Mwandishi wa habari mkoani Simiyu awekwa ndani, baada ya kupost Polisi akiwa bar

Lugano5

R I P
Jul 15, 2010
4,520
755
Updates:

Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu limemwachia kwa dhamana Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru mkoani Simiyu,Costantine Mathias waliokuwa wamemshikilia tangu asubuhi kwa madai ya kusambaza mitandaoni picha ya askari wa jeshi kituo cha Mwamapalala akionekana akinywa bia huku amevaa sare.Ila bado wanashikilia simu zake zote mbili za mkononi.

Xxxxxxxxxxxx

Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru *Constantine Mathias,* anashikiliwa na jeshi la polisi Mkaoni Simiyu.

Nineongea muda huu na Mwenyekiti wa Press club ya Simiyu Bwana Mwanga pamoja na Bi Severini naye ni mwandishi wa habari wamethibitisha uwepo wa tukio hilo.

Kosa analotuhumiwa nalo ni, matumizi mabaya ya mitandao, kufuatia kupost picha ya askari polisi wa kituo cha Mwamapalala (jina limehifadhiwa) akiwa anakunywa pombe akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu ya waandishi waliopo eneo la tukio mtuhumiwa bado yupo mikononi mwa polisi na tayari amechukuliwa maelezo yanayosubiri kusainiwa na Mwenyekiti wa Press club ya Simiyu. Hatufahamu nini kitaendelea baada ya kusainiwa maelezo yake.

Tunaliomba Jeshi la polisi kumwachia mwandishi huyo kwani, kwa mujibu wa sheria ya mienendo ya makosa ya jinai (CPA)ni haki ya mtuhumiwa kupewa dhamana.

*Nakala kwa*

*RPC Simiyu,*

*IGP* ,

*Taasisi za kihabari,*

*Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania,*
 
Weka hiyo picha hapa na sisi tuisambaze kupinga tabia ya kulewa huku ukiwa kazini
 
Vitu vingine ni kujitakia.
Sasa kuweka picha ya Mtanzani mwenzako akiwa baa kwa nia ya kumdhalilisha ina tija gani kwa taifa. Au ni bifu na chuki binafsi.

Je, alifanya fujo akiwa baa?
Au
Je, alikataa kulipa pesa za vinywaji vyake?
Au
Je, uwepo wake kama mteja mwingine yoyote kulizuia haki kutendeka popote?
Au
Je, hakuwa na kampani ambayo ilikua inafurahiya uwepo wake na kunywa naye kama mtu mwingine yeyote?

Kuweka picha tu bila maelezo yoyote inaleta tafsi nyingi na mjadala mkubwa bila sababu za msingi.

Nadhani ni vizuri kama waandishi wa habari tunahubiri juu ya haki na Uhuru basi tusiishie kwetu tu Bali tuhakikishe kila mtu anakua huru katika nchi yake hata kama kuna sheria za kikoloni zinazowanyima wenzetu Uhuru tusizitumie kama fimbo ya kuwakomoa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hujaelewa! Alikuwa bar akiwa na sare za jeshi which means alikuwa kazini! Au nyie kazini kwenu mnapewa uhuru wa kwenda bar na kunywa pombe muda wa kazi! Magufuli alisema waumbuliwe hadharani,na akaonyesha mfano kwa kumtumbua mzee kabwe (Rip)
 
Back
Top Bottom