Mwanza: Ajikata Nyeti na Kuzitupa Kwa Madai ya Kusumbuliwa na Ugonjwa

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
208
462
Mkazi wa Kijiji cha Kibitilo kata ya Ilula Wilayani Kwimba mkoani Mwanza Marco Samweli mwenye umri wa miaka 32 amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando baada ya kujikata nyeti zake kwa kutumia kisu na kisha kuzitupa kwa madai ya kuwa amechoka kuumwa ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa takribani miaka mitatu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea mara baada ya mwanaume huyo kutoka hospitali kwa kwaajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua na kueleza kuwa amekata tamaa ya kupona na kuamua kujikata uume wake.

Aidha kamanda Mutafungwa amesema kwa sasa mgonjwa huyo anapatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo kutokana na kitendo alichofanya cha kujijeruhi na pindi atakapopona jeraha lake atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.

Source: EastAfricaTV
 
Amekata National Resources
 
Back
Top Bottom