Mwanzo wa meditation

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,463
2,000
JINSI YA KUFANYA MEDITATION

Meditation Ya Pumzi:
Screen-Shot-2014-10-02-at-11.27.36-AM.png

MEDITATION:

Ni ile hali wakati mawazo yanapokuwa yameyeyushwa na kufikia mahali ambapo hakuna fikra yenye kuingia tena.
¡¤ Wengine wanaielezea tahajudi kwamba, ni sala za usiku wa manane.

FAIDA ZA MEDITATION:

1. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.
2. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji wa chakula mwilini.
3. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.
4. Husaidia kuleta furaha ya nafsi.
5. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya machale pamoja na nguvu zako za ziada.
6. Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).
7.meditation pia inaweza kutumika kuomba kitu unachohitaji,kama vile kazi au mahitaji mbalimbali,
8: Sala ni pale unapoongea na mungu lakini meditation ni pale unapomsikiliza mungu unaemuamini
9: Meditation Hukufanya ujielewe Zaidi,Uwe zaidi Uwe Zaidi ya wewe ulivyo
10: Kama unaswali halijibiki jibu lake utalipata kweny meditation

Hatua:
Kinachotakiwa wakati unajiandaa
Kufanya meditation ni kama ifuatavyo:

1. Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na makelele. Kaa kwenye kiti au chini, au lala kitandani. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.
burmesefront.jpg

images (5).jpg

images (1).jpg

2. Sahau matatizo yako yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote.
3. Ni muhimu sana kujali hisia zako wakati unafanya meditation.
4. Pumua kwa kuingiza pumzi ya kutosha mapafuni, halafu toa pumzi yote na kufanya kifua kiwe kama kitupu. Weka mawazo yako yote kwenye pumzi zako
breathing-meditation-image.jpg

Hizo Ndio hatua za kwanza kabisa za kufanya meditation ya pumzi

5:utakapo endelea kuweka fikra zako kwenye pumzi yako utaona kitu kama rangi rangi zinaanza kutokea kwenye eneo la katikati ya nyusi zako mbili za macho yaani pale ulipofumba macho kwa ndani utaona kama rangi rangi zinaanza kujiform usizitilie sana maanani rangi hizo ziache zije zenyewe
images (1).jpg

6: rangi hizo zitaform vitu kama picha wakati huo eneo lako la kati ya nyusi litaanza kuwa awaken yaani kuamka huku hilo eneo litaamka kwa staili moja kati ya mbili
Kuwasha mwanga mweupe eneo hilo au kutetemeka kama utosi wa mtoto mdogo
7583328_f520.jpg

7: hizo picha zitakazo kuwa zinajiform ukiendelea kuziangalia utaona ni matendo na matukio mengi uliokua ukiyafanya mwenyewe katika maisha yako sasa hapo kuna mawili ukiweza kuwa deep na hayo utakumbuka hadi utoto wako ulivyokuwa lakini ukiyapotezea utaendelea na kuweka fahamu zako kwenye pumzi itakupeleka hatua ya pili ya kuona spirits au viumbe visivyoonekana kama malaika na majini ulionao mwenyewe hawa wanaweza kukuskiliza kwa chochote utakacho waomba

8: ukiendelea kuwatizama basi utafanya mawasiliano nao ila ukiweka maanani kwenye pumzi utahama hatua nyingine ambayo ni deep zaidi na ndio zawadi ya meditation utaona kitu kama nuru inapitia katikati ya utosi wako na kujaa mwilini mwako kadri inavyojaa ndio unavyozidi kupata nguvu mwilini waweza kuishia hapo au ukitaka makubwa zaidi endelea na pumzi

9: utakavyoendelea na pumzi utaona ile power imekujaa kisha utaanza kuona kama sehemu unaanza kwenda deep zaidi ndani zaidi hapa ndio utaanza kuhisi uwepo wa mungu wa imani yako,

Kama ni muislam utaanza kuskia Qur-an inasomwa au utaanza kuona kitu kinachokupa imani zaidi kama mskiti wa makka maandishi ya Qur-an, Sauti za mawaidha n.k wengine waliojaaliwa huiona Baitil Maamur (Mskiti wa mbinguni) kwa vile atakavyooneshwa na mungu wake na itakusaidia kuweka mizizi ya imani katika dini yako,

kama ni mkristo hapa huhisi uwepo wa mungu wa imani yako na nguvu ya yesu au jesus na pia mambo mengine kama maneno ya biblia n.k wengine huona hata roho takatifu inawashukia n.k,

kama ni mpagani na dini zingine na huna imani basi atakae jitokeza ni huyo huyo unaemuamini n.k n.k n.k,

Hivyo hapo unaweza kupata power na mafanikio yoyote unayotaka within a short time kwa imani yako na Meditation haimuondolei mtu imani yake bali humjuza zaidi kuhusu imani yake

10: Utakapo kuwa umejawa na ile nguvu basi utaona mwili wako mzima umekua sealed na aura yako imefunga na kuwa ngumu yenye nguvu na yenye kuwaka katika imani yako kumbuka one deep inner travel can change your life so you have to practice with hope and love (Safari moja ya ndani zaidi ya mwili wako inaweza kubadili maisha yako hivyo fanya kwa upendo na matumaini uweze kufika malengo) kitu hadi ukipende ndio utakifahamu..

hapo utakuwa umecomplete meditation ya pumzi kumbuka sio kwamba utafanya siku moja na kufikia yote haya kila siku utakua ukipiga hatua
Naishia Hapo Ingawa Nitaendelea Kuupdate huu uzi....AINA ZINGINE ZA MEDITATION:

MEDITATE YA UDI:
High-Quality-Lotus-Wooden-font-b-Incense-b-font-Burners-Sandalwood-Buddha-font-b-Incense-b.jpg

Fuata Hatua Zifuatazo Kufanya Meditation Itakayo Fungua Jicho La Tatu & Psychic Power Zako Kwa Muendelezo...

HATUA:
1: Jiande Siku Au Saa Ambayo Baada Ya Hapo Utalala Kupumzisha Mwili...

2: Puliza Au Washa Udi Au Marash Yoyote Unayoyapenda Au Usitumie Chochote Kama Harufu Iliyopo Inakuridhisha

3: Vaa Mavazi Yasiyobana Wala Kukubughudhi Mwili, Na Hata Kama Unapete Cheni Heleni, Saa,mkanda au Chochote Chenye Kubana Kama Umesuka Subiri Siku Ukifumua Hii Husaidia Kuacha Mwili Wako Huru Na Uelewa..

4: Kaa Kwa Mtindo Miguu Wa X, Au Kaa Kwenye Kiti, Au Kaa Mtindo Wa Baadhi Ya Watu Kwa Kuikalia Miguu Juu Yaani Kama Vile Umepiga Magoti Kwa Kukalia.. Chagua Moja Kati Ya Hii Mitindo Utakao Ona Umekaa Hakuna Maumivu Sehemu Yoyote Ya Mwili..

5: hakikisha Mgongo Umenyooka Ili Kuzihesabu Chakra Zote Zimekaa Sawa.. Mgongo Ukiwa Umenyooka Chakra Zote Waweza Kuzihesabu.. Ndio Maana Tunasema Katika Ufunguzi Wa Third Eye Ndipo Unaweza Kucontrol Pia Chakra Zote...

6: Angalia Mbele Kwa Kufocus Vuta Pumzi Ndefu Mara 6 Yani Tatu Nje Tatu Ndani... Hakikisha Unapovuta Ndani Kifua Kinajaa Bila Kubakisha Sehemu na Unapotoa Toa Yote.... inapofika Ya Sita Nje Fumba Macho Taratibu..

7: Anza Kufuta Pumzi Za Kawaida Ila Zenye Kueleweka Na Anza Kuhesabu Kutoka 100,99,98-1... Ukivuta 100, ukitoa 99,vuta98, toa 97... Hakikisha Hauirudii Mara Mbili Namba Ukikosea Hata Kama Bado 4 Umalize Anza Tena 100 usifikirie kingine zaidi ya pumzi na namba...
articles-20131210-meditation-techniques-at-ymaa-retreat-center-part-1-4.jpg

8: Wakati Umeanza Kuhesabu Iangalie Sehemu Ya Third Eye Chakra, Humo Umefumba Macho Angalia Kwa Kupandisha Macho Yako Eneo La Katikati Ya Nyusi Zako Jitahidi Usikunje Ndita..

9: Pindi Utakapofika 3,2,1 eneo hilo la katikati ya nyusi ulioangalia utahisi kama kihali flani hivi wengine huhisi kama kiwembe kimemchana au hali flani nzuri huwa haielezeki au nuru ya mwanga kama niliotaja juu...
Hapo utaona kama vile macho yako yamefumbukia kwa ndani...

10: utaona kama video game ya matukio uliowahi kuyafanya inacheza mbele yako usinogewe sana, Iache Icheze Ufunguo Au Remote Yako Ni Hewa Unayoivuta Endelea Kuvuta Huku Ukiangalia Matukio Yako Ya Humo Ndani...

10: hizo ndio takataka zilizokujalia kwenye ubongo.. Zitaanga kupotea Moja Moja Na Utafikia Sehemu Utaona Kama Nyota Zinatoka Chini Zina Panda Juu Hizo Ndio Tunaita Spirits Za Crown Chakra Stage Hiyo Unaweza Kuomba Unachotaka Na Kikaja Kabla Ya Wiki Kuisha.. Ikitoka Hiyo Stage Utaona Zile Nyota Zimeshapanda Zote.. Hakuna Kingine Sasa Hapo Ndio Utaanza Kuhisi Kama Mvua Inapenya Katikati Ya Utosi Na Kusambaa Mwili Mzima.. Unataka Kujua Hicho Ni Nini?? ndiyo Charge Ya Pyschic Power Zako Inaanza Kuingia Ikadirie Isiingie Nyingi Kupita Kiasi Zikaja Kuwa Kero Baada Ya Kutoka Kwenye Meditation... Hakikisha Hii Ni Mara Yako Ya Kwanza Usifanye Zaidi Ya Dk 15-20.. Utakavyozidi Kufanya Siku Zingine Muda Wako Wenyewe Utaanza Kijiongeza Baadae Unaeza Hata Kufanya Saa Zima..
Ukitaka Kutoka Vuta Pumzi Ndefu Kama Ulivyoingia Mara 6 na gonga kidole chako kuashiria unatoka fumbua macho yako taratibu na uanze kuelewa eneo uliopo usikurupuke tulia macho yatambue kwamba umefumbua.. Utajisikia furaha sana, na utajiskia mwili unanguvu na mwepesi zikumbuke ndoto ulizoota siku hiyo zilete hapa tutakusaidia...

ZOEZI LlKIENDA TOFAUTI:
Fanya haya:

Ukiwa Katikati Ya Meditation ukahisi Eneo Unaloliangalia Linachemka Gonga Kidole utoke Utafanya Muda Mwingine..
Hii huwatokea sana wenye msongo wa mawazo.. Taratibu tutafika...
Ukihisi vibration kwenye eneo la third eye usiogope ni system inaanza kufunction... Ukiwa unaangalia matukio yako pale pale ukahisi eneo la third eye linachemka gonga kidole na utoke.... Hvyo unapofikia sehemu ukahisi utajua tu paji la uso linachemka maana utaanza kuhisi jasho pia gonga kidole na utoke...
Hivyo Njia Ya Kukwepa Unexpected Things Unagonga Kidole Tu Unatoka... Kumbuka Usiunde Kitu Maana Huo Ni Ubongo Wako Sio Mtu Wala Kiumbe Utakacho Unda utakupeleka Huko huko usiwaze kitu kuwa muelewa maana wengine huanza imagination hapa utakuwa hufanyi meditation...
Hakikisha hakuna makelele ulipokaa...

Meditation ya namba:
ambayo nayo taianzishia uzi wake,.
images.jpg

Hapa, unatakiwa kuhesabu namba kinyume nyume huku ukiwa umefumba macho. Unaweza ukaanzia 100, 99, 98, 97, 96, ¡-mpaka 1, au unaweza kuanzia 200, 198, 196, 194, 192, mpaka 2. hakikisha wakati unahesabu namba hizi hukosei, na ikitokea ukakosea namba yoyote hata
kama umekaribia kumaliza, itakulazimu kuanza upya. Meditation hii ni nzuri sana kwa kurejesha kumbukumbu, ingawa pia ina faida nyingine.

Hizo ni mbili tu za aina za meditation ambazo zipo nyingi kama 25 zote tazileta kwa awamu kwa wale wanaotaka kumaster meditation....

kwa haya na mengineyo tembelea Rakims Spiritual kujifunza zaidi

Na kama una swali la binafsi na upo nje ya forum basi tumia email hii:

Mawasiliano:

Rakimsspiritual@gmail.com

Rakims
 

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,463
2,000
Naomba nijulishe juu ya swali hili.
Ukija kwenye swala mkuu itakubidi usali rakaa mbili mbili za tahajudi au istikhara au kiyamul layl zote zina utaratibu wake lakini kwa ushauri ushauri wangu ni heri usali kiyamu mbilimbili zikifika mara mbili unavuta nyiradi kisha unaendelea, hii ni bora zaidi kuliko meditation.

Rakims
 

msafiri.razaro

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,102
2,000
Ukija kwenye swala mkuu itakubidi usali rakaa mbili mbili za tahajudi au istikhara au kiyamul layl zote zina utaratibu wake lakini kwa ushauri ushauri wangu ni heri usali kiyamu mbilimbili zikifika mara mbili unavuta nyiradi kisha unaendelea, hii ni bora zaidi kuliko meditation.

Rakims
 

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,463
2,000
Nimeona chenga kweli, meditation na Sara wapi na wapi, tunameditate kukwepa fikra, Sara ni fikra nuizi, mbona haviendi sawa?
Ni kweli mkuu haviendani, lakini watu huona meditation ni mlango wa kumsikiliza aliyewaumba sasa waislamu hufanya hivyo kutaka muongozo wa mola Wetu mkuu,

Rakims
 

mahatmaxlla

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
728
1,000
Wakati mwingine inaweza tokea hata ukiwa umetoka usingizini lakini unakuwa bado hujashtuka kwa bed,unajikuta umehama kimawazo unakuwa kama unaota lakini kama hauko usingizini vile,unaenda katika sehemu ambayo hata hujawahi fika kimsingi,wala kupaona yaani ni sehemu kama taswira ya kuzimu vile au ulimwengu mwingine.hii kitu huwa inanitokea kwa vipindi sana
Au hii huwa ni nini!
 

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
3,463
2,000
Wakati mwingine inaweza tokea hata ukiwa umetoka usingizini lakini unakuwa bado hujashtuka kwa bed,unajikuta umehama kimawazo unakuwa kama unaota lakini kama hauko usingizini vile,unaenda katika sehemu ambayo hata hujawahi fika kimsingi,wala kupaona yaani ni sehemu kama taswira ya kuzimu vile au ulimwengu mwingine.hii kitu huwa inanitokea kwa vipindi sana
Au hii huwa ni nini!
Astral Projection/mental projection rejea kwenye thread yangu hii

https://www.jamiiforums.com/threads/jinsi-ya-kutoka-nje-ya-mwili-astral-projection.801793/
Rakims
 
Top Bottom