Mwanza City: The Photo Gallery

Mwanza City: The Photo Gallery

Tatizo pia kwenye huo mradi wameweka mabati chakavu sasa hayo yananipa wasiwasi na huu mradi kama ni wauhakika au ni maduka tu kama ya mtaani kwetu, pia kama halmashauri wakiacha sehemu kama hiyo pajengwe bila kufuata master plan ya Mwanza CBD, tutakuwa na halmashauri ya ovyo sana.
Mbona kila siku tunasema exposure matters
 
Mabati chakavu haimaanishi mradi ni mdogo ....Kwa tuupe muda tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mbona kila siku tunasema exposure matters
hawa halmashauri wameruhusu NHC wajenge vibanda katikati ya mji, alafu kinachoniuma kwanini NHC wanadharau sana jiji la mwanza? je huko Dar wangeweza kujenga mabanda pale kariakoo kama walivyofanya kwa Mwanza? huu ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu mimi ningekuwa ni meya wa jiji aki ya mungu ningevunja vunja hayo mabanda ya maduka. Halmasahuri ijitathimini sana kwa utendaji wao wa kazi rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo.
 
NHC huwa ni wapuuzi sana! Yaani badala ya kujenga magorofa hapo mwanza na kupangisha kwa watu kwa bei affordable wao kazi yao ni kujenga majengo dodoma na Dar!
 
hii halmashauri wamezidiwa na dodoma ubunifu, halmashauri ya dodoma wa vitega uchumi vingi kama vile dodomd city hotel ambayo ni 10+ floor, kwanini Mwanza wasibuni miradi kama hiyo pale katikati ya jiji kwa kulipa fidia nyumba chakavu, pia kutengeneza recreational areas sehemu mbalimbli za jiji, lakini viongozi wapo wamelala huwa natamani ata kuwachapa viboko hawa viongozi wetu wapumbavu.
 
NHC huwa ni wapuuzi sana! Yaani badala ya kujenga magorofa hapo mwanza na kupangisha kwa watu kwa bei affordable wao kazi yao ni kujenga majengo dodoma na Dar!
huku Mwanza wametuona hatuna hadhi ya kuwa na magorofa ni vibanda tu tena kwenye cbd hii kitu huwa inaniuma sana hivi hawa huwa wanatuonaje watu wa nje ya Dar?
 
JIJI LA MWANZA NA JIJI LA TAMPERE NCHINI UFINI (FINLAND) LAWEKA MKATABA WA MIAKA MIWILI KUENDELEZA MAJIJI NA MAENDELEO ENDELEVU (SDG's)

Mstahiki Meya Jiji la Mwanza Mhe. Sima Constantine Sima pamoja na Mstahiki Meya jiji la Tampere Mhe. Matti Helimo wa nchini UFini (Finland) wameweka mkubaliano ya miaka miwili kutekeleza mradi utakaojulikana kama (Mwanza Tampere Sustainable Development Twinning Project) wenye lengo la kuhakikisha mpango wa umoja wa mataifa wa maendeleo endelevu (Agenda 2030) unatekelezwa Kwa pamoja.

Mkataba huo uliowekwa Leo tarehe 05.10.2022 Jijini Tampere baina ya Majiji Dada (twins sisters City) Jiji La Mwanza pamoja na Tampere unafadhiliwa na UN habitat ukihusisha miradi ya maendeleo kwa majiji hayo inayoenda sambamba na utekelezaji wa Malengo 17 ya dunia SDG ambapo Jiji la mwanza litakuwa la kwanza Nchini kutekeleza Katika ngazi ya mitaa kwa maendeleo endelevu ikijengewa uwezo kupitia ushirika wa Jiji la Tampere Ufini (Finland).

Hafla ya utiaji saini imehudhuliwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Yahaya Sekiete, Mwakilishi wa UN Habitat Finland na ALAT Tanzania. Meya jiji la Mwanza pamoja na ujumbe wake wapo nchini Ufini (Finland) kwa ziara ya kikazi itakayoisha 09.10.2022. katika ziara hiyo Mhe Sima amehudhuria kongamano Helsinki na sasa yupo Tampere kisha atamalizia ziara Hospital ya Hantaa kuwezesha hospital ya Nyamagana na anatazamia kutembelea kitengo ya wajasiriamali, Biashara na uwekezaji (Ensimetri) ili kujenga uwezo vikundi vya Akiba na Mikopo ambapo nchi ya Ufini ndio inaongoza kuwa na Ushirika Duniani. Kadharika Mhe. Sima atatembelea kituo cha Zimamoto Kusaidia kitengo cha Zimamoto Jiji la Mwanza kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo La Nyamagana🇹🇿
 
Hamna mtu mwenye mawasiliano na bw. Sina, mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri muwambie waje humu wachukue madini.....Kuna madini humu
 
sijaelewa hapo je vipi kuhusu mradi wa tampere park nao utajengwa au? hizo mikataba 17 ni zipi asee?
Hapo naona kitu cha maana ni hiyo tampere park kama haipo hapo hizo mikataba haitakuwa na maana kwa sasa.
 
Siasa nyingi sana Hawa watu utekelezaji 0
 
huu mradi wa tampere park kama umewashinda wauze eneo kwa sector binafsi sio lazima wao.
 
JIJI LA MWANZA NA JIJI LA TAMPERE NCHINI UFINI (FINLAND) LAWEKA MKATABA WA MIAKA MIWILI KUENDELEZA MAJIJI NA MAENDELEO ENDELEVU (SDG's)

Mstahiki Meya Jiji la Mwanza Mhe. Sima Constantine Sima pamoja na Mstahiki Meya jiji la Tampere Mhe. Matti Helimo wa nchini UFini (Finland) wameweka mkubaliano ya miaka miwili kutekeleza mradi utakaojulikana kama (Mwanza Tampere Sustainable Development Twinning Project) wenye lengo la kuhakikisha mpango wa umoja wa mataifa wa maendeleo endelevu (Agenda 2030) unatekelezwa Kwa pamoja.

Mkataba huo uliowekwa Leo tarehe 05.10.2022 Jijini Tampere baina ya Majiji Dada (twins sisters City) Jiji La Mwanza pamoja na Tampere unafadhiliwa na UN habitat ukihusisha miradi ya maendeleo kwa majiji hayo inayoenda sambamba na utekelezaji wa Malengo 17 ya dunia SDG ambapo Jiji la mwanza litakuwa la kwanza Nchini kutekeleza Katika ngazi ya mitaa kwa maendeleo endelevu ikijengewa uwezo kupitia ushirika wa Jiji la Tampere Ufini (Finland).

Hafla ya utiaji saini imehudhuliwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Yahaya Sekiete, Mwakilishi wa UN Habitat Finland na ALAT Tanzania. Meya jiji la Mwanza pamoja na ujumbe wake wapo nchini Ufini (Finland) kwa ziara ya kikazi itakayoisha 09.10.2022. katika ziara hiyo Mhe Sima amehudhuria kongamano Helsinki na sasa yupo Tampere kisha atamalizia ziara Hospital ya Hantaa kuwezesha hospital ya Nyamagana na anatazamia kutembelea kitengo ya wajasiriamali, Biashara na uwekezaji (Ensimetri) ili kujenga uwezo vikundi vya Akiba na Mikopo ambapo nchi ya Ufini ndio inaongoza kuwa na Ushirika Duniani. Kadharika Mhe. Sima atatembelea kituo cha Zimamoto Kusaidia kitengo cha Zimamoto Jiji la Mwanza kuwa na uwezo wa kukabiliana na majanga ya moto.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo La Nyamagana🇹🇿
UK
Utopolo tu,
 
Back
Top Bottom