo la hela.

Tafuta Kazi au jifunze Sales. Jenha client base yako.

Au jifunze huduma watu wanahitaji.

Alafu uza hiyo huduma.

Kama una tatizo la kiafya.

Badilisha mfumo wako wa chakula.

Fanya mazoezi kila siku.

Lala Saa 4 usiku.

Acha kula vyakula vya kukaanga na wanga.

Acha kunywa pombe. Acha kuvuta sigara.

Muda wako wote utumie ukiwa nje ya nyumba yako.

Jitahidi jua ligonge macho na ngozi kwa angalau nusu saa kila asubuhi.

Jitahidi kuwa social uwezavyo.

Jizungushe na watu.

Punguza muda unaotumia online.

Punguza kufuatilia taarifa za siasa au ishu yeyote negative.

Kaa mbali na walalamikaji.

Utashangaa baada ya hapo matatizo yako yote yanayeyuka bila kuhangaika sana.
 
Sikuskii bwashee ongeza sauti unasemaaa
 
Attachments

  • FB_IMG_1780315494134.jpg
    FB_IMG_1780315494134.jpg
    87.4 KB · Views: 9
Kuomba kunadumaza akili.

Japo pia, ukiomba kwa Imani unapata.

Kumbuka pia, Imani bila matendo (action) imekufa.

Sijui hata nilichoandika.
Bwashee , imani najua inafanya kazi kwenye akili ila sio kwa namna hiyo inayo aminishwa ,wewe kuamini kuna kiumbe kitakusaidia tofauti na uwezo wako ni kujilisha upepo
 
Bwashee , imani najua inafanya kazi kwenye akili ila sio kwa namna hiyo inayo aminishwa ,wewe kuamini kuna kiumbe kitakusaidia tofauti na uwezo wako ni kujilisha upepo
Kwa uzoefu binafsi, kusaidiwa kupo Tena sana tu, ila ni kwa Yale yaliyo nje ya uwezo wetu.

Mfano, upangiwe hatari ya namna yoyote halafu Mungu akuepushe. Mfano, ugonjwa (sumu) n.k.

Yale yaliyo ndani ya uwezo wako kuyatenda, sahau kusaidiwa.

Mfano: Yesu alimponya mgonjwa kwenye bwawa la Siloamu, hakuwa mgonjwa peke yake mahali hapo, bali alisaidiwa kwa kuwa hakuwa na mtu wa kumweka birikani maji yanapotibuliwa.
 
Mungu hayupo wala yesu hayupo unaongelea vipi mimi ambae siamini haya na ninateleza tu tofauti na muumini?
 
Mungu hayupo wala yesu hayupo unaongelea vipi mimi ambae siamini haya na ninateleza tu tofauti na muumini?
Kuamini kwako Mungu hayupo hakumfanyi asiwepo.

Chukulia lifuatalo,

Waafrika wengi hatuna historia hata za mababu zetu kufikia kizazi cha sita. Hata majina tu, nikikuambia utaje majina Yako unayotimia, utataja la kwako, baba, Babu ukizidisha sana utaishia jina la Babu wa Babu Yako.

Je, inamaamisha kutokea kwako duniani kunaanza na huyo unayejua jina lake pekee (mf Babu wa Babu?)

Kama huwezi kujua hata mtu wa kumi kwenye lineage Yako, sembuse Mungu ambaye ndiye chanzo cha Kila kituo.
 
Back
Top Bottom