Naamini KAMWE haiwez kuifikia Mlimani City ile iliyotumia Technolojia kali kabisa, wakandarasi wanne: Noremco- Civil Works, CSI Engineering-Structural Steel Works,Kampuni ya Roof ilitoka South Africa( jina limenitoka. Moja ya jambo ambalo tuliambiwa ni kuwa bati zitapigwa bila kutoboa bati kwa misumari, na ilikuwa hivyo, jamaa ni specialist kwa roofing works tu. Walikuja na mtambo wao ambao kwa kweli niliwakubali.
Mfumo wa AC ule ni Air Duct wataalam walitoka South Afrika. Zege ile ya floor ya jengo zima iliwekwa na Paver kama ile ya kuweka lami( asphalt concrere) na mtambo huu uitwao BidWell waliuleta NOREMCO, hata wale Makaburu waliofanya roofing walipiga picha na walikiri kuwa ni Technology ya kisasa kabisa. Nakumbuka hata zege tuliweka materials ziitwazo Rio Fibre na Rio Build. Naamini hao wajenzi wa huo mradi wa Mwanza wanaweza wakawa Wachina ambao ni wachakachuzi wa Ujenzi ila ni wazee wa fix au changa la macho kwenye finishing.
NOREMCO waliondoka nchini kwa kuwa ni sera ya NORWAY kutopendelea rushwa. Sasa trend ya kupata miradi Tanzania ilivyoingia muundo wa kirushwa rushwa wakaamua kuondoka nchini Tanzania. Mradi wao wa mwisho ulikuwa ni TBL pale Mbeya na Mlimani City Conference Centre. PPF Tower enzi hizo ni kazi ya NOREMCO, jengo zuri na refu la mwanzo nchini Tanzania, bila kusahau pale Akiba!