Mwema kung'atuka?


Majibu makini sanaa, kwa swali ambalo mhulizaji ajitambui, Habari za Iramba HAMY-D
 
IGP Mwema kiukweli alipoteuliwa alitegemea kufanya kazi za kiuadilifu kama vile alikotoka, lakini imekuwa sivyo ndivyo amejikuta akitumika kwa masilahi ya vigogo wachache wasioguswa [wakijifanya wako juu ya sheria] wakijinufaisha kupitia mgongo wa vyombo vya usalama, Jeshi la Polisi na usalama wa Taifa.

Lakini ieleweke kuwa kila kitu kina mwisho. IGP Mwema amekwisha liona hilo, anajaribu kujinasua kwenye mtego huo, angalau dhambi hiyo impitie mbali angalau Mola wake amsamehe yale maovu yaliyotendeka usoni pake.

Mimi naona kafanya vizuri tu kung'atuka maana amekwisha ona kitakachotokea huko mbele kuwa sio kizuri, ni balaa linakuja la kuwahujumu raia wema.
 

Nakubaliana kabisa. Hata rushwa barabani imeongezeka sana. polisi wanaomba rushwa wazi wazi. katika kipindi chake hili limeongezeka zaidi.
 
BAK,

Nini maoni yako kwa maamuzi yanayo tarajiwa kufanywa na IGP Mwema!!?

Ninasubiri afanye hayo maamuzi hayo kwanza ndiyo nitoe maoni yangu. Kwa sasa hizi zinabaki kuwa tetesi tu.
 
Tusije kushangaa tukisikia Kamuhanda anarithi kiti cha Mwema..
Manake hii nchi ukiua ndiyo unapandishwa cheo!
 
Tatizo lako, unajibu kwa hisia na upenzi wa awamu. Utendaji katika utumishi unapimwa kwa vigezo vinavyokubalika. Kama kigezo ni idadi ya matukio ya ujambazi badala kuamka usingizini na kusema matukio yamepungua. Hata kama ni idadi ya matukio, matukio pia yanapishana kwa uzito. Nidhamu ya jeshi la polisi ndiyo msingi wa utendaji bora wa jeshi husika. Kwa sasa hivi watu hawendi tena polisi kutaka msaada. Polisi ya sasa mlalamikaji atozwa rushwa malalamikiwa anatozwa. Na hakuna atakayefanikiwa mpaka mlalamikaji atakapojitoa mwenyewe kwa kuchoka kufuatilia. wananchi wanajiuliza kama nimeibiwa na sasa naibiwa tena na polisi, kuna faida gani
 
Hakuna kitu kinachoniudhi kama hili dafu la msoga linavyopindisha sheria na kanuni kienyeji enyeji kwa kuwaongezea hawa watu muda wa utumishi bila misingi ya kueleweka. Alinza na Katibu mkuu kiongozi Bwana Luhanjo, akamuongezea VC wa UDSM, Mzumbe na UDOM, akaja Mwema na Kova na wengine labda siwajui. Hivi ni kweli hakuna watu wenye capacity za kuhandle hizi nafasi? Huu si uvunjanji wa sheria na taratibu za utumishi wa umma bila sababu?
 
Kama Kikwete alimleta Mwema afanye mabadiliko katika jeshi la polisi basi he is a disastrous failure. Jeshi la polisi chini ya Mwema halina tofauti na jeshi la polisi chini ya Mahita.
 
Kile kiti ni cha moto kweli kweli. Atakayechukua baada ya IGP Mwema lazima awe very strong. Anaweza dondoka na presha
 
Propaganda ambazo hazina ukweli wowote ndio kazi zenu nyie. Kama huoni wala husikii jinsi jeshi la polisi lilivyopoteza heshima yake hata ashuke Mungu kukwambia hivyo huwezi kumuamini. Mie nimemaliza.
BAK,
Ukiangalia watu waliompa "like" kama Faizafoxy unaelewa tu kuwa hawa watu wanaendeshwa na kitu kimoja tu. Uislamu wa Mwema.
 
Reactions: BAK

Asante sana kwa kunifundisha heshima!
 
BAK,

Nini maoni yako kwa maamuzi yanayo tarajiwa kufanywa na IGP Mwema!!?

Kahofia kuendelea kupoteza sifa yake kwa jinsi jambavyo ccm wanavyolitumia jeshi la polic visivyo
 
Last edited by a moderator:

Mkuu HAMY-D ,

IGP Mwema Mema yake yote yanafunikwa na Udhaifu wake Uliopelekea Polisi kuwa ni Sehemu ya CCM.
We imagine Polisi wana execute task zao based on Malekezo ya Mwigulu.
 
Last edited by a moderator:
Ukiona hivyo kashajibebea chake kama kawaida ya ccm na wadau wake na sasa kaamua ajitoe fasta kuachia ngaz
 
kwa mtazamo wangu mwema umeona mbali na umfikilia mbali kisha ukaona kilichoko mbele yako faida zake na hasara zake halafu ukachukua uamuzi sahihi. hongela kwa hilo.
 
Damu nyingi sana ya watu waliouawawa na JESHI LA POLISI bila hatia itaendelea kudaiwa mikononi mwake SAID MBAYA,hasa MIGODINI kama Northmara,Chacha Ngoka,Clever na wengineo wako kuzimu ,they are waiting for you IGP SAID MWEMA.
 
Mwema ashtakiwe kwa kuyafumbia macho madhambi ya askari wake. Polisi sasa ni majambazi.
 
alitakiwa kustaafu hata kabla ya kuwa appointed.
 
BAK,
Ukiangalia watu waliompa "like" kama Faizafoxy unaelewa tu kuwa hawa watu wanaendeshwa na kitu kimoja tu. Uislamu wa Mwema.

Angalau Mahita alikuwa anaogopwa na polisi
alikuwa na heshima na hata Mkapa alikuwa anamheshimu Mahita
walikuwa na uwezo wakiamua...uhuni ulikuwa wa makusudi

sasa huyu Mwema ulisikia wapi jeshi la polisi likaahiti kutoa mlioni 100 ili kupata lead ya uchunguzi
na wasipate kitu? hiii ni comedy...sio jeshi la polisi
 
BAK,

Nini maoni yako kwa maamuzi yanayo tarajiwa kufanywa na IGP Mwema!!?

Kama muda umefika kisheria, Apishe ofisi. Siamini kama hakuna wengine wenye sifa za kushika ofisi hiyo.
Hata kama atakaa huo muda, Baada ya hapo si atakuja mwingine?. ya nini kuyaogopa maji hali ya kuwa ni lazima uoge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…