SoC01 Mwelekeo sahihi wa maendeleo Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Magalu Empire

New Member
Sep 14, 2021
0
0
MWELEKEO SAHIHI WA MAENDELEO YA TANZANIA
Maendeleo ni mchakato unaounda ukuaji, azimio, mabadiliko chanya, kupiga hatua, uchumi, mazingira, kijamii na idadi ya watu.

Kusudi la maendeleo ni kupanda kwa kiwango na ubora wa maisha ya watu pamoja na upanuzi wa mapato ya jumla na fursa za ajira bira kuharibu rasilimali za mazingira.

Pia maendeleo ni kama zana inayowezesha watu kufikia kiwango cha juu cha uwezo wao kwa kupeana uhuru wa kutenda, yaani uhuru wa vitendo vya kiuchumi, kijamii na kiifamilia. Nchi yoyote duniani ili iendele ni lazima ifanye utambuzi sahihi wa mwelekeo na njia sahihi za kimaendeleo zitakazowezesha kupiga hatua kutoka kwenye hali duni kwenda kwenye hali bora, vilevile kwa nchi yetu ya Tanzania tunalojukumu kubwa kuunda na kuimalisha mwelekeo sahihi wa kimaendeleo kulingana na mahitaji yetu ya sasa na ya baadaye, kwa kupeana uhuru, kuboresha huduma za afya, kuboresha mfumo wa elimu, kuimalisha usalama wa jamii na rasilimali za nchi, kuimalisha uchumi, kutengeneza fursa za ajira, kuboresha miundombinu, kilimo, usawa wa matumizi ya rasilimali za nchi, matumizi sahihi ya sayansi na teknolojia pamoja na siasa safi.

Uhuru
Uhuru ni kufanya ama kusema ulitakalo bila kushulutishwa na bila kukera wengine. Kakika maendeleo uhuru ni kuruhusu watu wawe huru kujadili, kuzungumza, kukosoa, kubishana vijiweni, mashuleni, vyuoni na migahawani, kwa uhuru huo utasaidia kubaini mielekeo mbalimbali ya kimaendeleo. Kwa matiki hiyo serikali ya Tanzania inalojukumu kubwa kuruhusu wasomi na watanzania wote kuchochea na kuanzisha mijadala mbalimbali ya kimaendeleo ili kuisaidia serikali katika kutunga na kuimalisha sera mbalimbali za kimaendeleo.

Kuboresha huduma za afya.
Afya ni ile hali ya ukamilifu kimwili, kiakili, kijamii na kutokuwepo kwa maradhi. Bila shaka afya ni mtaji namba moja wa kila mwanadamu, bila kuwa na afya njema huwezi kufanya shughuri yoyote ya kimaendeleo. Hivyo basi serikali na wananchi kwa ujumla tunapaswa kuliweka swala la afya zetu kuwa namba moja kwa kuimalisha miundombinu kama vile kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba muda wote. Pia serikali ihakikishe kila mwananchi anauwezo wa kumudu gharama za matibabu kwa kuimalisha na kuhakikisha kila mwananchi amekata bima au kuwa na bima kwa gharama nafuu ili kujiwekea uhakika wa kitibiwa muda wote.

Kuboresha mfumo wa elimu.
Katika upande wa elimu mimi nigependa kushauri kuwa tufanye marekebisho katika mfumo wetu wa elimu kwa kubadilisha kutoka mfumo wa kikoroni kwenda elimu ya kukizi mahitaji yetu kwa kuzingatia mazingira yetu tuliyopo, kwa mfano nashangaa sana kuona somo la standi za kazi kutokupewa kipa ubele ili hali linalenga maisha yetu moja kwa moja. Katika hili nashauri pia kuwepo na masomo rafiki yanayoendana na mazingira yetu kwa shule za misingi na sekondari, kama vile somo la kilimo na ufugaji, uvuvi na kadhalika ili kusudi mtoto anapokuwa anakuwa na ujuzi utakao muwezesha kujiajili katika shughuli kama hizo ambazo zimebeba uchumi wa Tanzania kwa asilimia kubwa. Pia nashauri kuwa kwa upande wa vyuo wapunguze muda wa kukaa darasani na vilevile waongeze muda wa kujifunza kwa njia ya vitendo (field), Kwa mfano kwa wale wanao soma miaka mitatu iwe miaka miwili ya darasani na moja kazini kwa ajili ya kumjengea mhitimu uzoefu mkubwa kazini, pia ikiwezekana muda wa likizo upunguzwe kutoka miezi mitatu hadi wiki tatu au mbili kwa ajili ya kukamilisha mada zote ndani ya miaka miwili ya darasani.

Kuimalisha usalama wa jamii na rasilimali za nchi.
Usalama ni udhibiti wa hatari zinazotambuliwa au ni ile hali ya kuwa salama. Usalama humfanya mtu kuwa huru. Katika swala la maendeleo usalama ni nguzo mhimu sana ambapo kama nchi inatakiwa kuimarisha usalama katika mazingira yote ya rasilimali za nchi kama vile ardhi, fedha, watu, msitu, wanyama, madini, maji, mipaka na kadhalika ili rasilimali zote ziweze kusaidia wananchi wake kwa kuzuia na kupambana kwa vitendo vyote vya kiharifu kama Rushwa, Ujambazi, wizi, utekaji, uporaji, ubakaji, ugaidi, utumiaji wa madawa ya kulevya, nk.

Kukuza na Kuimarisha uchumi
Katika swala la uchumi ni dhahili kuwa nguzo mhimu katika kukuza na kuimalisha ni uwekezaji. Kwa Tanzania tunapaswa kuongeza uwekezaji wa umma na wa watu binafsi katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kilimo, Viwanda, Utalii, biashara, mifugo, madini, usafirishaji, utamaduni na michezo ambazo zinatoa faida pana kwa jamii, kwa kuzalisha ajira nyingi, pamoja na kuboresha miundombinu ya maji, nishati, barabara pamoja na elimu na mafunzo. Pia serikali iwekeze katika sayansi na teknolojia katika kukusanya mapato ya nchi kwa kuimarisha mfumo mzima.

Mwisho ninapenda kuwashukru JamiiForums kwa kuanzisha mijadala muhimu kama hii inayochea ukuaji wa maendeleo ya nchi yetu. MUNGU AWABARIKI
 
Back
Top Bottom