Mwendo kasi jeuri kweli, wanakupakia halafu wanakupitisha kituo

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,913
Eti mabasi ya mwendo kasi yako ya kawaida na mengine kasi ya express. Ujinga mwingi tu. Mara ngapi nimepanda magari yao hayana matangazo ya wazi yanapokwenda wala hakuna vipaza sauti na hakuna konda.

Nakusudia niteremke Magomeni wananipeleka mpaka Manzese. Nasubiri jengine la kuelekea mjini ili niteremke kituoni kwangu na kwa mara nyengine wananirudisha mpaka Msimbazi, Nikapanda jengine mambo yakawa kama hivyo Nikasema ujinga gani huu napanda daladala ya kawaida. Nikalipa nauli nyengine na nikakosa karamu ya shughuli ya harusi.

Kama mnataka maoni yangu. Basi kila basi liwe na tangazo kubwa ubavuni linakwenda wapi au wekeni konda asaidie kuzungumza na dereva wake kuwasaidia abiria.
 
Mbona huwa wanaweka kibao au karatasi imeandikwa express... Ukiona hilo usipande
 
Mwanzoni mbele mabasi mengi
Yalikuwa yanaonesha wapi yanakwenda,
Sahv mabasi mengi wanaweka box mbele limeandikwa wapi linapoenda
Ukishaona wamefikia huko jua mradi
Unaenda kimkandamkanda

Ova
Mwanzoni eti ilikuwa unascan tiketi na inaisha muda wake baada ya saa moja.Sasa wanachana halafu una hiyari kuichukua au kutupa kwenye debe la taka.
 
Soma mbele! hakuna gari lisilo na kibao
Umewahi kusafiria kweli mwendo kasi.Ukiwa mle kwenye banda hicho kibao utakiona wapi.Kuna mabadiliko lazima yafanyike ili haya magari yawe ya kisasa kweli.
 
Nimepita hapo juzi kwa kweli ni masikitiko sana especially kwa mti kama ni mgeni. Mabango ya nauli yanasoma 750 wakati ni 1250, vituo havitajwi na wahudumu jeuri wana assume kila mtu ni mwenyeji dsm.
 
Nimepita hapo juzi kwa kweli ni masikitiko sana especially kwa mti kama ni mgeni. Mabango ya nauli yanasoma 750 wakati ni 1250, vituo havitajwi na wahudumu jeuri wana assume kila mtu ni mwenyeji dsm.
haya mabasi lazima yafanyiwe mabadiliko haraka na ya maana. Lazima kwanza yatenganishwe njia yanakoishia kwa kuwekwa rangi tofauti na upande wa kupanda abiria liandikwe kwa uwazi mfano GEREZANI/MWENGE. Kuna vijana na wazee wastaafu wanaotumia hayo magari wote pamoja.
 
Umewahi kusafiria kweli mwendo kasi.Ukiwa mle kwenye banda hicho kibao utakiona wapi.Kuna mabadiliko lazima yafanyike ili haya magari yawe ya kisasa kweli.

kila siku napanda mwendo kasi!
 
Back
Top Bottom