Mwanyika: Sihusiki na kashfa ya Richmond

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
na Mwandishi Wetu | Tanzania daima

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, amesema hana tatizo licha ya kutakiwa kujiuzulu na Kamati Teule ya Bunge, iliyopewa kazi ya kuchunguza mchakato wa zabuni ya Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond.

Aidha, Mwanyika alishindwa kuweka wazi dhamira yake ya ama kujiuzulu au kusubiri hatua za kinidhamu kutoka serikalini baada ya taarifa ya kamati hiyo iliyosomwa bungeni Jumatano wiki iliyopita kuanza kufanyiwa kazi.

Akizungumza kwa njia ya simu yake ya mkononi na Tanzania Daima jana, mwanasheria huyo alishindwa kabisa kusema dhamira yake. "Eeeh, ‘No comment'…unajingine?" aliuliza Mwanyika kabla ya kuhitimisha mazungumzo yake na gazeti hili.

Lengo la mwandishi wa habari hizi kumtafuta Mwanyika ni kujua hasa nia ya ama kujiuzulu au la, ya mwanasheria huyo anayetajwa kuhusika kwenye sakata la mkataba wa sh bilioni 172.9 kati ya serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Kampuni hewa ya Richmond.

Hata baada ya kumaliza mazungumzo na gazeti hili saa moja usiku, Mwanyika alituma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake wenye maelezo kuwa vyombo vya habari vinamfuata, lakini hana tatizo lolote na Mungu ndiye anayejua, hivyo anamwomba awasamehe wote.

Ujumbe huo ulisema: "Mnanitafuta lakini mjue kwamba mimi sina tatizo lolote. Mungu ndiye anayejua yote. Mimi namwomba awasemehe kwa hayo yote. Amen." Hata hivyo, juhudi za gazeti hili kumpigia simu ziligonga mwamba baada ya mwanasheria huyo kutopokea simu iliyotaka kufahamu nia ya Mwanyika kutuma ujumbe huo.

Aidha, taarifa ya kamati hiyo teule iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), ilisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshindwa kuiwakilisha vema serikali kabla ya kuingia kwa mkataba huo.

Taarifa hiyo ilibaini makosa mengi ya kisheria yaliyosheheni ndani ya mkataba huo, hali iliyoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalamu, ukosefu wa umakini ama ubinafsi kwa kushindwa kutambua ukosefu wa sifa za kikampuni zilizopo ndani ya Kampuni ya Richmond Development.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pia imeshindwa kuishauri serikali kuifanyia kampuni hiyo ukaguzi wa awali au ukaguzi, baada ya uteuzi na kushindwa kuona dosari za kisheria na kuona tofauti kisheria kati ya Kampuni ya Richmond, RDEVCO, RDVECO na RDC, majina ambayo wamiliki wa Richmond waliyatumia wakibadilisha badilisha kwa makusudi.

Pia taarifa ya Dk. Mwakyembe, iligundua kushindwa kwa Ofisi ya Mwanasheria huyo kuwashauri wajumbe wa Kamati ya Serikali ya Majadiliano (GNT) kuwa kadi ya biashara (business card) si mbadala wa hati mahususi kisheria na kushindwa kuishauri serikali kuhakikisha kuwa muhtasari wa majadiliano kati ya GNT na Richmond, ulizingatia baadhi ya masilahi ya nchi.

Mwanyika kupitia ofisi, na mwakilishi wake aliyetajwa kwa jina la Donald Chidowu, walishindwa kuishauri serikali kutumia fursa ya wazi ya kuvunja mkataba baada ya Kampuni ya Richmond kushindwa kutekeleza sehemu yake ya mkataba wake na kushindwa kuhudhuria idadi kubwa ya vikao muhimu vya majadiliano.

Kwa mujibu wa taraifa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika majadiliano yake na kamati hiyo, alionyesha kutoelewa kabisa kilichokuwa kinatendwa na wasaidizi wake.

Kwa maelezo hayo, kamati hiyo teule ilimtaka Mwanasheria Mkuu na Mwakilishi wake kuwajibishwa kinidhamu, kwa kuwa ushiriki wake kwenye GNT haukuwa na tija, hali iliyochangia kuliingiza taifa katika mkataba huu wa aibu uliogharimu sh bilioni 172.9.

Baada ya kusomwa kwa taarifa ya kamati hiyo iliyofanya kazi kwa siku 45 chini ya uenyekiti wa Dk. Mwakyembe, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, alijiuzulu kwa tuhuma za kushinikiza ushindi wa zabuni ya kampuni hiyo na kusababisha Rais Jakaya Kikwete, kuvunja Baraza la Mawaziri.

Pamoja na Lowassa, mawaziri wengine walioguswa kwa tuhuma za kuiingiza nchi kwenye mkataba huo wa aibu na hasara ambao nao walijiuzulu ni Nazir Karamagi, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini. Waziri huyu anatuhumiwa kushabikia mkataba huu huku akijua fika kuwa na hasara kwa taifa.

Naye aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Dk. Ibrahim Msabaha, alijiuzulu baada ya kutakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuliingiza taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni, uliosababisha hasara, ambapo sasa Kampuni ya Dowans, iliyorithi mkataba wa Richmond kulipwa sh milioni 152 kila siku kwa miaka miwili.
 
Unajua tatizo la Mwanyika ni moja. Hatusemi amehusika lakini kama ripoti ilivyosema "Yeye kama AG hakuishauri Serikali kwenye uwanja wake wa kujidai - Legal Aspects".................... Tukumbuke wote kuwa:
1. Mwizi ni yule aliyegundulika na kuwa proved kuwa ni mwizi
2. Mwizi ni yule aliyesaidia wizi utokee
3. Mwizi ni yule aliyeona mwizi akiiba na hakusema kitu
4. Mwizi can also be yule ambaye wizi umetokea katika himaya yake lakini akakaa kimya bila kusema kitu.

Sasa ndugu Mwanyika inabidi ajihoji mwenyewe yeye yupo katika kundi gani and/or atuhakikishie kuwa sio mmojawapo wa makundi hayo matatu. Mimi kama Morani nakubali kuwa ninaweza kuwepo katika kundi la tatu "3" lakini sikuwa na ushahidi hivyo nimepona. Kwa sasa after Mwakwembe's report nilipiga kelele za mwizi na mambo yakawa sawa, ha ha haaaaa!! So dhambi ya wizi ikanipitia pembeni!!!

Haya tungoje ni wangapi watajishataki wenyewe kwenye dhambi hizo nne "4" za wizi hapo juu!!!

Mungu Ibariki Tanzania............
 
Wasemavyo waswahili, mfa maji haachi kutapatapa.Kuna kitu kinaitwa crimes of ommission.Mtu amwambie hio kitu!
 
Atuambie ni vipi alizuia ufisadi usitendeke kwa kuishauri GNT wasiingie kwenye mkataba? hili ni swali ambalo hata yule mama Zakia inabidi alijibu, baada ya kudanganywa na Balalli kama anavyotaka tuamini, alifanya nini kuhakikisha mwajiri wake anajua na kuzirudisha pesa ambazo hazikutumika kwa matumizi halali ya serikali kama barua yake ilivyosema?
 
Naamini sasa kuwa Serikali ya Tanzania haina wanasheria? Kama Mh. Mwanyika anataka kutuambia kuwa haujui kuwa ukiona kosa ukafumbia macho na kukaa kumya ni kosa kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchii hii, hii ni sababu tosha ya kumtoa katika nafasi hii mara moja. :( Mwanyika rudi shule Teana brother
 
Naomba ajiulize swali moja "Nikwanini Mzee Mwinyi alijiuzulu akipata jibu basi apime uzito wa hoja yake na afanye maamuzi.
 
Hivi katiba ya nchi inasemaje kuhusu nafasi ya mwansheria mkuu barza likivunjwa. Fom my simple logic thinking nafikiri jamaa alipoteza kazi siku ile balaza lilipovunjwa since is one of the ministers. Unless I am missing something!! Naomba kuelimishwa kwa hili.
 
It is obvious kwamba JK anajua memgi juu AG.Huyu jamaa kachukua nafasi ya Chenge .Leo Chenge ni waziri na walikuwa mlango mmoja na JK wa kuingilia those days .Chenge , Maria Kejo na wengine wengi wanaujua uchafu wote wa mikataba a ndipo akawekwa jamaa kuziba pengo. JK siamini kama atamwacha kama kafikia hata kuvunja baraza.AG hajatumia busara kama za Kingunge na wengine wa kusoma alama za Nyakati .Watanzania hatumwamini tena yeye aondoke kwa amani .
 
Hivi katiba ya nchi inasemaje kuhusu nafasi ya mwansheria mkuu barza likivunjwa. From my simple logic thinking nafikiri jamaa alipoteza kazi siku ile balaza lilipovunjwa since is one of the ministers. Unless I am missing something!! Naomba kuelimishwa kwa hili.
 
Ukisema Bangusilo ina maana unaasema ataonewa hahusiki .Is this your statement Masatu ?

Lunyungu

Hamuoni Mwanyika anavyotia huruma na "kumuachia" Mungu... I feel sorry 4 him I can bet hawakumpa hata senti tano...
 
Attorney General ni sehenu ya cabinet, kwa hiyo baada ya cabinet kuvunjwa, nadhani kuwa Mzee Johnson Mwanyika naye hana kazi kwa sasa hivi. Ingawa ni mwanasheria mzuri sana, hasa aliposimamia zile kesi za uhaini za akina McGhee mwanzoni mwa miaka ya 80. Ameshindwa kuhakikisha kuwa mikataba ya nchi ni kwa manufaa ya nchi, hiyo ni failure for which he has to pay.
 
Mwalimu, AG ni mjumbe wa Cabinet lakini siyo Waziri. Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa anapewa haki zote za kuzungumza na kutoa maoni yake isipokuwa haki ya kupiga kura. Nafasi yake iko kama ya Katibu wa Baraza la Mawaziri ambaye anakuwemo humo lakini siyo sehemu ya Baraza hilo na likivunjwa yeye hapotezi kazi yake. Hivyo, AG ana procedure tofauti ya kuondolewa madarakani.
 
Inavyoeleweka duniani, AG yeyote yule ana majukumu yafuatayo:
1. Ndiye mshauri mkuu wa serikali wa masuala yote ya sheria e.g. uhalali wa maamuzi, sera mbalimbali.
2. Ndiye mshauri mkuu na mwakilishi wa serikali mahakamani nje na ndani ya nchi.
3. Ndiye mtetezi/mwangalizi wa maslahi ya umma katika deal yoyoye ile ambayo serikali inaingia na makampuni binafsi.
4. Ndiye mpatanishi/msuluhishi unapotokea mngongano wa kisheria kati ya wizara na idara mbali mbali za serikali.
5. Ndiye msimamizi wa kesi zote za jinai. kwa tanzania na kesi za madai pia.
6. Ndiye custodian wa mikataba ya serikali.
sasa inapokuja kwa Tanzania:

Ibara ya 59 ya katiba yetu, inaunda nafasi ya Attorney General na inabainisha sifa za uteuzi. Katiba inasema wazi kwamba AG atakuwa mbunge automatically kutokana na cheo chake (ex officio member) lakini haisemi hivyo kuhusu cabinet. Badala yake ibara ya 54 inasema kwamba mwanasheria mkuu wa serikali atahudhuria mikutano yote ya cabinet na atakuwa na haki zote isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura.. Hii ni tofauti na nchi kama marekani ambapo AG is a member of the CABINET hivyo ushauri wake unakuwa compromised na party ideology. Kwa mfano hapa kwetu was it Warioba aliyekuwa Waziri wa Sheria na Mwanasheria mkuu pia at the same time? mambo ya kofia mbili hayo!

Sasa hii ina maana gani kuhusu mwanyika?

1. Technically bado yeye ni AG, kwani ingawa anahudhuria vikao vya baraza la mawaziri yeye siyo mwanachama, na harusiwi kupiga kura humo. Hivyo hawezi kuwajibishwa kwa maamuzi ya cabinet labda pale itakapodhihirika alitoa ushauri mbaya kwa cabinet.

2. Katika mojawapo ya maajabu yaliyogunduliwa na kamati ya Mwakyembe ni kwamba Lowassa na Msabaha walikuwa wakitenda kinyume na uamuzi wa baraza la mawaziri! Yaani hawa jamaa walikuwa na kiburi na udhubutu wa kutekeleza kinyume na maagizo ya baraza la mawaziri. In this regard Mwanyika is off the hook...temporarily though! Hapa Kikwete inabidi atuambie..inakuwaye yeye kama mwenyekiti wa Baraza la mawaziri maamuzi hayafuatwi? Je ni katika hili la richmind pekee ambapo maamuzi ya baraza la mawaziri hakufuatwa?? what else?

3. Kinachomponza mwanyika ni kwamba Attorney General ndiye mwakilishi wa serikali katika kunegotiate mikataba. Tume ilipokuwa inamhoji alionyesha wazi kabisa kwamba alikuwa hana habari nini kinaendelea! Sasa huo mkataba ulisainiwa vipi? Sasa inamaana kwamba kulikuwa hakuna mawasiliano kati ya mwanyika na mwanasheria wa serikali alyekuwa anamwakilisha? In this regard Mwanyika kama AG kashindwa kusimamia 'public interest' mpaka taifa linaingizwa hasara ya mabilioni na kampuni ya mifukoni ambayo 'haiwezi kuchomeka hata bulb'. Aibu kubwa!hapa Mwanyika hata afurukute namna gani. lazima akubali kuwajibika.

4. Pamoja na kuachia ngazi kwa mwanyika ( i assume he will do the honourable thing!), tume ilitakiwa ipendekeze mapitio ya utaratibu mzima namna 'mawakili wa serikali' wanavyo simamiwa katika shughuli zao za uwakilishi kwenye wizara na bodi mbalimbali. hapa kuna weakness kubwa sana. serikali nyingi duniani huwa zinakodisha huduma za wanasheria na wataalamu wengine binafsi iwapo issue ni nzito...sambamba na kuendeleza wataalamu wake yenyewe!!
 
Lunyungu

Hamuoni Mwanyika anavyotia huruma na "kumuachia" Mungu... I feel sorry 4 him I can bet hawakumpa hata senti tano...

Hata Lowasa alijifananisha na Yesu lakini akapigwa chini. Hata Majambazi wakati mwingine huomba Mungu awasaidie, hivyo sishangai Mwanyika kujiumbua utakatifu wakati mazingira yanaonyesha kinyume chake. Ni muhimu na yeye apigwe chini.
 
Inavyoeleweka duniani, AG yeyote yule ana majukumu yafuatayo:
1. Ndiye mshauri mkuu wa serikali wa masuala yote ya sheria e.g. uhalali wa maamuzi, sera mbalimbali.
2. Ndiye mshauri mkuu na mwakilishi wa serikali mahakamani nje na ndani ya nchi.
3. Ndiye mtetezi/mwangalizi wa maslahi ya umma katika deal yoyoye ile ambayo serikali inaingia na makampuni binafsi.
4. Ndiye mpatanishi/msuluhishi unapotokea mngongano wa kisheria kati ya wizara na idara mbali mbali za serikali.
5. Ndiye msimamizi wa kesi zote za jinai. kwa tanzania na kesi za madai pia.
6. Ndiye custodian wa mikataba ya serikali.
sasa inapokuja kwa Tanzania:

Ibara ya 59 ya katiba yetu, inaunda nafasi ya Attorney General na inabainisha sifa za uteuzi. Katiba inasema wazi kwamba AG atakuwa mbunge automatically kutokana na cheo chake (ex officio member) lakini haisemi hivyo kuhusu cabinet. Badala yake ibara ya 54 inasema kwamba mwanasheria mkuu wa serikali atahudhuria mikutano yote ya cabinet na atakuwa na haki zote isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura.. Hii ni tofauti na nchi kama marekani ambapo AG is a member of the CABINET hivyo ushauri wake unakuwa compromised na party ideology. Kwa mfano hapa kwetu was it Warioba aliyekuwa Waziri wa Sheria na Mwanasheria mkuu pia at the same time? mambo ya kofia mbili hayo!

Sasa hii ina maana gani kuhusu mwanyika?

1. Technically bado yeye ni AG, kwani ingawa anahudhuria vikao vya baraza la mawaziri yeye siyo mwanachama, na harusiwi kupiga kura humo. Hivyo hawezi kuwajibishwa kwa maamuzi ya cabinet labda pale itakapodhihirika alitoa ushauri mbaya kwa cabinet.

2. Katika mojawapo ya maajabu yaliyogunduliwa na kamati ya Mwakyembe ni kwamba Lowassa na Msabaha walikuwa wakitenda kinyume na uamuzi wa baraza la mawaziri! Yaani hawa jamaa walikuwa na kiburi na udhubutu wa kutekeleza kinyume na maagizo ya baraza la mawaziri. In this regard Mwanyika is off the hook...temporarily though! Hapa Kikwete inabidi atuambie..inakuwaye yeye kama mwenyekiti wa Baraza la mawaziri maamuzi hayafuatwi? Je ni katika hili la richmind pekee ambapo maamuzi ya baraza la mawaziri hakufuatwa?? what else?

3. Kinachomponza mwanyika ni kwamba Attorney General ndiye mwakilishi wa serikali katika kunegotiate mikataba. Tume ilipokuwa inamhoji alionyesha wazi kabisa kwamba alikuwa hana habari nini kinaendelea! Sasa huo mkataba ulisainiwa vipi? Sasa inamaana kwamba kulikuwa hakuna mawasiliano kati ya mwanyika na mwanasheria wa serikali alyekuwa anamwakilisha? In this regard Mwanyika kama AG kashindwa kusimamia 'public interest' mpaka taifa linaingizwa hasara ya mabilioni na kampuni ya mifukoni ambayo 'haiwezi kuchomeka hata bulb'. Aibu kubwa!hapa Mwanyika hata afurukute namna gani. lazima akubali kuwajibika.

4. Pamoja na kuachia ngazi kwa mwanyika ( i assume he will do the honourable thing!), tume ilitakiwa ipendekeze mapitio ya utaratibu mzima namna 'mawakili wa serikali' wanavyo simamiwa katika shughuli zao za uwakilishi kwenye wizara na bodi mbalimbali. hapa kuna weakness kubwa sana. serikali nyingi duniani huwa zinakodisha huduma za wanasheria na wataalamu wengine binafsi iwapo issue ni nzito...sambamba na kuendeleza wataalamu wake yenyewe!!

Pale sheria kuna mtu anaitwa Maria Kejo .Slaa did mention her name and she has implicated several times na mambo ya mikataba hii .She is monster when it comes for money na % ya kwenye mikataba .Huyu ana power kuliko Mwanyika .Chunguza utajua .
 
Back
Top Bottom