Wakuu natanguliza shukrani za dhati kwenu wadau na wazalendo wa jiji letu la Mwanza na mkoa wetu wa Mwanza kwa ujumla.
Kumetokea teuzi za wakuu wa mikoa mbalimbali hapa nchi, kuna wengine wameachwa na wengine wakibadilishwa.
Kiini cha kuandika hapa leo ni kutaka kujua kutoka kwenu nyie wadau wa Mwanza, ni kipi kilichosababishwa mkuu wetu wa mkoa mchapa kazi eng.Robert Gabriel Luhumbi kutenguliwa ukuu wa mkoa wa Mwanza?
Kama kuna mdau atakayechangia naomba anitoe tongotongo kwani toka nijifahamu adi nimefika umri huu sijawahi kuona mkuu wa mkoa bora na mzalendo kama huyu ingawa kahudumu kwa muda mchache sana lakini kuna mengi mazuri na makubwa kafanya ndani ya mkoa wetu, yafuatayo ni mazuri aliyofanya japo ambayo mimi kitombile nitamkumbaka sana nazani haya ndio yalisababishwa atolewe?
1.kuhakikisha miradi ya mkoa wa Mwanza inakamilika kwa wakati?, kuna muda stendi na masoko yalikuwa yamesimama kutoka na pesa kutokufika kwa wakati badi kama mkuu wa mkoa alikuwa akiimiza serikali kupeleka pesa ili miradi ya mwanza ikamilike.
2.Kuzuia ubadhirifu wa pesa za umma, mfano alipoweka wazi wizi na ufisadi kwenye jengo la utawala la halmashauri ya sengerema.
3. Kukaa pamoja na wafanyabiasha mbalimbali wakubwa kwenye warsha mbalimbali na kuwasisitiza wafanye uwekezaji katika jiji la Mwanza.
4. Kuanzisha ujenzi wa shule 11000 katika mkoa wa Mwanza kwa nguvu za wananchi ili watoto wapate elimu bora
5.kuanzisha wazo la ujenzi wa barabara za lami ata kama ni 0.5km kwa pesa za tarura kuliko kutumia hizo pesa kwa kutengeneza na kuboresha mabarabara ya mjini yanayoharibika baada ya mvua kunyesha akasema ni bora tuwe tunajenga barabara imara kidogo kidogo kadri tutakavyopata pesa.
6.kupunguza ujenzi na wizi katika miradi ya kiserikali, majengo mengi yaliyojengwa chini ya kiwango aliweza kuyadhibiti.
7. Kuhimiza na kuanzisha ujenzi wa masoko mbalimbali kwa kuisumbua serikali kutafuta pesa kwaajili ya masoko ya mwanza kama ifuatavyo ujenzi wa soko la mchafu koge, makorobohi n.k alitaka yajengwe ikiwemo machinga complex.
N.B Mambo ni mengi sana adi nachoka kuandika inafikia hatua najiuliza huyu samia kwanini amefanya uhamuzi wa kumtoa huyu mkulungwa mzalendo.
Kama kuna mtu aranisaidia kuchukua hizi point na kuhanzisha uzi ni sawa tu lakini nimeona niandike humu wadau wa jiji la Mwanza wapate kuchangia kwa mawazo nimeandika sana nikiwa na mawazo sana juu ya hatima wa huu mkoa wangu.