Mwendokasi ni mateso!!

Mwendokasi ni mateso!!

Kwanza abiria wanakata tiketi, kisha wanasubiri gari zaidi ya saa moja.

Kinachosikitisha ni kuwa baadhi ya vituo havina viti vya kupumzika abiria wala vyoo.

Yaani abiria wa mwendokasi wamekuwa kama watumwa kwani ukisha ingia kituoni huwezi kutoka kwenda kujisaidia nje ya kituo kisha urudi na kuendelea na safari yako.

Endapo ukifanya hivyo lazima ukate tena tiketi, sasa jamani mnategemea watu wajisaidie wapi ilihali wanasubiri magari muda mrefu?

Bado tupo nyuma sana, hii yote inatokana na nafasi nyeti za uongozi kushikwa na watu wasio na ubunifu, kwa hali ya kawaida ilipaswa viongozi nao wawe wanasafiri kwa usafiri huo ili kuonja kero zake na kisha kuzifanyia kazi badala ya kusikilizia adha za usafiri huo jamvini
 
Hawawezi kupanda humo watakosa pumzi sie wenyewe tunapanda kwa vile hatuna usafiri mwingine, yaani wachukue hatua haraka hali sio nzuri kabisa hata maambukizi ya maradhi ni rahisi.
 
Kituo cha mwanamboka ( studio) Kwa njia ya kwenda Morroco kila siku kuanzia mida ya Saa 8 mchana tiketi hamna , wana print kituo kingine mnasubir lisaa zima , zikija mkienda kuscan inakwambia "wrong date", then wanakwambia pita direct, Pesa wanajua wanapopeleka,
 
Hawawezi kupanda humo watakosa pumzi sie wenyewe tunapanda kwa vile hatuna usafiri mwingine, yaani wachukue hatua haraka hali sio nzuri kabisa hata maambukizi ya maradhi ni rahisi.

Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli hebu sema neno moja tu! mwendokasi itakuwa kama ilivyokusudiwa
 
Aisee sasahivi niko hapa DIT kituoni, mabasi hakuna na kama likipita linakua limejaa kwelikweli.. Wanafunzi nao wanasota tu hapa.. Sad..
 
Kwanza abiria wanakata tiketi, kisha wanasubiri gari zaidi ya saa moja.

Kinachosikitisha ni kuwa baadhi ya vituo havina viti vya kupumzika abiria wala vyoo.

Yaani abiria wa mwendokasi wamekuwa kama watumwa kwani ukisha ingia kituoni huwezi kutoka kwenda kujisaidia nje ya kituo kisha urudi na kuendelea na safari yako.

Endapo ukifanya hivyo lazima ukate tena tiketi, sasa jamani mnategemea watu wajisaidie wapi ilihali wanasubiri magari muda mrefu?

Unaonaje sasa tukarudi kwenye ule utaratibu wetu wa KIMARA MWISHO-POSTA saa 2-3?
 
Back
Top Bottom