Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

Mwanza: Mangula azomewa kwa aibu

....
Awali Mangula alihutubia kwa dakika 5 tu kitu kilichowashangaza wengi n......

Man alijua kilicho mkuta Kar wakati unahitimishwa mchakato wa uchaguzi ndani ya 'Tawala' pale Dodoma. Kar aliongea mengi sana mpaka akaanza kuwaita watu wana vichwa vya samaki. Kwa hayo hizo dakika tano ni njia ya kukwepa mtego ule.
 
Ni dhambi na kufuru kusema ccm haikuleta maendeleo katika miaka 50 iliyopita:target:

wananchi hatuyaoni tunashindia pipi chakula tunakiona kwenye video halafu mafsad hamjui hata bei ya unga,mashetani wakubwa nyie ccm.
 
Viongozi wetu wanatakiwa kujifunza zaidi namna ya kuwasilisha hoja zao kwa watanzania wa leo la sivyo mambo haya ya zomeazomea yataendelea kuwaandama!
 
Kamwe giza haija wahi shinda nuru. Leo tena RFA toka magazetini hawaja isoma habari hii. Magazeti ya Mwananchi na Tanzania Daima haya kusomwa yote kabisa ili kuwafurahisha wakubwa wezi wa rasilimali zetu. Sasa hivi ccm watakimbilia wapi? Kusini kimewaka, kaskazini moto, kanda ya ziwa Mangula anayo majibu, Mbeya pachungu. Wananchi wamechoka na Propaganda, wanataka kuyaona Maisha bora .
 
Mh! SISIEM nao hawasomi harama za nyakati?!

Ingekuwa mimi nipo SISIEM nisinge jitokeza mbele za watu na kuzungumzia SISIEM kwamba ni chama kizuri.

Mh! ajabu kumbe hawa jamaa wanaroho ngumu!. Na wanameza tu hata kama ni sumu
 
Senior MemberArray


Join Date : 3rd July 2012
Posts : 219
Rep Power : 372
Likes Received24
Likes Given22


[h=2]
icon1.png
Npe aanza kufunga virago[/h]
nape nauye rudi ccj mapema maana unaona kasi ya mheshimiwa mtarajiwa edward lowassa anavyong'ara.wahenga walisema usitukane wakunga na uzazi ungalipo,ulimkashifu sana lowasa ukamuuta fisadi,ukamuta gamba ndani ya chama ukampa siku 90. Sasa nape kikwete anaondoka 2015 na lowasa anongoza ngome ya ccm kwa ukweli weka hii taarifa vizuri utasahaulika ndani ya ccm na utajutia domo kaya lako,if u don't believe call me na nikupe data zako zote.pole sana maana chadema hawatakuchukua maana wewe na nchemba ni member wa masalia labda cuf tu.lowasa ni kiongozi jasiri aakayeweza kufukuza wapuuzi wote ndani ya ccm viva lowasa. ccm mnajua bila ya lowassa na kundi lake hamna pesa za kuendesha chama.[COLOR=#49535A !important] +447534130796


[/COLOR]

Wewe naye na nape wakati uko uingereza ujui ya hapa tz tena ndani ya ccm usimtukane nape kwa raarifa yako lowasa wala awiki kama unavyo danganywa na wapambe wake uliza vizuri uambiwe
 
Nili hisis haya yatatokea tu. Unajuwa watu wameshachoka kusikia jina la chama hiki. labda wangetafuta chama kingine wakaungana likatoka jina lingine la chama labda watu wangepata apetite? Jina hili limefika turning point!



Makamu Mkiti wa CCM Philip Mangula alionja joto ya jiwe mkoani Mwanza pale msafara wake ulipozomewa vibaya njia nzima tokea alipotoka uwanja wa nyamagana kwenye mkutano wa hadhara.

Aibu hiyo ya zomeazomea iliwakumba pia Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye.

Wananchi walijipanga njia nzima msafara huo ulipopita huku wakionyesha ishara ya vidole viwili na zomeazomea ikishika kasi.

Awali Mangula alihutubia kwa dakika 5 tu kitu kilichowashangaza wengi na swala la msingi alilosema ni kwamba CCM imeleta maendeleo katika kipindi cha miaka 50 kwani zamani Mwanza ilikuwa na ghorofa moja tu la Bugando lakini sasa kuna 'Mabugando' mengi.

Source:Mwananchi Jumatatu.
 
Msafara wa Mangula wazomewa Mwanza

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa Philip Mangula jana alionja machungu aliyowahi kupata Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya msafara wake kuzomewa jijini Mwanza. Msafara huo wa Mangula ulizomewa jana muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wake katika uwanja wa michezo Nyamagana. Katika msafara huo mbali na Mangula pia walikuwapo Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Ujenzi, Grayson Lwenge na Katibu Itikati na Uenezi, Nape Nnauye.

Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, baadhi ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo ambao hawakuwa wamevalia sare za CCM, walijipanga kando ya barabara ya Posta na wakati viongozi hao wakipita waliwazomea huku wakionyesha ishara ya vidole viwili.

Kutokana na hali hiyo, vijana wa CCM maarufu kama Green Guard walianza kuvamia wazomeaji hao na kuanza kutembeza kipigo ambapo vijana wawili ambao majina yao hayakufahamika walijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili.

Septemba 17, mwaka jana, ndani ya uwanja wa Sahara, Pinda alizomewa na wananchi wakati akihitimisha ziara yake jijini Mwanza, kutokana na kero nyingi zinazowakabili wakazi wa jiji hilo, huku kiongozi huyo akiwataka waachane na ushabiki wa kisiasa.

Awali, akihutubia mkutano huo, Mangula alisema pamoja na kwamba wapinzani wamekuwa wakibeza mafanikio ya ya CCM lakini ukweli utabaki palepale kwamba katika kipindi cha miaka 50 ya utawala huo nchi imepiga hatua za maendeleo.

Mangula alitoa mfano kuwa wakati wa miaka ya nyuma kulikuwa na ghorofa moja la hospitali ya Bugando na sasa yapo ‘mabugando' mengi. Mbali na kuelezea mafanikio hayo pia aliwataka wanachama wa CCM kutumia vikao katika mashina kuzungumza na wanachama kubainisha matatizo yanayowakabili badala ya kuzungumza nje ya vikao, jambo ambalo limekuwa likikigawa chama.

Hata hivyo, Mangula ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu katika mkutano huo, tofauti na matarajio ya wengi hakuzungumza zaidi ya dakika tano. Wakati akiondoka baadhi ya wananchi hao walisikika walilalamika kuwa walitarajia kusikia mengi lakini hakuna walichosikia.

Kutokana na hali hiyo wananchi hao waliamua kukaa kando ya barabara ya Posta, nje ya uwanja huo na kuanza kuwazomea viongozi waliokuwa wakipita.


chanzo:gazeti la mwananchi
 
hivi ndugu yangu, wewe ujuavyo maendeleo ni nini? Hebu tupe muongozo wa maana ya maendeleo maana inaonekana unafahamu vizuri juu ya hili!

Nadhani wewe ndiyo unajua kuliko wenzako hao walio ona ni kejeli kuambiwa ghorofa lilikua moja la bugando tu na sasa yako mengi!hahahahaha! siamini kama ni Mangula Koangea hivi,Mzee huyu bora angejipumzikia tu kule Njombe. Sasa ana kazi yakutuambia EPA,GREEN DIP,RICHMOND,USWISS,PESA ILIYO ONGEZWA KWENYE BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI KUTOKA MTWARA,WIZI WA WANYAMA,MENO YA TEMBO na machafu mengi tunayo yaona ndani ya chema chetu cha Mapinduzi.
 
Makamu Mkiti wa CCM Philip Mangula alionja joto ya jiwe mkoani Mwanza pale msafara wake ulipozomewa vibaya njia nzima tokea alipotoka uwanja wa nyamagana kwenye mkutano wa hadhara.

Aibu hiyo ya zomeazomea iliwakumba pia Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye.

Wananchi walijipanga njia nzima msafara huo ulipopita huku wakionyesha ishara ya vidole viwili na zomeazomea ikishika kasi.

Awali Mangula alihutubia kwa dakika 5 tu kitu kilichowashangaza wengi na swala la msingi alilosema ni kwamba CCM imeleta maendeleo katika kipindi cha miaka 50 kwani zamani Mwanza ilikuwa na ghorofa moja tu la Bugando lakini sasa kuna 'Mabugando' mengi.

Source:Mwananchi Jumatatu.
NA MAGHOROFA YALIYOKO CAPE TOWN NA YALE YALIYOKO KENYA,UGANDA BURKINA FASO,GHANA NIGERIA,USA,GERMANY yameletwa na CCM?, hivi kuna mjanga wa kuambiwa eti ELIMU, AFYA, MAJENGO, VIWANDA, MASHAMBA ktk nchi vimeletwa na CCM? tunchohitaji si majengo sisi wala magari tunahitaji elimu bora kwa kuwa elimu iko kote ulimwenguni na majengo yetu wenyewe wananchi sio majengo ya ma---------, na wageni na viongozi wa chama cha mapinduzi.
 
mbaya ni kwamba sasa wao wanadhani uwepo wa masalia ni neema ya kupoteza wananchi mwelekeo wa kudai haki hapo wananchi wanaposugua ndipo mimi nadhani tungeenda wote vivyo hivyo mpaka mwisho hawa jamaa hawana tena legitimacy ya kusimama mbele ya umma na nchi inayoyoma hii
 
Ina maana maenedeleo ni Magorofa? Na hayo Magorofa yamejengwa na Serikali? Vilaza wa CCM ni wengi sana, sehemu kuna weza kukawa na Nyumba zilizo ezekwa kwa majani lakini kukwa na maendeleo,

Kama anaona maendeleo ni magorofa huyo ni MBULULA..maendeleo hupimwa kwa mwananchi wa kawaida kabisa..je anaweza kupata mahitaji yake km..afya,elimu malazi na makazi kama mahitaji ya msingi
 
Siyo alikwepa aibu maana vijana wa Mwanza naambiwa walikuwa na hamu nae kweli kwani wanajua kuwa yeye ndiyo alifanikisha ili dili la EPA kuwa yeye ndiyo alikuwa master plan...
Mkuu yegella Nadhani alikuwa hana hoja ndiyo maana alihutubia kwa dakika 5 tu.
 
magula na nape walitakiwa kuonja kichapo maana akili zao ni za kijinga sana wanaenda kudanganya watu wenye akili timamu kama mwanza ikiwa na watu wengi walio nauelewa na kisomo cha kutosha kama mtwara/lindi nako naona wameshaamka hakuna mjinga katika nchi yetu kwa sasa
 
Back
Top Bottom