Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Hiki kitu kilichofanywa na mangula kwa watu wa mwanza ilikuwa ni dharau na kejeli kubwa kwa watu wa Mwanza.This was typical sarcasim na alipata anachostahili
 
Hivi Mayor wa Ilemela hakuwepo atumie vifungu kuwazuia wananchi wasimzomee Mangula?

Alikuwepo kaka,alipanda jukwaani na kusema 2015 atagombea kupitia maccm. Dialo aliharibu aliposema tukigundua mtumishi wa umma anashabikia upinzani tunamfukuza kazi.Pia aliwaambia walimu wasiwafundishe wanafunzi mabaya ya ccm. Watu wakaguma mmmh! kumbe ccm wanatambua kuna mabaya kwanini wasiyalegebishe bac.
 
Mkuu Umenena vilivyo lakini wahusika wameweka Pamba masikioni au Kama sivyo basi tatizo ni wenye akili kuongozwa na wajinga.

Mfano: juzi Kati nimekuta watoto wadogo wanakimbizwa na mwenyekiti wa mtaa kisa wamedungua bendera ya ccm kwenye Nyumba ya mwenyekiti na kuamua kuigombania kwa kuichana Chana na kila mtoto kuondoka na kipande chake wakionyesha hasira walikuwa wanakimbizwa Huku waki ichana bendera ya ccm lilikuwa kundi la watoto Kama 20 Mwenye umri mdogo ni Kama miaka 7 na mkubwa ni Kama miaka 13 nikamuuliza mtoto mmoja kwanini mnafanya hivi akasema tumewachoka Hawa apa unapotuona broo tumerudishwa shule kisa hatujalipa ada baba anakwepa kwenda shule anasema yote Hii ni ccm ndio maana tukaonesha hasira zetu na Huu ni mfano tutazunguka mtaa mzima tuchane zote. Nikamuuliza kwa kebehi kwani ccm inahusika vipi na mzazi wako kukosa ada huoni ni kosa la baba yako kutolipa? Akasema Hakuna bro wenyewe wanajilipa na kujipandisha vyeo Huku watoto wametusahau, Embu ona bro, walim wameturudisha wiki Hii mzima hatujasoma wengine ndio kwanza tumeingia darasa la7 wengine apa walim wanatuambia lazima tufaulu tusiwatie Aibu shule Yao alafu wanaturudisha nyumbani tutafauluje? Kwani wameshindwa kutuvumilia? Na kwa nini watuchape na kuturudisha kwa nini wasimchape baba aliye shindwa kulipa? Nikamwambia na baba anasemaje kuhusu Hilo akasema baba yeye Hana Hela najua juzi katoka kumlipia dada Ada ya secondary tena nusu na analalamika Hana ila baba mi namjua angekuwa nayo angelipa.
Nikatafuta swali la mwisho nikamwambia sasa ukichana bendera ya ccm ada ndio italipwa? Akasema we bro ni ccm? Maana nyie watu wa ccm Mko wengi sana hata Mwalimu minja ni ccm Yule lazima ndio maana akaturusha tutawakomesha Hawa ccm Mwaka Huu, nikapata swali jipya nikamuuliza utawakomeshaje ccm wakati nyie ata kura hampigi nyie bado watoto? Akasema we bro hujajua wewe sisi apa tukikuta bendera tunachana na pakiwa na Uchaguzi wakiweka matangazo tunachana yote. Na kwa mfano tukiwa na mechi au shuleni tunaambiana sababu tuna kaa mtaa tofauti hata mikoa pia. Akaniuliza au wewe unaona raha kuchapwa na muanzi bro kisa Huna Ada kwani mi nafanya kazi? Nikamwambia kweli yeye Hana kosa ila ata ccm haina kosa wakanizomea na kutokomea wakisema agh ndio nyie nyie we kula kona nikala kona kweli Huku najiuliza wale vijana wa Arusha, musoma na kwingineko Wanasema ni wavuta bangi wa cdm na Hawa watoto je?????? JIULIZE KWANZA kisha chukua hatua



Si jambo la kufurahia sana. Tunajenga kizazi cha watu wasioridhika na uendeshaji wa serikali. Watoto wetu wanajifunza kutoiheshimu na kuithamni serikali bila kupata ufumbuzi wa haraka. Watoto wanaona kwamba serikali ni chombo cha maadui wao. Kwa hakika itakuwa kazi kubwa kuwawajibiosha huko tuendako.
CCM jifunzeni kwa reaction za watu. Huu si upepo tu kama msemavyo, bali ni hali halisi "mnachukiwa sana" kibaya zaidi mnatuharibia sana kizazi tutakachokitawala sisi watu makini.
 
Ni dhambi na kufuru kusema ccm haikuleta maendeleo katika miaka 50 iliyopita:target:

So kweli kabisa kwani ccm imeleta mafanikio ya propaganda tuu na sio kingine. Mangula anasema ccm imeleta Maendeleo mwanza kwani ccm ikishika nchi mwanza kulikuwa na gorofa moja la bugando eti sasa magorofa kibao si Aibu Hii? Yani shirima na Mwita wakijenga gorofa ndio ccm imejenga? Hospital zote za mission, barabara zinajengwa na wafadhili Pamoja na kodi je mapato ya raslimali Kama utalii, bandari, gas, madini etc vinakwenda wapi? Ni Maendeleo yapi hayo ya mkopo na Deni kuja kukitesa Kizazi chetu? Ungekuwa karibu yangu ningekulamba kibao au nikutukane nini ndio maana gambaz wewe
 
Niliona Nnauye anawaonyesha wazomeaji kidole kama ishara ya kufirwa. Nimemwona kama kiongozi asiye na Busara,akiri na hekima,naomba apewe ushauri nasaha namna ya kuvumilia wananchi pale wapomkataa.
Punguza ukali wa maneno na matusi, JF ni jukwaa la wastaarabu na siyo kijiwe cha wavutaji wa ile sigara kubwa...........!
 
Kumzomea haitoshi ilitakiwa wamtandike na viboko sijui kwanini hawa magamba hawakati tamaa wananchi hawawataki tena sijui mnawang'ang'ania nini? it's too late mmeshachemka pelekeni ufisadi wenu kule hatutaki hata kuwaona
 
Hiki ni kituko cha kushangaza kama siyo kusikitisha pale wananchi wanaposhabikiwa kwa kuzomea zomea msafara wa watu au wanasiasa.

Watanzania tumeanza kuonyesha dalili ya kuanza kufilisika kisiasa kwa kuanza kushadadia zomea zomea kama ndiyo njia mbadala ya kujenga hoja wakati hii ni dalili ya ukosefu wa ustaarabu kisiasa na mwanzo wa uvunjifu wa amani katika jamii.

Lazima tuendeshe siasa zenye msingi wa kukubali kutokubaliana katika hoja na siyo hoja za nguvu katika misingi ya zomea zomea (Hooliganism)

-We can't entertain let alone practise the idea of being flag-waving and intolerant.

-Tufike sehemu na kusema, this is not right.
 
Punguza ukali wa maneno na matusi, JF ni jukwaa la wastaarabu na siyo kijiwe cha wavutaji wa ile sigara kubwa...........!

Ulitaka asemeje?unajua alikuwa na mood gani?unafahamu ni kiasi gani CCM imemchosha?
 
Hiki ni kituko cha kushangaza kama siyo kusikitisha pale wananchi wanaposhabikiwa kwa kuzomea zomea msafara wa watu au wanasiasa.

Watanzania tumeanza kuonyesha dalili ya kuanza kufilisika kisiasa kwa kuanza kushadadia zomea zomea kama ndiyo njia mbadala ya kujenga hoja wakati hii ni dalili ya ukosefu wa ustaarabu kisiasa na mwanzo wa uvunjifu wa amani katika jamii.

Lazima tuendeshe siasa zenye msingi wa kukubali kutokubaliana katika hoja na siyo hoja za nguvu katika misingi ya zomea zomea (Hooliganism)

-We can't entertain let alone practise the idea of being flag-waving and intolerant.

-Tufike sehemu na kusema, this is not right.

Mkuu hii ni sawa kwa wanyonge wanaotetea rasilimali za nchi zao zisiporwe.

Hiyo ndiyo dawa ya watu kama kina Nape wanaodhani sera ni kutukana Chadema matusi.

Keep it up People from Mwanza.God bless you!
 
SIASA


mangula.jpg

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Philip Mangula

Na Frederick Katulanda, Mwanza

Posted Jumatatu,Januari21 2013 saa 8:57 AM

KWA UFUPI
Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo ambao hawakuwa wamevalia sare za CCM, walijipanga kando ya barabara ya Posta na wakati viongozi hao wakipita waliwazomea huku wakionyesha ishara ya vidole viwili.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Philip Mangula jana alionja machungu aliyowahi kupata Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya msafara wake kuzomewa jijini Mwanza.

Msafara huo wa Mangula ulizomewa jana muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake katika uwanja wa michezo Nyamagana.

Katika msafara huo mbali na Mangula pia walikuwapo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Grayson Lwenge na Katibu Itikati na Uenezi, Nape Nnauye.


Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo ambao hawakuwa wamevalia sare za CCM, walijipanga kando ya barabara ya Posta na wakati viongozi hao wakipita waliwazomea huku wakionyesha ishara ya vidole viwili.

Kutokana na hali hiyo, vijana wa CCM maarufu kama Green Guard walianza kuvamia wazomeaji hao na kuanza kutembeza kipigo ambapo vijana wawili ambao majina yao hayakufahamika walijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.

Septemba 17, mwaka jana, ndani ya uwanja wa Sahara, Pinda alizomewa na wananchi wakati akihitimisha ziara yake jijini Mwanza, kutokana na kero nyingi zinazowakabili wakazi wa jiji hilo, huku kiongozi huyo akiwataka waachane na ushabiki wa kisiasa.

Awali, akihutubia mkutano huo, Mangula alisema pamoja na kwamba wapinzani wamekuwa wakibeza mafanikio ya ya CCM lakini ukweli utabaki palepale kwamba katika kipindi cha miaka 50 ya utawala huo nchi imepiga hatua za maendeleo.

Mangula alitoa mfano kuwa wakati wa miaka ya nyuma kulikuwa na ghorofa moja la hospitali ya Bugando na sasa yapo ‘mabugando' mengi.

Mbali na kuelezea mafanikio hayo pia aliwataka wanachama wa CCM kutumia vikao katika mashina kuzungumza na wanachama kubainisha matatizo yanayowakabili badala ya kuzungumza nje ya vikao, jambo ambalo limekuwa likikigawa chama.

Hata hivyo, Mangula ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu katika mkutano huo, tofauti na matarajio ya wengi hakuzungumza zaidi ya dakika tano.

Wakati akiondoka baadhi ya wananchi hao walisikika walilalamika kuwa walitarajia kusikia mengi lakini hakuna walichosikia.


Kutokana na hali hiyo wananchi hao waliamua kukaa kando ya barabara ya Posta, nje ya uwanja huo na kuanza kuwazomea viongozi waliokuwa wakipita.

 
Ujue CCM inabidi wabadilike wasinzani watanzania bado ni wapumbavu au watu ambao ni raisi kudanganyika kama hapo zamani watanzania wa leo ni watu tofauti kabisa japo wapumbavu bado wapo ila wajinga wamepungua sana kwa hiyo CCM iwe macho ibadilike hisi taarifa za ufisadi na wizi wa mali za umma zinazotolewa na vyombo vya habari si taarifa njema kwao kama leo hii hata wanajeshi wanajihusisha na ujangili. Makontena ya pembe za ndovu yanapita bandarini kimya kimya alafu yanaenda kukamatiwa nje. Pesa zimefichwa uswisi na serekali haichukui hatua yoyote yakufuatilia pesa hizi imekaa kimya ni aibu kubwa kwa serekali ya CCM kwa hiyo hata ikichukiwa isishangae watu hawafurahishwi na haya yanayotekea. Hata kama hawausiki wachue hatua basi ya kuwawajibisha wanaohusika kwani hata baba mwanao aikiwa mkosaji usipomwazibu kila siku anapotenda kosa atakudharau ataona huyu ni baba gani ambaye hana msimamo na hawezi kunifanya lolote. Serekali ya CCM chukueni hatua acheni kubembelezana itawakosti 2015
 
Ulitaka asemeje?unajua alikuwa na mood gani?unafahamu ni kiasi gani CCM imemchosha?
Hata kama alikuwa na mood mbaya kiasi gani kuhusiana na hawa magamba wanavyomkera!! Lakini kwa kiasi kikubwa wachangiaji humu JF, tunatakiwa tuwe na uvumulivu mkubwa, na hawa magamba tunapaswa tuwajibu kwa hoja na siyo kuwatukana, na mwisho wa yote, mwaka 2015, tuwang'oe madarakani, kwa kutumia sanduku la kura!!
 
[h=2][/h]JUMATATU, JANUARI 21, 2013 04:49 NA JOHN MADUHU, MWANZA

*Mkutano wa CCM wavurugika, watu wajeruhiwa, polisi waingilia kati
*Mangula, Dk. Mwakyembe waonja joto, warushiwa chupa za maji

VURUGU kubwa zimezuka na kusababisha baadhi ya watu kujeruhiwa vibaya, baada ya kutokea mapambano baina ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Vurugu hizo zilisabaishwa kufungwa kwa muda kwa baadhi ya barabara, baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philiph Mangula na Mawaziri Dk. Harrison Mwakyembe na Jerryson Lwenge.

Wafuasi wa Chadema baada ya kuona hali ya usalama imedhibitiwa ndani ya Uwanja wa Nyamagana kulikokuwa kukifanyika mkutano wa hadhara, waliamua kuwasubiri viongozi wa CCM pamoja na wafuasi wao katika makutano ya Barabara za Kenyatta na Posta katika mzunguko wa magari na walianza kuwazomea kwa kuwaita mafisadi, huku wakiwatupia chupa za maji pamoja na mawe.

Kutokana na vurugu hizo, vijana wa CCM walianza kuwatimua wafuasi hao wa Chadema kwa kupambana nao hali iliyozusha vurugu kubwa na watu kadhaa kujeruhiwa vibaya kutokana na kupigwa mawe pamoja na fimbo.

Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi liliwatawanya wafuasi wa vyama hivyo na kuwachukua majeruhi zaidi ya 10 na kuondoka nao.

Kutawanywa kwa vijana hao kuliwafanya wanachama wa CCM waliokwama katika Uwanja wa Nyamagana kuweza kutoka kwa kutumia mabasi maalumu waliyokuwa wameandaliwa kuwarejesha makwao.

Akihutubia mkutano huo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe, aliapa kuendelea kuwasafisha viongozi wasio waaminifu walioko katika taasisi zilizo chini ya wizara yake na kusema ambao hawataki kubadilika wanapaswa wajiondoe wao wenyewe.

“Nitawafyeka wote ambao wamekuwa wakishindwa kubadilika na kuchuma mali za wananchi bila huruma, wapo ambao najua watanuna na wamekuwa wakitishia kuhamia vyama vya upinzani, waende tu kwani hawatufai.

“Kuna baadhi waliamua kwa makusudi kuchomoa baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kumsaidia mgeni ainyonye nchi hii, ufisadi umekithiri na nitaendelea kupambana nao kwa kuwa tayari nimeshachukua kwa kufanya mabadiliko katika baadhi ya maeneo muhimu yaliyo chini ya wizara,” alisema Dk. Mwakyembe.

Kwa upande wake, Meya wa Ilemela (Chadema), Henry Matata, alisema yuko tayari kuisambaratisha Chadema na tayari ameshaanza kwa kuwatimua madiwani wa chama hicho kwa kutumia rungu lake la Umeya.

“Mimi ni diwani wa Mahakama nimechaguliwa na madiwani wa CCM, hivyo CCM ni nyumbani kwangu na niko tayari kuwasaidia waweze kuchukua nafasi ya udiwani katika kata ambazo niliwatimua madiwani wa Chadema kutokana na kushindwa kuhudhuria katika vikao kwa mujibu wa sheria na kanuni,” alisema Matata.

 
Kweli Tz kuna ubakaji wa demokrasia, CCM wanafurahi tu jinsi huyo Matata na vituko vyake, kisa anawasaidia kuibomoa CHADEMA! Km kweli kawatimua madiwana wa CHADEMA na CCM wameridhia maana wao si ndio wanajidai ni mahakama; basi waitishe UCHAGUZI mdogo ktk kata husika tuone kama kweli CHADEMA imebomoka Mwanza ama la.

Ninavyowafahamu wanaMWANZA hawadanganyiki tena na CCM. Kama CCM wanabisha waitishe uchaguzi huru waone na wakija kosea ku_UPDATE DAFTARI la wapiga kura wataaibika mbaya.
 
Back
Top Bottom