Ni Mradi ulioanza kwa mbwembwe tukaahidiwa mambo mengi mazuri ikiwepo uzingatiwaji wa muda wa kukaa kituoni, tukawa tukionjeshwa matangazo ya kila kituo, ndani kulikuwa na Camera kuangalia wizi ndani ya bus, kulikuwa na ubao wenye taa, mbele na ubavuni ukionyesha mwelekeo wa gari na muda utakaotumika kufika vituoni, madereva walikuwa smart kwenye Uvaaji uniform hadi uendeshaji. Leo hii imefika mahali tunazitamani daladala zetu tulizikuwa tukiingilia madirishani.
Tumezikumbuka kwa sababu MwendoKasi haizingatii muda, ukikata ticket utakaa si chini ya lisaa kituoni ukisubiri bus lije ambapo hakuna tofauti na tulivyokuwa tukichelewesha kwenye foleni na daladala. Ukiingia ndani ya Mwendokasi ni kusukumana na kukanyagana
Ndani ya Mwendokasi kuona mtu mzima au mtoto akizimia kutokana na kukosa hewa kutokana na msongamano ni kitu cha kawaida kabisa. Ndani ya Mwendo kasi hakuna kutangaziwa vituo tena Kama zilivyokuja Kituoni abiria wamejaa kusubiri bus, dereva anawapita abiria gari ikiwa tupu kabisa, anaamua yeye ni wapi akachukue abiria.
Ndani ya bus la mwendo kasi kuna viti vimetengwa maalum kwa Wazee, wajawazito na Vilema, hakuna dereva anayeelewesha abiria kupisha hawa waliotengewa viti vyao. Madereva wa mabasi haya ni bora wale wa daladala zetu wanaendesha hovyohovyo kama wamebeba magunia ya mkaa au mikungu ya ndizi.
Ndiyo maana nasema Mradi huu unaenda kufa wakati wowote. Ushahidi ni jinsi mabasi mabovu walivyoyajaza vituoni yakiwa yameondolewa hadi matairi. Nenda Kimara, Kivukoni hadi Gerezani yamejazana utafikiri hizo stand ni Garage, hapo wananchi hatujashuhudia kule ndani ya yard yao pale jangwani.
Nitoe ushauri kwa serikali kuwarudishia wamiliki wa Daladala kazi yao. Serikali na Kisena mmeshindwa huu Mradi,hata Kama Kisena yupo Jela, tunajua serikali na yenyewe ni mbia kwenye huu Mradi.
Mnakwama wapi?.