Mwanza City: The Photo Gallery

Kaka mwanza unakuza iende wapi? Mwanza inachohitaji ni uboreshaji wa mji Kuanzia katikati ya mji.
Dar na mza wanatakiwa watu wapigwe marufuku ujenzi wa nyumba za chini,
Kuna watu wengi tu wanaweza jenga apartments za maghorofa.
Uwepo utaratibu na usimamiwe, sio mitaa yote imejaa maduka sie ndio tunaita mji umechangamka.
Nimeshasoma serikali ya mkoa inatakiwa kujenga shopping centers angalau kila kata, anayetaka kufanya biashara anaenda kufanyia kwenye shopping area sio kila mtaa ujae maduka tu.

Unaiongelea Paris, unajua wakati iko size ya mza ilikuwaje?
Au unafikiri ilikua kwa kuhamisha stendi?
 
Hata mim nakuunga mkono kwenye ujenzi wa apartment...hata hvyo hatuwezi kurundika apartment eneo Moja maybe city center..mji sio makazi tu ..mji kukua sio kuongezeka makazi tu Bali pia uwekezaji mwingine kama maeneo ya viwanda, recreation center, maeneo ya taasisi,na maeneo ya shopping kama ulivyosema ..... serikali inaweza kupiga marufuku ujenzi wa nyumba za chini sawa .lakin bado Kuna watu wangependa kuishi na familia zao kwenye mansion zao utawazuia ?... otherwise kuwe na factor kama uhaba wa ardhi,na idadi kubwa ya watu kama ilivyo miji ya china
 
Mikdde hivi unajua kwamba jiji la Mwanza ni kubwa mnoo mnoo sasa tukitaka tulipanue kabla hata hatujalijaza jiji, baadae utakuja kutwambie jiji lipanuke mpaka lifike huko mwigumbi shinyanga, subiri kwanza hizi wilaya zetu mbili ziwe na hadhi ya jiji kwelikweli, maeneo bado ni makubwa mno ndugu yangu

Ukitoka igombe ukiwa unaelekea kayenze unaeza dhani sio sehemu ya Mwanza Sababu ni mapori kweli kweli,

Kwa hiyo hoja yangu ni kwamba hamna haja ya kufanya expansion ya mji artificially, miji inapanuka yenyewe naturally, kwani stand ni Nini mzee!
 

Noma
 

Nzuri
 
Sasa unadhani huko igombe na Kayenze kutakua vip kama hamna allocation ya huduma na miundombinu...ebu assume Kayenze wakajenga bandari ya kwenda ukerewe patakuwaje .Kwa sababu pale ndio Pako karibu na ukerewe
 
Hamna mji unaokuwa naturally brother.. forget it .hata dar inakuwa artificial...watu wanafata resources, opportunity,na huduma ...
 
Shida idadi kubwa ya watu wa Mwanza ni wapangaji, sasa umwambie mtu apande mti halaf ni mpangaji tu sio permanent resident atakuelewa?
Tatizo kubwa hapo sio upangaji bali ni ubinafsi, mche wa mchongoma au mjakaranda ambayo inastawi vizuri sana mwanza ni shilingi elfu moja na haihitaji maji mengi na kama utaipanda kipindi cha mvua hauta hangaika kumwagilia.

Lakini ukiwaza tu kwamba hapo ulipo umepanga sio kwako kwa maana hiyo unampandia mwenye nyumba ndio tatizo linaanzia hapo. Lakini kiuhalisia mti utakaopanda utanufaisha dunia mzima.
 
Hamna mji unaokuwa naturally brother.. forget it .hata dar inakuwa artificial...watu wanafata resources, opportunity,na huduma ...
Mwanza na Dar zinakuwa naturally ila Dodoma ndo artificial kwa kufosi kingi kuhusu igombe na kayenze huko pameshakuwa sema serikali inachelewesha miundombinu mfano kata ya Bugogwa ambayo ni igombe mwaka 2012 ilikuwa na watu 39000 utasemaje ni vijijin vp takwimu za 2022
 
Kuna li project limoja huko Arusha yule kichaa the sunk cost kalipost kule kwenye battle asee lile ghorofa ni noma hata kabla halijaisha, mbona sisi huku vighorofa vinavyojengwa ni 7floors zikizidi Sana halafu building materials ni matofali tuu wenye hela mnakwama wapi kushusha vitu vya maana, we need modern city bna

Kero ya pili ni ile miwaya ya tanesco sijui waya za simu zile around the city center yani ni uchafu tuu
 
Ile institution investment.iliyo chini ya serikali...ni makao makuu ya umoja wa posta Africa..Wala hata usiogope .
 
Hao watu wataishi kwenye nyumba zilizopo, mbona ulaya wanaweza hakuna anayejenga kule hata hao footballers na pesa zao hswajengi. Kwa nini sisi tusiweze? Tuna utaratibu mbaya wa kupigia magoti matajiri ndio tatizo lilipo.
 
Na ndio imezalisha kata ya Shibula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…