Mwema naye apangua mabosi Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwema naye apangua mabosi Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmbangifingi, May 5, 2012.

 1. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Ally Mwema amefanya mabadiliko kadhaa ya makamanda wa polisi Mikoa ambapo Kamuhanda ameondolewa Ruvuma na kupelekwa Iringa, Andengenye Thobias katolewa Arusha na kurejeshwa Makao makuu.

  Je; Kamuhanda anaondolewa baada ya tume iliyoundwa kuchunguza mauaji yale ya polisi dhidi ya raia? Arusha amepelekwa Sabas ambae ni mwana mabadiliko,atasapoti harakati za cdm na kumdhibiti Mwombeki Zuberi?
   
 2. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Source: Please
   
 3. w

  waku Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mkuu tupe madiliko yote nani kaenda wapi
   
 4. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Habari zilizotufikia punde zinasema IGP Mwema naye ameafuata nyayo za Rais Kikwete kwa kupangua makamanda wa polisi katika ngazi mbalimbali. kwa taarifa zaidi subirini kidogo nitawajuza.
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Haya twasubiri
   
 6. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hamjui kwamba IGP mwema ni peopleeees! Kapeleka mtu wa kurekebisha mambo ili CDM iingie Ikulu kiulaini.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ngoja niende kwenye viti virefu kufurahia Andengenye kun'golewa.
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  nani kakudanganya?endelea kujifariji.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa wana Iringa mna haki ya kulalama kila anayeharibu huletwa apo.
  RC katoka songea kaja iringa the same to RPC
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kama kigezo cha kumwondoa Andengenye ni kushindwa kuthibiti moto wa CDM, hata Mwema mwenyewe angeletwa Arusha asingeweza.
   
 11. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mangala anaenda Shinyanga, Iringa ntamkumbuka kwa kupunguza kiasi ya uchafu wa askari traffic
   
 12. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  ni mchaga,inajulikana.
   
 13. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nzenga kaya mbona unaendekeza sana ukabila ndugu,au wewe ni puppet from Rwanda,hata wao siku hizi wanazungumza lugha moja.Duh!
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naona umeingia mitini!
   
 15. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mwenye orodha aluletee tafadhali. Me nimesikia redioni kwenye mapitio ya magazeti, imesomwa title tu. Huku kijijini hadi nipate gazeti ni baada ya siku mbili.
   
 16. senior citizen

  senior citizen Member

  #16
  May 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mwenye orodha tunaomba atujuze kwani sehemu nilipo sina access ya kupata gazeti.
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  IGP Saidi Mwema amefanya mabadiliko katika jeshi.....
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP), Saidi Mwema amefanya mabadiliko katika jeshi hilo kwa kuwahamisha makamanda wa polisi wa mikoa kadhaa, kuwateua makamanda mapya na wakuu wa vitengo ndani ya jeshi hilo.

  Katika mabadiliko hayo ambayo utekelezaji wake utaanza Juni 1, mwaka huu, IGP Mwema pia amewateua makamanda wa polisi wa mikoa mipya minne ya Geita, Njombe, Simiyu na Katavi.

  Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Advera Senso alisema jana kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuimarisha utendaji ndani ya jeshi hilo, pia kutekeleza maboresho (reforms) yanayoendelea kufanywa.

  ASP Senso alisema miongoni mwa maboresho hayo ni kuundwa kwa vikosi vitatu maalum vitatu vipya vya polisi ambavyo ni Mazingira (Enviromental Police Unit), Utalii (Tourism Police Unit) na Migodi ya Madini (Mining Police Unit).

  Alisema katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Thobias Andengenye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Utawala na Rasilimali, Polisi Makao Makuu na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa RPC Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Liberatus Sabas.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Adolfina Chialo amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi (CID – HQ) na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ilala, ACP Fautine Shilogile.

  Mabadiliko mengine yamewagusa RPC Kilimanjaro, SACP Absalom Mwakyoma ambaye amehamishiwa mkoani Mara akibadilishana na RPC Mara, ACP Robert Boaz ambaye amehamishiwa mkoa wa Kilimanjaro.

  Senso alisema RPC Ruvuma, SACP Michael Kamuhanda amehamishiwa mkoani Iringa kuchukua nafasi ya ACP Evarist Mangala ambaye amehamishiwa mkoa wa Shinyanga, wakati aliyekuwa kamanda wa Shinyanga, ACP Diwani Athumani amehamishiwa mkoani Mbeya kuendelea na wadhifa wake huo.

  Aliyekuwa RPC Mbeya, ACP Advocate Nyombi amehamishiwa Ofisi ya Upelelezi Makao Makuu katika kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini huku aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Ferdinand Mtui akiteuliwa kuwa mkuu wa kikosi hicho nchini, kuchukua nafasi ya SACP Anaclet Malindisa ambaye anastaafu.

  Makamanda wa Polisi wapya wa mikoa walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu mkoani Arusha, ACP Akili Mpwapwa (RPC Manyara), aliyekuwa Ofisa wa Opareshini Mwanza, ACP Philipo Kalangi (RPC Kagera) aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Arusha, ACP Leonard Paul (RPC Geita) na aliyekuwa Ofisa Mnadhimu mkoa wa Dodoma, ACP Furgence Ngonyani (RPC Njombe).

  Wengine ni Ofisa wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Marieta Minangi (RPC Ilala), ACP George Mwakajinga aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Lindi anakuwa RPC Lindi, ACP Linus Sinzimwa kutoka CID Makao Makuu anakuwa RPC Singida na ACP Salum Msangi pia kutoka CID Makao Makuu anakuwa RPC Simiyu.

  Senso alisema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa Makao Makuu ACP Dhahir Kidavashari anakuwa RPC Katavi, RCO Mwanza, ACP Deusdedith Nsimike anakuwa RPC Ruvuma, ACP Saada Juma Haji ambaye ni Ofisa Mnadhimu Ilala anakuwa Kamanda wa Kikosi cha Reli Dar es Salaamn na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Arusha, ACP Amir Konja anahamia Dar es Salaam kuendelea na kazi hiyo.

  Walioteuliwa kuwa wakuu wa vikosi vipya ni ACP George Mayunga kutoka CID Makao Makuu anayekuwa mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Mazingira, kikosi cha Ulinzi wa Watalii kitaongozwa na ACP Benedict Kitarika kutoka Kitengo cha Sheria na Utafiti Makao Makuu na ACP Deusdedith Katto kutoka Oparesheni Makao Makuu ataongoza Kikosi cha Ulinzi wa Migodi ya Madini.

  Senso alisema mabadiliko hayo pia yamevigusa vyuo vya polisi ambapo aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, SACP Elice Mapunda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mafunzo Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukukiwa na Mkuu wa Chuo cha Kidatu, ACP Ally Lugengo.

  Mkuu wa Mafunzo katika Chuo cha Polisi Moshi, ACP Nasser Mwakambonja amehamishiwa Kidatu ambako anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo hicho wakati aliyekuwa Mkuu wa Mafunzo SACP Abdulrahman Kaniki ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Utafiti cha Jeshi hilo.

  Senso alisema maofisa wanaotarajiwa kustaafu utumishi wao ni Mkuu wa Mafunzo wa Kitengo cha Sheria na Utafiti, SACP Donald Kaswende na baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

  Makamanda hao na mikoa yao kwenye mabano ni SACP Henry Salewi (Kagera), ACP Sifueli Shirima (Lindi) SACP Celina Kaluba (Singida) na Mkuu wa Usalama Barabarani Kada Maalum ya Dar es Salaam, ACP Vitus Nikata........
   
 18. b

  bob malya JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  heri andengenye wa arusha kaenda utawala wa rasilimali DSM.kwani hapa arusha kazi yake ilikuwa ni kuwadhibiti cdm badala ya majambazi .andengenye nenda nenda katawale rasilimali kwani arusha uliishindwa nenda nenda kamanda wa ccm
   
 19. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  First angeweka traffic police wote on mark time tujipange upya.
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kansa huwaga haiguswi hata kidogo, ikiguswa inasambaa. Tubakie hivi hivi na traffiki wetu, mpaka kifo kitukute
   
Loading...