Mwenendo huu wa Siha na Kinondoni dhidi ya Upinzani unaongeza chuki kutoka kwa wananchi kuliko faida

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,535
44,002
Anaandika kada wa CCM Rashid Chilumba Sifahamu ikiwa CCM na Serikali inafahamu mwenendo huu wa Siha na Kinondoni dhidi ya Upinzani unaongeza chuki kutoka kwa wananchi kuliko faida. Watu wanaona, wanasoma, wanasikia na wanashuhudia. Na walio wengi siyo mazezeta wanajua lililo jema na ovu, haki na batili, wanaumia na wanabaki na chuki mioyoni na wanaongeza wafuasi wa chuki dhidi ya chama chenu.

Msichana mdogo amefariki kwa risasi akiwa na Mkoba wake wa daftari pekee, mawakala wa wagombea kutoka vyama pinzani wamesumbuliwa kupata viapo, na bado wamenyimwa haki kwa muda kutoingia vituoni. Sasa uchaguzi ulikuwa na umuhimu gani? Mambo haya yanapoteza kila sifa na kazi kubwa mnayoifanya serikalini, maana watu watajiuliza kama mnafanya kazi kubwa na ya manufaaa kwa taifa haya mengine ya nini? Kinahofiwa nini hadi kuwe na mazingira ya wazi ya kukosekana usawa na uhuru katika chaguzi ndogo kama hizi? Watu watawahukumu kwa makosa haya ambayo wala hayakuwa na umuhimu wowote kutendwa.

Ikiwa hatuwezi kujenga nchi pamoja na wengine wanaotukosoa ni bora tuseme na tuchukue hatua za wazi na si vificho. Tufute vyama vyote kibaki kimoja ili tuokoe fedha tujenge standard gauge kwenda Zambia.

Mnaaibisha Taifa letu kwa kweli
 
Mimi naamini hii nchi kwa sasa ipo chini ya uongozi wa shetani. Ni shetani ambaye hajali uhai wa binadamu, hajali uhuru wa watu, hajali machozi ya binadamu wengine.

Kuna mahali tulifanya makosa tukakubali kubali kumwingiza shetani ili asimike utawala wake katika Taifa letu. Ni lazima tutaandamwa na laana mbalimbali.

Wanaojua biblia watakumbuka jinsi Mungu alivyowaadhibu wana wa Israel walipomkosea. Aliwatia utumwani hata wakawa watumwa wa tawala za kishetani. Na kutoka haikuwa kazi rahisi. Baadaye alipotubu, walirudishwa kwenye utawala wake. Watu walitubu baada ya kupewa ujumbe toka kwa manabii waliotumwa na Mungu.

Nani atakuwa nabii kwa watanzania? Nani atakayewaletea ujumbe wa Mungu ili watubu na hatimaye tuondoke kutoka kwenye utumwa wa utawala wa shetani?
 
Leo mnalalamika Ila kesho mkifanyiwa mema mnasahau....Chama Dola lazima kitawale
 
Kalia siasa ,huujui huu mchezo,Mbowe anawauza,mtakuja shtuka mmevaa kandambili za rangi tofauti.
 
Kupitia hizi chaguzi ndogo nimeshuhudia nguvu kubwa ya darasa la saba ikitumiwa ipasavyo!
 
J
Kosa kubwa katika maisha ni kuzaliwa na kuitwa Mtanzania toka viongozi wake wa Taifa hadi wananchi ni maiti na vichaa.
Watanzania wenyewe tupo na furaha na hujawa na furaha itamkwapo Tanzania tunajivunia kuwa Watanzania The Cradle of Human Kind.
Nyie manyang'au na mizoga ndio mnapata taabu na haya ndio yatakuwa maisha yenu
 
J

Watanzania wenyewe tupo na furaha na hujawa na furaha itamkwapo Tanzania tunajivunia kuwa Watanzania The Cradle of Human Kind.
Nyie manyang'au na mizoga ndio mnapata taabu na haya ndio yatakuwa maisha yenu
Mzoga umasahau ni baba yako na familia yako kukuza ktk maadili ya matusi mtoto wa laana ww
 
Kwa wakati huu hakuna chama cha upinzani imara chenye ubavu wa kuiyumbisha ccm, vyama vikuu chadema na cuf ambavyo vilikuwa vinategemewa kutoa upinzani mkali kwa chama tawala vyote vimepoteza mwelekeo, angalia chadema na cuf zilivyo sambaratika !!!! hakuna kitu kabisaaa !!! na bado vinazidi kusambaratika wamepoteza nguvu na umoja, hakuna tena upinzani zaidi ya unafiki !!!!

Hakuna wa kumlaumu, wajilaumu wenyewe , ni vyema mkajipanga upyaa.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom