Mwandosya alifuata nini Butiama?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
2B.jpg

miaka kadhaa iliyopita Mwandosya alikwenda kumtembelea mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama. Mwandosya alifuata nini kwa mwalimu?
 
Asiee hapo nawaona kina Bnard Nzugu(mwenye Suti ya Blue),ambaye ni Afisa Tawala wa Iringa kwa sasa,Mmoja ya watu waliofanya kazi pale Mara kwa muda mrefu sana..Kwa kuwa namfahamu nitamtafuta na kumuuliza kama anakumbuka ni nini mwalimu aliwaambia wakina Mwandosya..
 
Hiyo picha isingekuwa na Mwalimu ningesema alienda kutembea.. lakini jibu la swali mbona liko kwenye picha!? Lakini zaidi ni kuwa watu hao wengine sita walienda kutafuta nini Butiama, iweje swali lielekezwe kwa Mwandosya?
 
View attachment 1798

miaka kadhaa iliyopita Mwandosya alikwenda kumtembelea mwalimu Nyerere nyumbani kwake Butiama. Mwandosya alifuata nini kwa mwalimu?

Kweli hapo NIDHAMU YA WOGA ILIKUWA WAZI!
Yani ni kama wako na MUNGU MTU!
Haswa haswa huyo mwenye suti nyeupe ya kijamaa!
Mwalimu alijitwisha mzigo wote wa kuliongoza Taifa na ndio maana baada ya kufa kwake linayumba!
Lakini mwishowe utakuwa mzuri kwani sasa ni wadau wote wa nchi watashirikishwa kwenye ujenzi wa TAIFA!
NB:Huyo aliyeko kulia kabisa ni MUSEVENI,CHEYO...Ama macho yangu?
Maana Kinana ni light skin zaidi!
 
Mwandosya ni "Prominent figure" kuliko hao wenngine labda analingana na Joseph nyerere huyo aliye nyuma ya mwalimu. kwa kawaida hata bush alikuja na watu wengine zaidi ya 300 lakini aliyetajwa kwamba alikuja Tanzania ni yeye na siyo hao wengine 300!! Tafakari??!!
 
Asiee hapo nawaona kina Bnard Nzugu(mwenye Suti ya Blue),ambaye ni Afisa Tawala wa Iringa kwa sasa,Mmoja ya watu waliofanya kazi pale Mara kwa muda mrefu sana..Kwa kuwa namfahamu nitamtafuta na kumuuliza kama anakumbuka ni nini mwalimu aliwaambia wakina Mwandosya..

Samahani...Sikuona kuwa ni NZUGU!
Samahani kwa usumbufu kwani UPARA WAKE UMEKAA KICHEYO AMA MUSEVENI AMA KINANA.
Nashukuru kwa info!
Ila wengineo ni kina nani hao?
 
Mwandosya ni "Prominent figure" kuliko hao wenngine labda analingana na Joseph nyerere huyo aliye nyuma ya mwalimu. kwa kawaida hata bush alikuja na watu wengine zaidi ya 300 lakini aliyetajwa kwamba alikuja Tanzania ni yeye na siyo hao wengine 300!! Tafakari??!!

Sasa kila mtu akitoa picha na yale waliozungumza na MWALIMU NA SHERRIF HAMAD WA CUF MBONA HASIKILIZWI?
Ama hii nayo PROPAGANDA ZA KUMWAKILISHA Mwandosya?
Mtu aliyetayarishwa na mwalimu hatumtaki tena kwa ya MKAPA YAMETOSHA!
TUACHANE NA MAMBO YA ZAMANI NA TUJENGE TAIFA!
Tuzingatie tu UMOJA!
 
Kweli hapo NIDHAMU YA WOGA ILIKUWA WAZI!
Yani ni kama wako na MUNGU MTU!
Haswa haswa huyo mwenye suti nyeupe ya kijamaa!
Mwalimu alijitwisha mzigo wote wa kuliongoza Taifa na ndio maana baada ya kufa kwake linayumba!
NB:Huyo aliyeko kulia kabisa ni MUSEVENI,CHEYO...Ama macho yangu?
Maana Kinana ni light skin zaidi!

hapo hakuna Kinana wala Museveni na wakati mwingine nikiiangalia hii picha huwa najiuliza hofu ya waliokuwa wanakutana na Mwalimu ilitoka wapi? Huyo mwenye suti nyeupe ni Mdogo wake Joseph Nyerere mtu pekee anayetajwa kubishana mara kwa mara na Mwalimu.

kuna wakati job Lusinde aliwahi kusema mawaziri walikuwa wakisikia kwamba wanaitwa Ikulu na mwalimu walikuwa wanatetemeka kama wanakwenda kuliwa na simba,na alisema kwamba mara nyingi mawaziri wengi hata wasaidizi wake walikuwa wanashindwa kuangaliana na mwalimu Uso kwa Uso!
 
Sasa kila mtu akitoa picha na yale waliozungumza na MWALIMU NA SHERRIF HAMAD WA CUF MBONA HASIKILIZWI?
Ama hii nayo PROPAGANDA ZA KUMWAKILISHA Mwandosya?
Mtu aliyetayarishwa na mwalimu hatumtaki tena kwa ya MKAPA YAMETOSHA!
TUACHANE NA MAMBO YA ZAMANI NA TUJENGE TAIFA!
Tuzingatie tu UMOJA!

Tusiwe kama kichwa cha mwendawazimu katika kufikiri,kila jambo si lazima lihusishwe na siasa,picha hii haihusiani na propaganda za yeyote yule kutayarishwa kwa chochote kile,nimeiweka kuleta Sai (challenge) ya wana JF kufikiri!

Picha hii inaweza kuwa pia ni changamoto (catalyst) ya wale wanaopenda kuyajua mambo kijujuu,kwani ni Kikwete wanamtandao wenzake waliokuwa wanamwita mtoto wa Mwalimu na si Mwandosya. Tafakari!!
 
Hapo alikuwa kwenye mikutano ya kiserikali akaona ni bora aweze kumsalimia mzee kwani sidhani kama wakati huo alikuwa na ndoto za Urais.........

Kwani hata shati lake alilovaa wakati ule nakumbuka vijana walikuwa wanaliita bahama mama na wa mjini wakiliita ujiuji...........
 
Hiyo picha isingekuwa na Mwalimu ningesema alienda kutembea.. lakini jibu la swali mbona liko kwenye picha!? Lakini zaidi ni kuwa watu hao wengine sita walienda kutafuta nini Butiama, iweje swali lielekezwe kwa Mwandosya?
Hao wengine kama nilivyosema hapo juu ni viongozi wa serikali na CHama,nadhani kama ilikuwa Ziara Mwandosya akiwa waziri
 
1. Viongozi wa sasa waache kabisa kumtamka mwalimu, nimeangalia alipo na nikaangalia vijana wawili walionyuma yake. Nakuhakikishia hakuna kiongozi wa sasa anayeweza kukaa na watoto kama wale kwenye mazingira yake wakati kumekuja wageni.

2. Mwandosa ni kati ya watu wachache walioweza kuwa academician wazuri pia mwanasiasa. Sijui kwa nini alichagua kuwa Engineer maana inaonekana alipenda sana siasa.
 
Kuwa na watoto kama hao kwenye background kumesaidia nini zaidi ya mafisadi kuzitumia hizo picha kuomba msaada wa pesa na huku wakiuza nchi kwa kutumia sera zile zile za MWALIMU?
Mwalimu was ok..But then he was very wrong!
Nia alikuwa nayo nzuri!
UBISHI NA DOUBLE STANDARD NA UKABILA NDILO TATIZO KUBWA LILILOMKABILI!
 
By then he was katibu mkuu ktk moja ya wizara chini ya Utawala wa Mwinyi
 
Back
Top Bottom