Mwandishi wa Vitabu pitia hapa

Investaa

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
794
656
Habari wana JF,

Ni kitambo kidogo sijaonekana humu JF, leo nimeona nitoe ushauri kwa waandishi wa vitabu; nimepokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wakitaka kujua namna ya kuuza vitabu vyao online(e-book) na namna ya kupata jukwaa nzuri la kuuza vitabu vyao bila kutapeliwa na wajuaji online.

Mwaka 2019 nilitengeneza platform ambayo ingewasaidia waandishi kuuza vitabu vyao online bila kusambaa mitandaoni na waandishi kupata pesa wanayostaili kupata kila mwezi, lakini waandishi wengi uelewa ni mdogo kuhusu ebook, wengi wao wanaishi kutapeliwa ingawa unaingia nao mkataba. Nilipata nafasi ya kuongea na mwandishi mkubwa sana wa hapa jf anaandika simulizi za kijasusi, uzuri alitoa mawazo yake namna app inatakiwa kuwa na nikampa mchanganua wa biashara tutakavyofanya kisomi kwa kuingia mkataba wa kisheria ili kila mtu awe safe kwa upande wake.

Tufika mahali tukakubaliana ikabaki mm kutengeneza app, baada ya wiki kadhaa nilimaliza na kumtumia app atest ili kinachofuata ni kuingia mkataba na kuanza kupakia vitabu kwenye app, na hiyo kazi anaifanya mwenyewe maana kwenye app kuna sehem ya mwandishi kupakia vitabu na sehemu ya admin kuona vitabu vyote kwenye app.

Kilichonishangaza no feedbak na nikimpigia sim hapokei . App nilitengeneza iwe inaruhusu watu kusoma vitabu vyote kwenye app kwa malipo ya 3000 kwa mwezi, kama netflix wanavyofanya. Kila mwezi wasomaji wanalipia tena kusoma vitabu kitu ambacho tungepata wasomaji wengi sana kutokana na bei kuwa ndogo.

Huyu mwandishi ana wasomaji kama 500k kwa mwezi hapa JF, na kila msomaji anajua madini ya huyu mwandishi ni rahisi kupata watu 10k kwa mwezi kulipia kutokana na simulizi zake.

Juzi nimeona kwenye account yake ya fb anauza kitabu sh 50k.

Ukiwa kama mwandishi jifunze kubadilika kutokana na mazingira, watu wamehamia kwenye simu inabd uhame nao. Hardcopy ni gharama sana kuuza kutokana na gharama ya uchapishaji, ili softcopy gharama ni bando tu. Kingine ni rahisi sana kuuza nakala nyingi online kuliko offline , kwasababu online bei yake ni ndogo ukilinganisha na offline. Mfano online wasomaji wanalipia kwa mwezi sh 3000 wanasoma vitabu vyote kwenye app bila ata kupakua wala kukopi, offline msomaji lazima awe anakipato kikubwa kununua kitabu, kitabu unauziwa 50k, nani yupo radhi kununua kitabu 50k na hali hii ya uchumi.

Biashara yoyote ukiwatenga maskini uwezi kufanikiwa kwenye biashara yako, jifunze kwa azam bidhaa zake, mfano kwenye king'amuzi cha azam kuna kifurushi cha siku ambacho 1000, mchezo kama simba vs yanga unadhani watu wanaolipia kifurushi hicho kuangalia mechi hiyo inaweza fika ata 1m.

1m x1000 = ? Kwa mechi moja ya simba vs yanga. Azam anadili na watu wote kwenye bidhaa zake, fanya utafiti utaona.

Ushauri kwa waandishi
1. Undeni chama cha wandishi wa vitabu kwa kujisajiri serikalini ili kiwe kinatambulika kuepuka kutaliwa na wajuaji
2. Weka ada ya kujiunga kwenye uwanachama kwa kila mwandishi anayetaka kuuza viatbu vyake online
3. Weka tozo kwa kila mauzo ya kitabu online
4. Fungua akaunti ya kupokea malipo ya mauzo online(collection account)
5. Weka mfumo mzuri wa malipo kila mwezi kutokana na mauzo ya vitabu kwa kila mwandishi

Mkiwa na hayo mnaweza kunitafuata tufanye biashara kwa kuwawekea app itakayo wasaidia kuuza vitabu vyenu bila kutapeliwa, kila kitu mtakuwa mnakiongoza wenyewe.

App itakuwa na sifa zifuatazo:
1. Itamsaidia mwandishi kuuza vitabu vyake online kwa kupakia mwenyewe na kuweka bei yake
2. Itamsaidia mwandishi kuona mauzo yake yote ya kila mwezi
3. Itamsaidia kujua wasomaji ni wangapi kwa kila kitabu
4. Itamsaidia kukuza kipato na kutunza vitabu vyake sehem salama bila kusambaa mitandaoni(kuongeza demand).
5. Itamsaidia kuwafikia washabiki wake wote wenye smartphone kwa haraka zaidi nchi nzima.

Kama chama kipo mnaweza kunitafuta kwa namba hii 0652247221, au kama kuna mwandishi anataka auze vitabu vyake pekeyake unaweza pia nitafuta kwa namba hiyo.

Unaweza ukauza vitabu vyake kwa mfumo wa subscription bussiness model, yaani wasomaji wanalipia kila mwezi kusoma vitabu vyote ulivyopakia kwenye app, ni njia rahisi sana ya kuuza sana kama una fans base kubwa.

Kazi kwako mwandishi...
 
Haya maelezo Ni muhimu sana, Mimi Ni mmoja ya waandishi hao wenye nia.

By Akida Siri Rambao.
 
Nitakutafuta ngoja nikamilishe mambo yangu.
 
Ukiwa kama mwandishi wa vitabu unayetaka kufanikiwa kupitia kazi yako ya uadishi, soma iki kitabu cha mwandishi mwenzako aliyeuza nakala 1 kwa watu 5M. Ukisoma vizuri hichi kitabu utaelewa idea yangu ninayotoa hapa JF kuhusu ebook business.

1644827024885.png
 
Back
Top Bottom