DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 18,025
- 45,578
Anaandika kada wa CCM Rashid Chilumba Sifahamu ikiwa CCM na Serikali inafahamu mwenendo huu wa Siha na Kinondoni dhidi ya Upinzani unaongeza chuki kutoka kwa wananchi kuliko faida. Watu wanaona, wanasoma, wanasikia na wanashuhudia. Na walio wengi siyo mazezeta wanajua lililo jema na ovu, haki na batili, wanaumia na wanabaki na chuki mioyoni na wanaongeza wafuasi wa chuki dhidi ya chama chenu.
Msichana mdogo amefariki kwa risasi akiwa na Mkoba wake wa daftari pekee, mawakala wa wagombea kutoka vyama pinzani wamesumbuliwa kupata viapo, na bado wamenyimwa haki kwa muda kutoingia vituoni. Sasa uchaguzi ulikuwa na umuhimu gani? Mambo haya yanapoteza kila sifa na kazi kubwa mnayoifanya serikalini, maana watu watajiuliza kama mnafanya kazi kubwa na ya manufaaa kwa taifa haya mengine ya nini? Kinahofiwa nini hadi kuwe na mazingira ya wazi ya kukosekana usawa na uhuru katika chaguzi ndogo kama hizi? Watu watawahukumu kwa makosa haya ambayo wala hayakuwa na umuhimu wowote kutendwa.
Ikiwa hatuwezi kujenga nchi pamoja na wengine wanaotukosoa ni bora tuseme na tuchukue hatua za wazi na si vificho. Tufute vyama vyote kibaki kimoja ili tuokoe fedha tujenge standard gauge kwenda Zambia.
Mnaaibisha Taifa letu kwa kweli