Kero za Rushwa Trafic kituo cha Mwendo Kasi - Ubungo Kibo

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
67
125
Hivi karibuni Trafic Police wanakaa sambamba na kituo cha Ubungo Kibo kuzuia magari yasipite njia ya mwendo kasi (kuelekea Ubungo). Sambamba na kituo hicho, kuna kituo cha daladala pia na bajaji zinapakia na kushusha.

kutokana na pilikapilika mahali hapo, waendesha magari kuna wakati wanalazimika kupishana kwa kusogea upande wa mwendo kasi ili kuzuia msongamano wa magari au kujihepusha kukwanguana na bajaji/daladala. Kitendo cha kukanyaga msitari wa upande wa mwendo kasi, gari inakamatwa na kuambiwa kwamba umefanya kosa la kupita njia ya mwendo kasi.

Wanakutia hofu kwamba kutokana na kosa hilo, utawekwa ndani badaye kupelekwa mahakamani na ili kukomboa gari utatakiwa kulipa TZS600,000. Wengi wanajitetea mwishowe unaambiwa ulipie makosa 3 hadi 5 (90,000 hadi 150,000) ili wakuachie. Hela hizo zinalipwa mfukoni mwao.

Vyombo husika viliangalie hili tatizo na kuondolea raia wema kero

- za kubambikiza makosa kwa nia ya kujinufaisha.

- za kuwachelewesha kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi

hawa maaskari wapo hata leo trh 07 Jul, 2020 na wanaendelea na usumbufu huo kwa raia wema. Tafadhari vyombo husika liangalieni hili kuondoa usumbufu husio wa lazima kwa waendesha magari.
 

Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,628
2,000
Toka mwaka huu uanze trafik wamekuwa wakali sana...kuna hawa wanasimama shekilango road utawakuta pale golden fork na Mugabe.

Yani unaona mtu analitafuta kosa kbs ilimradi akuandikie cheti tu
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,044
2,000
Ile foleni pale tazara Kama unatokea taifa /bandarini kuelekea ubungo ...hawavuti magari ya upande huo Sasa nikasema nipite service road ya kulia nikachepukia mataa ya Serengeti moja kwa moja Hadi mataa ya sokota nikamkuta Askari akanionyesha niendelee ili nikachepukie kiwanda Cha sigara Kisha narudi mataa ya tazara ..hapo katikati nikakuta wamekatama magari kibao na mimi nikiwemo eti kwanini tumepita service road ya upande wa kulia ...ndio ikawa mwendo wa buku tano au cheti

Sent using Jamii Forums mobile app
 

joshua_ok

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
12,876
2,000
Ile foleni pale tazara Kama unatokea taifa /bandarini kuelekea ubungo ...hawavuti magari ya upande huo Sasa nikasema nipite service road ya kulia nikachepukia mataa ya Serengeti moja kwa moja Hadi mataa ya sokota nikamkuta Askari akanionyesha niendelee ili nikachepukie kiwanda Cha sigara Kisha narudi mataa ya tazara ..hapo katikati nikakuta wamekatama magari kibao na mimi nikiwemo eti kwanini tumepita service road ya upande wa kulia ...ndio ikawa mwendo wa buku tano au cheti

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado hukuona una makosa?
 

hoffman

Senior Member
Jul 21, 2011
179
250
Wale ni kuwaregesha tu na TAKUKURU. Wameshanivunja 150k, nina hasira nao hadi leo.
 

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Toka mwaka huu uanze trafik wamekuwa wakali sana...kuna hawa wanasimama shekilango road utawakuta pale golden fork na Mugabe.

Yani unaona mtu analitafuta kosa kbs ilimradi akuandikie cheti tu
yes, kama mwaka jana walijisifu kuongeza mapato, sasa mwaka huu itabidi wavunje rekodi ya mwaka jana!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
67
125
Trafic wanafanya kazi nzuri ukizingatia hali ya sasa ya utii wa sheria za barabarani na kupungua kwa idadi ya ajari. Lakini
kwa issue ya Kituo cha Mwendo kasi cha Kibo wanaitumia kama chambo cha kupambana na makali ya December/January. Si vyema kuwafanya raia wema vitega uchumi kwa kubambikiza makosa.

Nahamini wakuu wataliona hili na kulitolea mwongozo.Ukweli inaudhi hadi mtu unatamani ingilie hata barabara ya mwendo kasi Kimara ili ukihadhibiwa useme kweli I did it siyo hivi wanavyofanya!.
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,455
2,000
Mimi kila siku naona wamekamata magari kibao, huwa sijui kosa ni nini. Kumbe ndo hilo kupenya kidogo kwenye mwendo kasi!

Hawa maaskari basi ni watata, mbona kunamaeneo mengi kama hayo? na magari yanapenya kama eneo la mwendo kasi liko wazi na mabasi yamepaki kumaliza eneo zima?. Tusema wanatumia hiyo nafasi kujichotea pesa kutoka kwa raia. ndilo tatizo la nchi masikini na isiyofuata sheria ambavyo kila mwenye mamlaka ni kama mfalme.
 

esokero

Member
Dec 29, 2019
85
125
Kwa nn ufanye kosa ulaolifaham Ni kosa ,wewe hukuona au huoni umevunja Sheria barabarani ,Kati ya laki 6 au laki 150 Bora lipo,,Traffic wanafanya Kaz nzur
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,882
2,000
DISPLEI,
Huenda wewe ni muhanga wa kweli wa usemayo.
Upande wa pili wa sarafu kuna madereva vichaa jana tu kuna mmoja alitaka atugonge watu hapopo Kibo kwenye zebra crossing, wenzie wamesimama kupisha watembea kwa miguu, yeye kawaona hawana haraka katanua kulia kaingia njia ya mwendokasi pembeni ya kituo cha mwendokasi kwa speed kubwa nusura atuuwe.

Namba zake ni gari la binafsi sio la umma, bahati mbaya nilikuwa na haraka na safari yangu sikushika namba zake ningeweka hapa atafutwe yule dereva hatari kwa maisha ya watu.
 

Akili Sina

JF-Expert Member
Jan 18, 2018
267
500
DISPLEI, Mkuu pole sana, hii imekuwa kero sana, hapa Mimi nipo njian naenda kumekea mdhamana jamaangu pale town, kesi ni hiyohiyo kisa eti kakanyaga mstari wa mwendo kasi na kulikuwa na songamano.........hata hivyo hii ya kwako imetokea 07 /7 2020 , au itakuwa ni typing error

Sent using Jamii Forums mobile app
 

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
67
125
Mkuu pole sana, hii imekuwa kero sana, hapa Mimi nipo njian naenda kumekea mdhamana jamaangu pale town, kesi ni hiyohiyo kisa eti kakanyaga mstari wa mwendo kasi na kulikuwa na songamano.........hata hivyo hii ya kwako imetokea 07 /7 2020 , au itakuwa ni typing error

Sent using Jamii Forums mobile app
Typing Error leo Jumanne January 07, 2020
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom