Mwenge High School Singida Kunani ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenge High School Singida Kunani ?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mtanga Tc, Apr 21, 2012.

 1. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakuu,nimepata neema ya kupita ktk shule ya Mwenge leo ambayo ilikuwa na sifa kedekede miaka ya nyuma pamoja na heshima ktk huu mji mdogo wa Singida.Lengo kuu ni kujidhirisha na mazingira ya elimu ktk shule hii ambayo "my lost rib happened to school there about more than twenty years ago"

  Kweli inasikitisha kuona sehemu hii kama imetelekezwa!Indeed it does not reflect the presence of Life around nor enticing the ambitious young generation to focus on their studies due to its current status!!!

  To the best of my understanding,shule hii imetoa some intelectual heavyweights who are in very prestigious positions not only across the country but also Across the boarders! Mimi kwa mtazamo wangu nadhani kwamba kwa sababu yeyote ile...shule hii haitendewi haki....

  kwa wale wadau mliopitia shule hii mimi nimeonelea niwakilishe mada hii,nani ajuaye kwamba suluhisho litapatikana kuinusuru hali halisi ya mazingira ya shule hii???
   
 2. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Duh kama ni hivyo basi inasikitisha. Nilisoma hapo 1972 chini ya Headmaster Mr. Mishael Muze na wakati huo mkuu wa mkoa alikuwa hayati Kanali Moses Nnauye. Mwenge Sec. kwa kweli ilikuwa ni shule kinara!
   
 3. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna tatizo gani uliloliona mkuu
  Singida ni mkoa sio mji mdogo.
  OTIS
   
 4. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kama una moyo wa uzalendo ukiona mazingira ya shule hii leo,chozi la huzuni laweza kukutoka! Mimi nadhani utunzaji wa mazingira pekee hauhitaji hata pesa za wafadhili hata wanafunzi waliopo,naambiwa wanafikia 700 wanaweza kufanya zamu za kufanya usafi na hata kupanda maua na miche mingineyo inayoweza kubadilisha mandhari ya shule hii..wadau wa JF mliopitia hapa you can do something!
   
 5. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakubali sahihisho...Singida mkoa mdogo.
  Judging from its appearance and surrounding enviroments,naona ina dalili ya kutelekezwa,vijinjia vya wenyeji vinapita kati ya madarasa & mabweni,vichaka katikati ya shule,kutokuwepo kwa uzio kuitofautisha shule na maeneo ya jirani yanayoizunguka,hata wanafunzi wanaonekana wapo wapo tu,hakuna utanashati wowote kati ya mengi ambayo ni ngumu kuelezea!!!
   
 6. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo la viongozi wa Shule wasipoambiwa kuna mashindano ya usafi na utunzaji wa Mazingira, huwa hawajihangaishi. Pamoja na hali ya ukame, Mwenge iliwahi kuwa na mazingira mazuri na safi miaka ya themanini hadi kati kati ya miaka ya tisini mambo yalipanza kubadilika kidogo kidogo.
   
 7. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nami nimepata elimu yangu katika hiyo shule kongwe..safari yangu ya kitaaluma ilianzia shuleni hapo.
  Kwa sasa mazingira hayaridishi kabisa..shule inahitaji ukarabati mkubwa.Watawala wetu watasema hakuna pesa!
  Kinachotusumbua ni kutofahamu namna ya kupanga vipaumbele vyetu.
   
 8. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Yaani nilipokuwa mwanafunzi zama hizo sikuwahi kufikiria wala kuota kwamba miaka ya baadaye shule ya Mwenge itakuja kuporomoka kiasi hicho kimazingira. Kwa mtaji huu wa kutokujali iko siku mpaka ikulu nayo itaota vichaka.

  Hebu fikiria, miaka arobaini iliyopita shule ilikuwa imezungushwa seng'enge na majengo yalikuwa yanapakwa rangi pia kulikuwa na mageti matatu. Kulikuwa na mabweni ya wavulana na wasichana na kila jumamosi tulikuwa na mashindano ya usafi! Hii hali unayozungumzia sasa nashindwa kuelewa kwa nini watanzania tunakubali kurudi nyuma karibuni kwenye kila fani, badala ya kwenda mbele!
   
 9. L

  Luushu JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 593
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 60
  Ukamae si sababu kwangu mimi nakumbuka tulikuwa tunaenda umiseta tukitokea Mkwese tech sec school Mwenge ilikuwa nzuri kimazingira,kielimu na nithamu leo hii vyote hakuna.Cha kufanya ni kuung'oa kwanza utawala ulioko madarakani mambo yatanyooka kwani si Mwenge pekee iliyooza bali hata Ihanja,Mkwese na Iambi nazo uozo mtupu
   
 10. Rabi wa Leo

  Rabi wa Leo Senior Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu anipe nguvu 2015 nilinyakue jimbo lile..Mkoa mzima shule zenye advance ni 3..Miaka ya 2004,Mwenge ilikua na uwezo wa kuchukua wanafunzi wa bweni na kutwa,wasichana na wavulana,form one hadi form six!Lakini leo,inachukua boarding tu,wavulana tu,advance tu!Shule imekua kichaka,majengo yamechoka hadi unaogopa kukaa pembeni..,miundombinu duni,hakuna uzio,pamepauka,pamechoka.,hakuna vyoo vya uhakika,nyumba za walimu wanaishi wapita njia...HALI NI MBAYA!!!
   
 11. Rabi wa Leo

  Rabi wa Leo Senior Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tujiulize tena swali dogo tu...SERA YA MKOA JUU YA MAENDELEO YA ELIMU,HASA YA ADVANCE IKO VIPI??
  Tunaleta siasa kwenye elimu.,Shule ya Mwenge inapaswa kuwa pambo la mji kwa kua iko katikati ya mji...lakini unapofika mjini,hutamani kupita pale na mgeni,NI AIBU!!!
   
 12. Rabi wa Leo

  Rabi wa Leo Senior Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanaleta siasa kwenye maswala ya msingi..,mambo yasiyo ya msingi wanayafagilia sana.,wanatumia bilions of money kwenye maswala ya kipuuzi kabisa..Hivi kweli mkoa mkubwa kama Singida unakuwa na shule za serikali za advance 3???
   
 13. c

  calvingyan Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo nayo haikuwa kati ya zile shule zinazoitwa shule za wazazi zizokuwa zinamilikiwa na wana magamba....!!
   
 14. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Naikumbuka . mimi nilikuwa pale 1974 Headmaster akiwa Prof. DAVID KAPINGA . bweni langu lilikuwa azimio. nakumbuka kulikuwa na majengo mazuri na walimu pia. labda tuliopita pale tujipange ili tuipige Tafu. Tunaweza kuanzia umoja huo huku JF. mnaonaje?
   
 15. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Georgeallen kwanza nikupe salute kubwa kwa huo mwaka uliopita mwenge...inaonyesha umekula kachumvi! Naunga mkono hoja yako kwa asilimia zote.Perhaps iundwe namna ya Alumni wa Mwenge then from there imtafute the way forward!
   
 16. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Duh, kwa hiyo inaonekana hatujapishana sana. Nilikuwepo 1972 na Mr. Kapinga alikuwa Assistant wa Mr. Muze. Namkumbuka na sauti yake nzito ya kiaina wakati wa Roll Calls za jumamosi jioni. Wakati mwingine (ilipokuwa zamu yake) alikuwa anakuja asubuhi kutuamsha kwenda kwenye mchakamchaka. Nimesikia Prof. Kapinga amefariki dunia (RIP kama ni kweli!). Mwenge ya enzi hizo ilikuwa ni shule mojawapo top nchini.
   
 17. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Prof. D.S Kapinga amefariki Machi, 2010. May His Soul RIP!
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hii shule naifahamu vizuri. Kwa sasa ipo ICU, hoi bin taaban.
   
 19. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa!
   
 20. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole. Serikali yetu haina uwezo wa kujiendesha tena hivyo shule nzuri za awali kaputi!!! Bora kanisa katoliki wameanza mkakati na wameomba kurejeshewa zile za kwao na tayari mambo mazuri yanaonekana. Kithibitisho ni Forodhani ilichakaa hadi popo wakafanya nyumba kwenye paa na pembeni mwa nyumba but now it is almost new. Kwa hiyo nashauri serikali irejeshe shule zote za misheni ili kupunguza gharama maana wameshindwa. I happened to visit DODOMA Secondary, kwa wanaoijua ni nzuri ajabu but sasa inaelekea kuwa gofu. Pugu Secondary je? Nafikiri kanisa katoliki lichukue shule zake kuanzia TABORA, KILAKALA, WERUWERU na nyingine nyingi. Hiyo ya mwenge du siijui kama ni serikali parsee basi jua inaelekea kuwa gofu la maonesho (ruins).
   
Loading...