Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Hivi karibuni ,tarehe 2 Machi 2010 Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe Aggrey Mwanri alizindua ukarabati wa kisima cha maji katika Jimbo la Kibakwe.Wakati anazindua maji yalikuwa yanatoka kwenye mabomba tena kwa wingi tu.Chakushagaza wakazi wa eneo hilo waliopatiwa kisima hcho kwaajili ya kukabiliana na tatizo la maji hawayapati maji hayo kwani kisima hicho hakitoi maji yeyote.Ikumbukwe kuwa Kisima hicho kimezinduliwa ndani ya mwezi huu machi. Tulipokuwa kwenye Operesheni Sangara katika jimbo hilo tuliambiwa kuwa kisima hicho hakitoa maji na hivyo wananchi bado wanapata tatizo la maji kama ilivyokuwa awali. Inasemekana kwamba Mkandarasi alimadanganya mheshimiwa Mwanri kwa kujaza maji kwenye kisima hicho na hivyo kufanya maji yawe yanatoka kwa kipindi cha muda mfupi sana..
Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa kisima hiki ulifanyika kwa mbwembwe na kupewa vipaumbele kwenye vyombo vya habari na pesa pia imetumika katika uzinduzi huu fake...
Habari ndio hiyo.
Kisima chenyewe hiki hapa.
Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa kisima hiki ulifanyika kwa mbwembwe na kupewa vipaumbele kwenye vyombo vya habari na pesa pia imetumika katika uzinduzi huu fake...
Habari ndio hiyo.
Kisima chenyewe hiki hapa.