Mwanri Umezindua Mradi wa Maji Fake

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Hivi karibuni ,tarehe 2 Machi 2010 Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe Aggrey Mwanri alizindua ukarabati wa kisima cha maji katika Jimbo la Kibakwe.Wakati anazindua maji yalikuwa yanatoka kwenye mabomba tena kwa wingi tu.Chakushagaza wakazi wa eneo hilo waliopatiwa kisima hcho kwaajili ya kukabiliana na tatizo la maji hawayapati maji hayo kwani kisima hicho hakitoi maji yeyote.Ikumbukwe kuwa Kisima hicho kimezinduliwa ndani ya mwezi huu machi. Tulipokuwa kwenye Operesheni Sangara katika jimbo hilo tuliambiwa kuwa kisima hicho hakitoa maji na hivyo wananchi bado wanapata tatizo la maji kama ilivyokuwa awali. Inasemekana kwamba Mkandarasi alimadanganya mheshimiwa Mwanri kwa kujaza maji kwenye kisima hicho na hivyo kufanya maji yawe yanatoka kwa kipindi cha muda mfupi sana..

Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa kisima hiki ulifanyika kwa mbwembwe na kupewa vipaumbele kwenye vyombo vya habari na pesa pia imetumika katika uzinduzi huu fake...

Habari ndio hiyo.

Kisima chenyewe hiki hapa.
 
Attachments

  • DSC03418.JPG
    DSC03418.JPG
    262.2 KB · Views: 96
  • DSC03411.JPG
    DSC03411.JPG
    395.8 KB · Views: 65
Kwani ni kitu gani kilichozinduliwa hata na RAHISI mwenyewe kikadumu?
Anazindua majumba yaliyojengwa kinyume na ramani za TANROADS na yanavunjwa immediately akiondoka, but no one cares!
Ni utamaduni wa kawaida kwa irresponsible leaders wa Tanzania...Hata ukimuuliza alichofanya jana amesahau!
 
Inanikumbusha enzi zile Mwalimu Nyerere akienda kutembelea mashamba ya Mboga mboga katika vijiji vya ujamaa... Wanapanda kabichi kuubwa siku tatu kabla... Yaani aliyetuloga Wallah ameshafariki...
 
Unashauri nini kifanyike?
 
-huu ni uozo na uzembe kama kawaida,hapo wakaguzi wa huo mradi wanatakiwa wawajibishwe ipasavyo

-Nani alikua anafanya project appraisal,na je project evaluation?

Hapo ni kuwajibishana hatua kwa hatu tu,hakuna mjadala.Uzembe umetugharimu sana
 
Subirini, watazindua miradi mingi feki hasa ya maji karibia na uchaguzi!!! Imagine kuna mradi wa maji wa visima vikubwa wamechimba Mbagala kwa ajili ya kusambaza maji karibia wilaya yote ya Temeke sehemu chache Ilala (kuongezea nguvu current flow) na uko tayari siku nyingi ila unasubiri kuzinduliwa jirani na kampeni. Yaani wananchi wanakunywa maji machafu na kufa kwa kipindupindu kwa kusubiri fujo za Chama. Lo!
 
Wangeanza kusambaza kwanza halafu Mkulu aje kwa MBWEMBWE baadaye... Mmmh...
 
attachment.php
Hivi karibuni ,tarehe 2 Machi 2010 Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe Aggrey Mwanri alizindua ukarabati wa kisima cha maji katika Jimbo la Kibakwe.Wakati anazindua maji yalikuwa yanatoka kwenye mabomba tena kwa wingi tu.Chakushagaza wakazi wa eneo hilo waliopatiwa kisima hcho kwaajili ya kukabiliana na tatizo la maji hawayapati maji hayo kwani kisima hicho hakitoi maji yeyote.Ikumbukwe kuwa Kisima hicho kimezinduliwa ndani ya mwezi huu machi. Tulipokuwa kwenye Operesheni Sangara katika jimbo hilo tuliambiwa kuwa kisima hicho hakitoa maji na hivyo wananchi bado wanapata tatizo la maji kama ilivyokuwa awali. Inasemekana kwamba Mkandarasi alimadanganya mheshimiwa Mwanri kwa kujaza maji kwenye kisima hicho na hivyo kufanya maji yawe yanatoka kwa kipindi cha muda mfupi sana..

Ikumbukwe kuwa uzinduzi wa kisima hiki ulifanyika kwa mbwembwe na kupewa vipaumbele kwenye vyombo vya habari na pesa pia imetumika katika uzinduzi huu fake...

Habari ndio hiyo.

Kisima chenyewe hiki hapa.
 
Kwa jinsi nilivyokasirika jinsi Waziri mchapakazi huyu alivyoingizwa mkenge... Imenibidi nimtumie link pamoja na Attachments kwenye Mail yake... amwanri@parliament.go.tz

Kama nilivyotabiri...
Hi. This is the qmail-send program at yahoo.com.
I'm afraid I wasn't able to deliver your message to the following addresses.
This is a permanent error; I've given up. Sorry it didn't work out.
:confused::confused::confused::confused:
 
Hii picha ilipigwa na Kamera Aina ya Sony DSC-S750 Machi 25 saa nne na dakika 50 asubuhi. Kamera hii toka inunuliwe haijapiga picha 4000, kwa hiyo inaonesha ni kamera mpya.
base_media
 
Ile picha ya jiwe la msingi ndio ilipigwa kwanza (saa nne na dakika 48 asubuhi). Picha ilikuwa na flashi. Ile picha ya tenki haikuwa na flashi. Mpiga picha wetu alipiga picha sita (hajaziambatanisha) baada ya jiwe la msingi, kabla ya kupiga picha ya tenki.
 
Mkuu kama unaweza kuwa na utambuzi huu kwanini basi hamtoi elimu ya kutambua visima feki?
 
Kwani kamera yenyewe ina rangi kama hiyo?

Well... kutambua visima feki panahitaji elimu?
 
Inanikumbusha enzi zile Mwalimu Nyerere akienda kutembelea mashamba ya Mboga mboga katika vijiji vya ujamaa... Wanapanda kabichi kuubwa siku tatu kabla... Yaani aliyetuloga Wallah ameshafariki...

Utaua.
Yaani nimecheka hadi basi. Jamaa walikuwa wanategeshea kabichi!! Lakini afadhali na hao walikuwa na akili kuliko wale wanaopaka majengo rangi siku mkubwa anapofanya ziara
 
Back
Top Bottom