Mwanza: Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet

Mwanza: Afariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet

Nilikuwa mmoja wa Wasafiri hiyo Jana. Ndege baada ya kufika kwenye njia ya kupaa iliongeza mwendo tayari ku take off ghafla tukasikia kama tairi ya mbele imegonga kitu na ikawa kama inataka kuacha njia baadae ikarudi na kupaa huku Abiria wakiwa wameshtushwa na wale wenzangu na Mimi tukiwa tumeshasali sala ya toba! Hatukuelewa what happened!
 
Tena kama bajeti ni ndogo unaweza kujenga upande mmoja tu hadi juu huko. Inatosha kum discourage mwenda kwa miguu. Apumzike kwa amani
Hata uzio wa miba tu wameshindwa kuweka hawa "sheethole"....sa wanajifunza uzalendo gan?
 
Mwanza, Shinyanga na Geita...basi hili la kuruka na ungo robert sendabishaka kakusingizia maana mi najua 'marubani asili' wa nchi hii wanatokea Ziwa Tanganyika.

Au na kwenu wapo? Maana mzee baba si kwa kasi ile ya kuwajengea uwanja
utakuwa umemix mambo !marubani wa asili ni wasukuma mziee baba !hehehiyaa wanasafiria na FISI!
yule naye anajenga uwanja ambao sina hakika sana km una manufaa na kilikua kipaumbele ! uskikia neno 'mbiti' ndo hayo mafisi wanayosafiria !
 
b93fa7536f5816caa530cd32f8d8612c.jpg
Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya FastJet iliyokuwa ikiruka katika uwanja wa ndege wa Mwanza kuelekea Dar es salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.

Alisema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea Dar es salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.

"Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo treni", amesema Mayongela.

Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka, taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna chochote.

"Haijulikani mtu huyo alitokea wapi, vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika", amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalamu wa usalama uwanjani hapo.

"Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukubaliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia njia ya kurukia ndege", amesema.

Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.

Chanzo: Mwananchi
ameingia kwenye historia ya kugonga ndege
 
utakuwa umemix mambo !marubani wa asili ni wasukuma mziee baba !hehehiyaa wanasafiria na FISI!
yule naye anajenga uwanja ambao sina hakika sana km una manufaa na kilikua kipaumbele ! uskikia neno 'mbiti' ndo hayo mafisi wanayosafiria !
P1130221.JPG


Mimi MBIOOOOOOOO!
 
Au alidandia wakati wa taxiing
Maana kuna maswali kuliko majibu
 
Mwanza. Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.
Amesema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.


“Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege.


Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema Mayongela.
Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka, taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.
“Haijulikani mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.



Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama uwanjani hapo.
“Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia katika njia ya kurukia ndege,” amesema.



Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini
 
Kiukweli uwanja wa ndege Mwanza security bado ni changamoto mno hasa kwa maeneo yanayouzunguka uwanja. Mbali na kuwepo kambi ya jeshi karibu lakini changamoto ya kuwepo wavuvi na wakulima kuzunguka eneo la kingo za ziwa victoria hasa upande wa uwanjani/ilemela ni nyingi mno!

Wakati mwingine ninaamini kabisa pale panalindwa na Mungu zaidi ya mamlaka husika!
 
Tabora mmevamia tuu wenye mkoa wao ni wanyamwezi.
Unaanzaje kumtofautisha msukuma na mnyamwezi? Wewe unaonekana hujui lolote kuhusu huku.

Iko hivi kuna wasukuma wa aina nyingi sana mfano msukuma wa Kahama/mdakama lafudhi yake ni tofauti na hawa wa Mwanza. Pia wanyantuzu wa Bariadi ni tofauti na wale wa Shinyanga na Mwanza.

Pamoja na yote hayo, chukuwa myamwezi, msukuma wa Mwanza, mdakama wa Kahama na mnyantuzu wa Bariadi waweke pamoja wafanye kikao kwa pamoja hakuna ambaye hatamuelewa mwenzake anasema nini.

Wasukuma ni kabila kubwa na lugha hii ni pana sana na inamisamihati ya kutosha.
Mfano neno moja tu HAPANA linaweza kusemwa, yaayah, biyah, au ndohoh. Sasa hapo utasema ni makabila 3 tofauti?

Kipindi hicho wazungu hawajaita eneo lile Tabora wasukuma wa Mwanza walikuwa wanawaita wenzao wa Tabora kuwa ni watu wa magharibi yaani wa ng'weli, wazungu wakatohoa kuwa nyamwezi.

Unazani Makufuli siku alipofika Tabora akanza kuhutubia kwa kisukuma alikuwa anapoteza muda? alikuwa anajua nini anafanya.

Leo hii unapoongelea sukuma land hapo ni mikoa 5, Tabora, Shinyamga, Simiyu, Mwanza na Geita.
 
Back
Top Bottom