BAK,
Sidhani kama umemaanisha ambacho umekiandika hapo!
Katika ma-IGP walio tenda kazi nzuri kwenye nyanja ya usalama wa raia na mali zao ni huyu IGP ndiye anae ibuka kidedea.
Huwezi kupima tu Tanzania ya leo katika mambo ya kiuhalifu na ile ya enzi za Mkapa na Mwinyi?
Leo hii ujambazi na unyang'anyi ni kama hadithi vile, matukio ya aina hii ni ya kutafuta na tochi, unadhani hali hii imetokana na nini?
Hayo matukio uliyo eleza ni kweli yametokea wakati wake, ila yakupaswa uelewe kuwa uhalifu unazidi kukua, huwezi kufananisha mbinu za uhalifu za mwaka 1947 na za leo, hivyo jitihada ni kubwa za kupambana na matukio ya aina hiyo ndio maana hutokea mara chache chache.