Kumbuka mlimani city slop rocky city gorofa
Naamini hata kama ni ghorofa, kwa prototype hiyo, haiwez kuifikia Mlimani City, mark my words! Hata parking bado haiwez kuwa sawa na pale Mlimani City. Hiyo ya Mwanza inakisiwa kuchukua magari 7000 kwa siku, wkat Mliman City ni magari 3000 kwa wakati mmoja! Hata hivyo hongera jiji la Mwanza kwa Mall ya kisasa
Kuhusu umiliki wa Serikali au Umma kwa ujumla pale Mlimani City, kwa kuwa nilikuwa tu upande wa ujenzi, tuliambiwa kuwa mradi ni wa miaka50 chini ya Mwarab wa Botswana, mwenye Malls nyingi kule SAfrika. Katika kipindi hicho, Mwarab atalipa kodi za serikali, atawapa mgawo kidogo UDSM, baada ya hapo ataipa serikali na kwa hapa ni UDSM. Mfumo huo unaitwa ni BOOT- Build, Own, Operate and Transfer! Huu ni tofauti na BOT au PPP, japo una mambo ambayo yanafanana!