Mwenendo wa Gazeti Raia Mwema

Mwenendo wa Gazeti Raia Mwema

General ulimwengu anatafuta pesa za uzeeni nafkr

Ila akumbuke ccm Wana roho ya shetan anaweza kuwatakasa na kuwalamba viatu ila wakamsahau kwenye mvinyo

Red wine ya ccm wanakunywa mabepari tena makupe wacha Generali asimamishe kofia yake km bata mzinga ipo siku......
 
Kwa maoni yangu hili gazeti limeshapoteza mwelekeo. Tangu kipindi cha uchaguzi walionesha msimamo wao wa kiitikadi na kuiponda sana UKAWA. Msimamo huo wameendelea nao hata baada ya uchaguzi. Leo magazeti mengi yameripoti juu ya uchaguzi wa Umeya Dar (ukurasa wa mbele) isipokua gazeti hili la Jenerali Ulimwengu.

Magazeti mengi yameifanya habari ya Umeya wa Dar kuwa Lead Story, Anchor story or Strap story ktk ukurasa wao wa mbele. Kwa kifupi yameifanya issue ya Umeya kuwa habari ya kuuzia gazeti. Lakini Raia Mwema ni kama vile hawaishi Dar wala hawajui kinachoendelea.

Hivi habari kubwa kama hii ya Umeya unaachaje kuiripoti? Hasa ukizingatia ilikua na sintofahamu ya muda mrefu? Kumbuka uchaguzi wa Umeya Dar umefanyika mara 4 bila mafanikio mara ya 5 ndipo umefanikiwa. Je hii si habari?

Yani Raia Mwema wamempa coverage "Babu wa Loliondo" wakaacha kuzungumzia Umeya wa Dar?? Maajabu haya. Yani Babu wa Loliondo ana "make news" kuliko Issue ya Umeya Dar?

Nimegundua media zetu za kibongo bado zina safari ndefu sana. Zinaripoti kwa mahaba ya itikadi na si kwa weledi. Naamini CCM ingeshinda Umeya jana Raia Mwema wangeifanya hiyo habari kuwa habari kuu kwny ukurasa wa mbele.

Ni jambo la ajabu kwamba hata Habari Leo gazeti la serikali limeizidi Raia Mwema. Habari Leo angalau wameripoti kwnny ukurasa wa Mbele wakiandika "Dar mikononi mwa Chadema". Lakini Raia Mwema kimya kama vile Umeya hauwahusu. Kwa lugha rahisi ni kwamba Raia Mwema wameumia sana UKAWA kushinda Umeya wa Dar kuliko serikali ya CCM ilivyoumia.

Mahaba yanapozidi weledi ni tatizo kubwa ktk ulimwengu wa habari. Wenzetu Ulaya wanajua kuripoti kwa weledi. Linapokuja suala lenye maslahi kwa umma wote hulipa uzito bila kujali itikadi zao. Nimefatilia media za magharibi zote ziko busy na BRUSSELS Attack. Watu wanafanya live coverage, story analysis, wanafanya interview kuhusu hiyo attack.. yani wenzetu wanajua kutengeneza news na kuset agenda.

Lakini hapa bongo mahaba kwanza weledi badae. Angalia matukio ya hapa Nyumbani uone kipaumbele kiko wapi. Nakumbuka wakati Mv.Spice Islanders inazama Startv walikua wanaendelea na wallpaper yao, TBC wanagonga Bongo Flavour.. Who cares.?? Bado tuna safari ndefu sana.!

Malisa GJ.!

Siku ukijua kukokotea asimilia ya ushindi kwenye uchaguzi ndiyo utajua kama Raia Mwema imepoteza mwelekeo au la.
 
Mleta mada amesahau kutuambia kuwa hata yeye anafikiri kwa kutumia moyo
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya gazeti litolewalo kwa wiki mara moja (la kila wiki mfano Raia Mwema na Dira) na gazeti litolewalo kila siku (gazeti la kila siku mfano Tanzania Daima na Uhuru)...
Nadhani hapo ndipo mwandishi hakupaelewa. Magazeti ya wiki yanafika mikoani hata siku moja kabla ya tarehe yake. Alipaswa afahamu hilo
 
Kwa maoni yangu hili gazeti limeshapoteza mwelekeo. Tangu kipindi cha uchaguzi walionesha msimamo wao wa kiitikadi na kuiponda sana UKAWA. Msimamo huo wameendelea nao hata baada ya uchaguzi. Leo magazeti mengi yameripoti juu ya uchaguzi wa Umeya Dar (ukurasa wa mbele) isipokua gazeti hili la Jenerali Ulimwengu.

Magazeti mengi yameifanya habari ya Umeya wa Dar kuwa Lead Story, Anchor story or Strap story ktk ukurasa wao wa mbele. Kwa kifupi yameifanya issue ya Umeya kuwa habari ya kuuzia gazeti. Lakini Raia Mwema ni kama vile hawaishi Dar wala hawajui kinachoendelea.

Hivi habari kubwa kama hii ya Umeya unaachaje kuiripoti? Hasa ukizingatia ilikua na sintofahamu ya muda mrefu? Kumbuka uchaguzi wa Umeya Dar umefanyika mara 4 bila mafanikio mara ya 5 ndipo umefanikiwa. Je hii si habari?

Yani Raia Mwema wamempa coverage "Babu wa Loliondo" wakaacha kuzungumzia Umeya wa Dar?? Maajabu haya. Yani Babu wa Loliondo ana "make news" kuliko Issue ya Umeya Dar?

Nimegundua media zetu za kibongo bado zina safari ndefu sana. Zinaripoti kwa mahaba ya itikadi na si kwa weledi. Naamini CCM ingeshinda Umeya jana Raia Mwema wangeifanya hiyo habari kuwa habari kuu kwny ukurasa wa mbele.

Ni jambo la ajabu kwamba hata Habari Leo gazeti la serikali limeizidi Raia Mwema. Habari Leo angalau wameripoti kwnny ukurasa wa Mbele wakiandika "Dar mikononi mwa Chadema". Lakini Raia Mwema kimya kama vile Umeya hauwahusu. Kwa lugha rahisi ni kwamba Raia Mwema wameumia sana UKAWA kushinda Umeya wa Dar kuliko serikali ya CCM ilivyoumia.

Mahaba yanapozidi weledi ni tatizo kubwa ktk ulimwengu wa habari. Wenzetu Ulaya wanajua kuripoti kwa weledi. Linapokuja suala lenye maslahi kwa umma wote hulipa uzito bila kujali itikadi zao. Nimefatilia media za magharibi zote ziko busy na BRUSSELS Attack. Watu wanafanya live coverage, story analysis, wanafanya interview kuhusu hiyo attack.. yani wenzetu wanajua kutengeneza news na kuset agenda.

Lakini hapa bongo mahaba kwanza weledi badae. Angalia matukio ya hapa Nyumbani uone kipaumbele kiko wapi. Nakumbuka wakati Mv.Spice Islanders inazama Startv walikua wanaendelea na wallpaper yao, TBC wanagonga Bongo Flavour.. Who cares.?? Bado tuna safari ndefu sana.!

Malisa GJ.!
Msichojua ni kwamba gazeti husika hasa ni Raia Tanzania, nalo la Raia Mwema lakini hilo lilianzishwa mahsusi na CCM ili liponde wapinzani na ndilo lilikuwa kiunganishi cha Dr Slaa na CCM. Ni kansa ya njaa imeingilia vyombo vya habari Tanzania. Hivi inakuwaje hadi leo hakuna chombo chochote kilichofanya kazi ya kuchunguza sababu na ushahidi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi Oktoba 25 Zanzibar. Juzi matokeo, vyombo hivyo vimekalia Dr Shein kapata ushindi wa kishindo, alikuwa anashindana na nani? Na matawi ya CCM? Kama bado kuna vyeo vya Ukuu wa wilaya havijatangazwa tutasoma na kusika utumbo mwingi kuisifia CCM. Kila mwandishi,mhariri anashika kompyuta yake akiwaza kama JPM atamkumbuka!
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya gazeti litolewalo kwa wiki mara moja (la kila wiki mfano Raia Mwema na Dira) na gazeti litolewalo kila siku (gazeti la kila siku mfano Tanzania Daima na Uhuru)...

Lumumba acheni kutetea ujinga. Gazeti analoandikia Mwanakijiji, Raia Mwema, halitaweza kuripoti mambo mazuri ya UKAWA. Uchaguzi wa Meya ulifanyika jana mchana. Hii sio stori ya kukosekana kwenye gazeti lolote (hata la kila wiki) kwa sababu ya muda.
 
Ujumbe wa Lumumba hauwezi kumfikia mtu mwenye akili sawa kama mimi
Mtu mwenye akiuli sawa hawezi kuishi kwa kutegemea malalamiko kila kukicha. Unachokiona kikifanywa na raia mwema, kimefanywa na mwananchi, tanzania daima kwa muda wote wa kampeni, ila wewe huwezi kuona udhaifu mpaka unapokigusa kile ambacho moyo wako unakipenda.
 
Kuwapangia cha kuandika ni kuingilia Uhuru wa habari.
 
Lumumba acheni kutetea ujinga. Gazeti analoandikia Mwanakijiji, Raia Mwema, halitaweza kuripoti mambo mazuri ya UKAWA. Uchaguzi wa Meya ulifanyika jana mchana. Hii sio stori ya kukosekana kwenye gazeti lolote (hata la kila wiki) kwa sababu ya muda.
Sasa sijui nikuiteje mkuu wangu...

Ni wapi nimetetea ujinga (ama wewe ni mjinga?)..

Kumwambia mtu kuna tofauti kati ya magazeti ya kila wiki na ya kila siku ni kutetea ujinga?...Angalia usije ukaonekana wewe ni mjinga kabla haujamtuhumu mtu anatetea ujinga..

Gazeti la Raia mwema linatoka kwa wiki mara moja..Na habari zake nyingi ni za 'Makala'..Uchaguzi wa Meya wa Jiji umefanyika jana..Gazeti limeanza kusambazwa jana jioni kwenda mikoani...Meaning lilikuwa tayari hata kabla huo uchaguzi haujafanyika...Hiyo habari imeandikwa na magazeti mengi tu yanayotoka kila siku..

Halafu, sijui unatumia vigezo vipi kumbrand mtu kama 'wa Lumumba'....Ni kwa sababu anatofautiana na kile unachotamani akiandike/akipost?
 
Habari Leo wanajikosha tu baada ya kupondwa hapa JF.

Kuhusu Rai Mwema nadhani tatizo ni kuwa hilo si gazeti la kutoka kila siku hivyo huenda lilishaandaliwa kutoka kama lilivyotoka.Yaani haliripoti habari za kila siku
mkuu ukumbuke kwamba Hii Raia Mwema tumeiweka kwenye kamera tangu uchaguzi mkuu .
 
huu ni upuuzi wa kiwango cha lami, yani unalazimisha chombo binafsi kureport habari yako, hata kama wao wanaiona kwao haina maslahi??

habari ya meya wa dar haiwezi kuuza gazeti leo, sababu jana ilikuwa ndo trend ya siku na mitandao karibu yote ilifanya coverage live, ikiwemo television katika taarifa ya habari, sasa nani leo ataenda tena kununua gazeti ili kurudia kusoma habari hiyo??

Magazeti yanaendeshwa kibiashara na taarifa ya nani kawa meya si profitable news anymore sababu kila mtu anaijua tayari
 
kweli mkubwa uwe muelewa wakati unahoji swala LA weledi Kwa RAIA mwema pia uhoji weledi Wa Tanzania daima mwanahalisi na dira
 
Mleta mada amesahau kutuambia kuwa hata yeye anafikiri kwa kutumia moyo
Bora moyo kuliko makalio
Mtu mwenye akiuli sawa hawezi kuishi kwa kutegemea malalamiko kila kukicha. Unachokiona kikifanywa na raia mwema, kimefanywa na mwananchi, tanzania daima kwa muda wote wa kampeni, ila wewe huwezi kuona udhaifu mpaka unapokigusa kile ambacho moyo wako unakipenda.
Huwaro linaandikaga nini sasa
 
huu ni upuuzi wa kiwango cha lami, yani unalazimisha chombo binafsi kureport habari yako, hata kama wao wanaiona kwao haina maslahi??

habari ya meya wa dar haiwezi kuuza gazeti leo, sababu jana ilikuwa ndo trend ya siku na mitandao karibu yote ilifanya coverage live, ikiwemo television katika taarifa ya habari, sasa nani leo ataenda tena kununua gazeti ili kurudia kusoma habari hiyo??

Magazeti yanaendeshwa kibiashara na taarifa ya nani kawa meya si profitable news anymore sababu kila mtu anaijua tayari
Unaendesha kibiashara bila Maslai ya Taifa
 
Back
Top Bottom