Innocent Prim M. MungyKulingana taarifa Zetu, tatizo hili lilikuwepo miaka mitatu nyuma Na lilitatuliwa baada ya leseni kutolewa Kwa mawasiliano Kwa mhusika na hakuna taarifa yeyote ya roaming Kwa wananchi Wa loliondo. Ofisi yetu ya kanda pamoja Na maafisa toka Makao Makuu wakati huo walithibitisha kuwa kulikuwa Na tatizo hilo wakati huo Na lilitatuliwa. Kama hii taarifa ni sahihi Kwa sasa, Mamlaka itafanya uchunguzi Na kuchukua hatua za kisheria kwani ni kosa kufanya hivyo. Naahidi kuleta taarifa hii mara ikithibitika pamoja Na hatua zitakazochukuliwa.
Mwarabu wa Loliondo amefunga BTS pale Loliondo ambayo ina Sattelite Link to Kwao Huko (Kwenye Network ya Kwao)
Watu wakipita yale Maeneo, simu zao zina detect kuwa pale kuna Best signal so zina Trigger Roaming.
" Ni kama Vile unapotua Armsterdam na Kuwasha Simu yako"
Thats Why watu wanapata zile Announecement za "Welcome to UAE..."
QUESTIONS..
Huyu Mwarabu BTS yake ina Transimit kwa Frequency zipi????
TCRA, nani amempa huyu Mwarabu Hizo Rights???
Nani amempa huyu Mwarabu Frequency na Kufanya huu upuuzi Tanzania
Je ana Licence za Kufunga hiyo BTS???
Je wa Tanzania wanapo Roam kwenye coveregae ya ile BTS, si wanakuwa charged Katika Roaming Rates???
Roaming rates si ziko Juu!!!!!, hamuoni kuwa watu wa wanapo roam na Kufanya Transaction e.g calling wanakuwa wanaingia extra cost za Roaming wakiwa Nchini mwao???
Au TCRA hawalijui Hili au wanalijua na Wanajua kuwa Wa Tanzania Hawajui lolote katika hili so ni Style ya Funika Kombe!!!!!!
cc Pasco , John Mnyika , Zitto , Mfikishie Huu Ujumbe Rafiki Yako Makamba
KEY
BTS: Base Transiver Station === Radio ambazo zina uwezo wa Ku tuma na Kupokea Mawasilianao kati ya Simu na Mnara (Ziko kwenye Mnara wa Simu)
Kulingana taarifa na rekodi zetu, tatizo hili lilikuwepo miaka mitatu iliyopita (2009) na lilitatuliwa baada ya leseni ya mawasiliano kutolewa na kuzuia kutumika kwa mtambo uliopelekea wakazi Wa Loliondo kufanya roaming ndani ya nchi yao. Mmhusika alipewa leseni na tangu wakati huo hakuna taarifa yeyote ya roaming kwa wananchi wa loliondo kwa sasa. Ofisi yetu ya kanda pamoja Na maafisa toka Makao Makuu wakati huo walithibitisha kuwa kulikuwa na tatizo hilo wakati huo na lilitatuliwa. Kama hii taarifa ni sahihi kwa sasa, Mamlaka itafanya uchunguzi Na kuchukua hatua za kisheria kwani ni kosa kufanya hivyo. Tunaahidi kuleta taarifa hii mara ikithibitika pamoja Na hatua zitakazochukuliwa. Jambo hili linakatazwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki Na Posta No. 3 ya Mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.
Endapo itabainika kuwa hali hii imejirudia tena, basi TCRA itachukua hatua kali kama ilivyofanya mwanzo. Tunaahidi kutoa taarifa baada ya uchunguzi.
Asante Kwa taarifa hizi.

Tunasubiri confirmation kama ulivyohaidi maana hili suala ni serious sana.
Pia unaweza kufafanua hiyo leseni ya mawasiliano aliyopewa mhusika?
Nilichojifunza ni kwamba wananchi hawatoi Taarifa kwenye vyombo husika pale wanapoona kuna Tatizo, yawezekana hii hali ingekwisha pata ufumbuzi muda mrefu,
Nazani kuna ile imani kwamba mamlaka ziko kila kona na hazihitaji support ya wananchi,
Halafu mbona wananchi tumekuwa watu wa kulia bila kutoa taarifa? nime mtag facebook msemaji wao in 2min ametoa hii responce tuwa polisi jamii, tutoe taarifa kwa kila jambo mengine tunaweza lalamika bure

Ni kweli organ za serikali ziko weak lakini naona TCRA wanajitutumia, ni wakupewa ushirikiano na kuwabana pale inapobidi, tatizo kila kitu ni siasa siku hiziSijui lakini kuna mamlaka nyingine hata ukiwapa taarifa hawafuatilii au wakifuatilia wanafanya hivyo kwa muda wanaoutaka.
At least TCRA wametuhabarisha kulingana na taarifa walizonazo, unless there is a different story on the ground.
Namba zao za simu tunazo tukiona kimya baada ya muda ni kuwashitua kujua nini kinaendelea, wakifanya usanii basi jibu tutakuwa tumepata, wakiwajibisha jibu tutakuwa tumepata pia kwamba hakuwa na taarifaNi vizuri ikithibitika kwamba madai haya yana uzito basi leseni isimamishwe kwa muda.
Kamanda Kazi, ZUKU hawako kwenye kuwajibika kuonesha local channels. ZUKU Na DSTV wako kwenye mfumo tofauti Na Mabadiliko ya kutoka Analojia kwenda Dijitali. ZUKU Na DSTV wako katika mfumo Wa Satelite ambao ni Wa dijitali tangu zamani. Mfumo huu ni Wa Malipo, ili uone channel local, kwanza lazima yawepo makubaliano kati ya Content Service Providers (mtengeneza maudhui) pamoja na Mtoa huduma. Lazima kulipia huduma hii kuona kwani ni ya malipo (subscription service).
Channel ZA bure zinatakiwa kuonekana katika mfumo Mpya Wa Utangazaji Wa dijitali Wa Terrestrial Digital Broadcasting ambao, channel zote zilizokuwa zinapatikana kupitia Terrestrial Analogue Broadcasting bure zinapaswa kuwa katika kila kingamuzi Cha watoa huduma watatu wanaotoa huduma hii (Multiplex Operator) yaani Agape Associates, Basic Transmission pamoja Na Star Times, na hii ni Kwa mujibu Wa Sheria. Watoa huduma wote watatu wametekeleza matakwa haya ya sheria.
Aidha ifahamike kuwa hata katika mfumo Wa tatu Wa Utangazaji (Digital Cable TV Broadcasting) maarufu maeneo mengi nchini pia ni wa Malipo Na Channel local kuonekana pia kuna utaratibu wake na haihusiki Na mabadiliko ya kuhamia dijitali Na matakwa ya kuwa local channel zote. Huu ni utaratibu kama ilivyo katika mfumo Wa leseni ZA Utangazaji. Ni kama kuhoji kwa nini mwenye leseni D ya udereva haruhusiwi kuendesha bus la abiria.
Tafadhali pitia katika website yetu www.tcra.go.tz upate taarifa zaidi kuhusu leseni Na maelekezo yake. Aidha angalia ukurasa wetu wa FB www.facebook.com/TCRA1 Kwa maelezo zaidi.
Ni vizuri kuielewa sekta, mfumo Wa leseni, masharti pamoja Na kanuni zinavyoiongoza sekta ili kutokuchanganya hii mifumo. Aidha kuhusu TCRA kama unavyohisi iko, tunaheshimu mawazo yako na Asante kwa ushirikiano Na mawazo yako.

samehe tu,kwani wengine humu ni Un-great thinker!
Mfumo na Leseni ZA Mawasiliano ziko nyingi Kwa mujibu Wa sheria, mtu yeyote anayehitaji leseni hupatiwa leseni kwa mujibu wa mahitaji yake. leseni iliyotolewa ni ya Mawasiliano ya simu ya kuunganisha toka Tanzania (Loliondo Wakati Kiongozi huyo Mwana Wa Mfalme anapokuwa nchini). Leseni hii hutolewa kwa wengine kurahisisha mawasiliano maeneo ambayo miundombinu haitoi huduma zainazokusudiwa.
TCRA inachukua taarifa hizi Kwa uzito kwani tumepewa dhamana ya kusimamia hii sekta kwa niaba ya Watanzania wote. Uhalifu Na ukiukwaji Wa Sheria katika sekta hii ni jambo tunalolifuatilia Kwa karibu. Bahati mbaya Mamlaka haina ofisi kila sehemu nchini. Tunategemea kupata taarifa hizi kutoka Kwa wananchi ili kuweza kubaini matatizo Na kuyafanyia kazi. Ni wajibu Wa kila mtanzania kusimamia haki pamoja na kutoa taarifa Kwa vyombo husika. Mamlaka inapenda kuwakumbusha wote kuwa ili kufanikisha majukumu ya taasisi zenye dhamana yankuwatumikia Watanzania, ni vizuri kutoa ushirikiano Na kutoa taarifa ili kutoa huduma zinazotegemewa Kwa ufanisi. Wote tunawajibika, Na tunawasihi, tuache kunungunika, chukua hatua, toa taarifa Na lalamika wazi kama hapa Jamii Forum, tunafuatilia kila kinachoandikwa na kufanya utafiti ili kujiridhisha Na kutambua tatizo lipo wapi Kwa msaada wenu.
Tunawshukuru tena Kwa ushirikiano. Wakati mwingine tunaomba mtuletee taarifa kupitia malalamiko@tcra.go.tz au complaints@tcra.go.tz.